Maswali kwa Mwanakijiji na wengine wenye kufanana naye katika mtazamo wa siasa...

Mwanakijiji,wewe ni mtu wa media sioni tofauti na Pasco mzee wa vibahasha.
Huko ulipo unaweza ukawa unakula vibasha vya kutosha ukija bongo ndiyo usiseme.
Waandishi wa habari wa Afrika ni bendera fuata Pesa tu.

MMM ni sehemu ya Watanzania wachache sana wenye uwezo mzuri wa uchambuzi wa mambo ya kisiasa, amekuwa msaada mkubwa kwa wanasiasa wengi, hata mimi amenisaidia sana kupata ujuzi wa kuziangaza siasa za kiswahili.

Kama tulivyo binadamu, Mwanakijiji nae ana matatizo yake, na hili ni sehemu ya tatizo tajwa,
 
Last edited by a moderator:
Ikiwa hutumii akili yako utaamini kila liandikwalo hapa jf,

Umbeya na uzushi huu ni wa tangu 2005, leo tupo 2013,

Akili yako haizinduki tu dada?

Dhambi ni dhambi tu. Iwe imefanyika leo, jana, juzi, majuzi, mwaka uliopita, miaka iliyopita, karne iliyopita. Hubaki kuwa dhambi tu.
 
Binafsi ningemshauri asifanye mkutano wowote hivi sasa hadi hatima yake ndani ya CDM iamuliwe.


Mkuu MMKJ;Mwisho wa siku si uzushi tena, ni kweli Zitto kafanya Mkutano wa hadhara Kigoma.

Na ili kuendeleza mapambano aliyoyaanzisha ya Mkakati wa Mabadiliko ambao akina Dr.Kitila wamejaribu kumsafisha Zitto lakini mwenye akili anafaa asome mabango yaliyoshikwa kwenye hizi picha hapo chini.
News Alert: Picha,Zitto atikisa





Na hiyo haitoshi hotuba yake inatoa mwanga wa nini anaota/taraji/anaamini!


Je Uhuru wa mawazo bila Kanuni ?


Kama hatuwezi kujenga vyama vinavyorutubisha uhuru wa mawazo na tofauti za mawazo, tutajenga Taifa lenye watu wenye kuogopa na waliojaa woga.
Wanachama wanapoogopa uongozi ni udikteta, lakini uongozi unapoogopa wanachama ni demokrasia. Bila demokrasia ya uwazi na kuvumiliana tutakuwa Taifa la kidikteta. Lazima vyama vya siasa, viongozwe kwa namna ile ile ambayo Taifa litaongozwa.


Maelezo/maneno haya hapa chini !!!!!!!!!!. Je unafaa kumwamini mtu wa aina gani na kumvumilia wa aina gani kama binadamu?


Demokrasia bila kuaminiana, demokrasia bila kuvumiliana sio demokrasia ya kweli.





Hili nalo neno! na inahitaji mfumbuzi!


Juzi nilipoingia Bungeni kwa mara ya kwanza baada ya matukio kadhaa yanayoendelea ndani ya chama chetu nilikaa pamoja na mbunge Tundu Lissu. Wabunge wengine walidhani tutarushiana ngumi na badala yake ikawa ni vicheko na mazungumzo. Hii ni kwa sababu sina chuki na mtu yeyote yule. Mmenifunza kutojenga chuki na watu na badala yake kuchukua kila tukio kama changamoto ya maisha. Siasa ni kupambanisha mawazo tofauti na hatimaye kutafuta suluhu ya pamoja. Na siasa ina misingi yake ambayo sisi wanasiasa huwa tunasahau kwa maksudi. Msingi wa siasa ni kuwa inapaswa kuleta unafuu wa maisha ya wananchi na sio malumbano tu ya kurushiana maneno na kuzushiana ili kujijengea umaarufu wa kisiasa. Siasa si kuwekeana chuki na kuonyeshana ubabe.

CC Yericko Nyerere Mzee Mwanakijiji
 
Pasco
wewe ni kiona mbali na tena unatumia Darubin kali
zitto hawezi kusubiri maamuzi ya cc kwa sasa,yeye ni mbunge na waliomchagua wengi hawakuwa na vyama na anahaki ya kuongea na wapiga kura wake,
niungane na wewe kuwa,maamuzi ya cc yapo wazi na hata ukiwasikia wanapozungumzia swala hili la akina zitto na ukiwaangalia vizuri usoni unagundua kuwa hakuna litakaloweza zuia SUNAMI lililoandiliwa na binadamu,ni kwamba zitto yawezekana kuvuliwa uanachama na ubunge ndio ukapotea,lakini bado anaweza kuweka pingamizi la kisheria mahakamani na akaendelea kuwa mbunge kupitia mahakama na si chama tena,hapo atakuwa na uwezo wa kuendelea kuongea na wapiga wake.
lakini kwa sasa,kwakuwa panga bado halija tangazwa la kumvua uanachama,inamaana bado ni mbunge na ni mwanachama wa cdm na anahaki ya kuongea na wapiga kura wake kama mbunge.
cha msingi ni yeye zitto kutokukiweka chama ktk wakati mgumu sasa kama cc ilivyomfanyia yeye,kwani kikawaida,waswahili wanasema usilipize ubaya kwa ubaya.ni mategemeo yetu kuwa zitto ataongea na wapiga kura wake juu ya maendeleo ya eneo husika na mambo mengine na kama wapiga kura watahitaji msimamo wake juu ya kilichotokea,ni wazi kuwa zitto ni mwelewa na atakuwa na majibu mazuri yasioweza kusababisha chama chake kuwa ktk wakati mgumu
Zitto atafukuzwa hata akienda kuongea na wananchi ama vyovyote vile na ndo maana anakimbilia mahakama. Huu ni muda zile pesa na magari vinamtokea puani
 
Majibu ya maswali haya ameyajibu Zitto kupitia agizo la mahakama na ukweli wa katiba ya Chadema
 
Back
Top Bottom