Nduka
JF-Expert Member
- Dec 3, 2008
- 8,553
- 2,374
Natarajia kwenda kumuona bwana Mnyika nyumbani kwao Kimara ikiwa ni kumjulia hali na kubadilishana naye mawazo baada kipindi kirefu kupita (mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2005). Kwakuwa humu kuna wakazi wa jimbo la Kibamba ambao wangependa kusikia kitu kutoka kwa mbunge wao, na pia watanzania wanachama wa CHADEMA ambao wangependa kusikia kitu kutoka kwa kiongozi wao, natoa fursa kwa yeyote mwenye swali aniandikie hapa na mimi nikimkuta hali yake inaruhusu nitamuuliza na kuleta majibu hapa. Hii ni katika kusaidiana tu.