Maswali kwa bashe dhidi ya mgombea wake.

Maswali kwa bashe dhidi ya mgombea wake.

Kichale

Member
Joined
Mar 12, 2015
Posts
16
Reaction score
7
SWALI
Nicodemad Tambo (kimeta wa mpui );
1. HAUONI KAMA MGOMBEA MNAYEMNADI NA MARAFIKI ZAKE WANA TASWIRA YA UFISADI..?

JIBU
HUSEIN BASHE: Kwanza nianze na UFISADI, Taswira ya Ufisadi ni taswira ya CCM whether ina ukweli ama haina imeishakuwa Taswira ya chama kizima,kila kiongozi wa chama chetu anatuhuma ya Ufisadi whether ya ukweli ama ni uongo,

hakuna ambae hana Tuhuma kwahiyo hakuna kiongozi mwenye "Moral Authority "ya kumnyooshea Kidole mwingine Kuhusu tuhuma za Ufisadi so huu ni mtego ambao sisi kama wana CCM tulikubali kuingia tukidhani tunamaliza mtu flani ama watu flani ni kama Historia ya WW1 askofu ambaye alikua Protestant. Aliposema

"When they come after catholic I did nothing bcs I was not catholic,when they come after gays I did nothing bcs I was not gay,when they come after Muslim I did nothing bcs I was not moslim,when they come after women I did nothing bcs I was not a women,when come after me there was no body to help"

Hoja Ufisadi ilianza kumtafuna mmoja mpaka ilipokigeukia chama na sasa hakuna aliesalama. So si Amini ktk Hoja Hii na CCM ikiendekeza Hoja Hii tukubaliane Kuwa 2015 hatuna Mgombea kwakua sote ni mafisadi na Hakuna ambae hana Tuhuma ya UFISADI.

SWALI
Nicodemas Tambo (kimeta wa mpui);
2.HUONI KAMA UMEJITWISHA MZIGO KUMNADI LOWASSA..?

Jibu
HUSEIN BASHE:
Kujitwisha mzigo wa Kumnadi lowassa,Huu si mzigo na si mzigo mzito katika wagombea ambao naamini Kuwa ni Rahisi kumnadi Lowassa ni mmoja,na Hakuna uzito wowote katika kumuuza

SWALI
Nicodemas Tambo (kimeta wa mpui );
3. JE JUKUMU LAKO LA KUMNADI LOWASSA LINAGHARAMA KUBWA KIASI GANI...?

JIBU
HUSEIN BASHE:
hapana jukumu hili Halina gharama kubwa kabisa kwasababu nashiriki kumnadi mgombea ambae anakifahamu chama chake anaifaham Nchi yake ,anafahamika miongoni mwa wana CCM,nje ya CCM ana Track record watu watampima kwa matendo yake wanayoyafahamu ameacha alama Chanya na Hasi

" Hasi kama Binadam" na hapa kama mwana CCM nitampima je Anasifa za Kuwa mwenyekiti wangu wa chama? Jibu NDIO anafaham Historia, madhumuni, Malengo ya chama chetu? Jibu Ndio na katika jamii aloitumikia huu si mzigo mzito kabisa kwahiyo sijaona Gharama kubwa unayoiona ww....miongoni mwa wagombea Rahisi kabisa kuwanadi ni EL bcs ana Historia ya kupimika na nina Amini Alama chanya alizoaacha ktk Jamii zina Uzito kuliko mapungufu yake,
Na ni mgombea pekee ambae Hakumbati JOHO la UMASKINI kama Sifa ya Kuwa Kiongozi.

SWALI
Nicodemas tambo (Kimeta Mpui);
4. JE ENDAPO HATOPITISHWA ATAHAMA CHAMA..? JE NANYI MTAHAMA DHULMA IKITOKEA..?

JIBU
HUSEIN BASHE:
Kwanza nikuhakikishie chama chetu kina viongozi Makini ambao hawako tayari kuona Dhulma inachukua nafasi, wanahistoria ya Kuumizwa kwa kutotendewa haki huko Nyuma,

naamini wanafahamu machungu ya Dhulma becouse they happen to victims huko nyuma, Mwaka 2002 mpaka 2005 Ndg Mwenyekiti wetu alipitia haya haya ambayo leo EL anapitia na zanzibar katika kikao cha NEC/CC aliwahi ku protest openly juu ya Faulo anazochezewa, mwaka 2005 mzee Sozigwa na Mzee Mangula walioandaa Mafaili kama haya haya ambayo leo yanaandaliwa dhidi ya wagombea wengine lakini Busara za Mzee Mkapa kusimamia Haki ziliweza kuchukua Nafasi....

Ndg Kinana aliwahi kudhulumiwa ndani ya chama hiki anayajua Machungu ya Dhulma na Madhara ya kusimamia dhulma, Naamini watasimamia Haki na Haki inasifa kuu (1)Itendwe kwa wakati (2)Itolewe kwa wakati (3) Ina wajibu wa kutolewa kwa mlengwa.
Kwahiyo kwakua HAKI inasimamiwa na ikikosekana CC itapatikana NEC ikokosekana NEC itapatikana Congress. Ikikosekana Congress Itapatikana kwa UMMA.

"Hakuna mwenye Mpango wa kuhama chama EL hakuhama dhulma ya 95, hakuhama 2008, hakuhama alipotukanwa na kuitwa gamba"

Hii Hoja ya kuhama si mpya ndani ya Politics za CCM 2005 walisema JK atakatwa na atahama na wanaoibeba leo ndo wale wale walibeba dhidi ya JK 2005 ,i belive Kuwa 2015 will be the same

nikuhakikishie CCM inafahamu Madhara ya kukumbatia dhulma hakuna atakae hama na Haki itapatikana na.

Tumesikia wengine wanasema Kuwa CCM haitapitisha mwenye Tuhuma kama tuhuma ndo msingi wa maamuzi CCM inatuhumiwa Kila kona..je tumekosa Uhalali mbele ya watanzania,je Kila anaetuhumiwa anakosa Sifa..?
Viongozi wa kisiasa Hutuhumiwa na Tuhuma pekee si kigezo bali Ushahidi.

kumekua na Tabia ya kutumia maneno ya Baba wa Taifa through mfano wa mke wa mfalme alietuhumiwa kuzini, huu nauita UTUMWA WA HISTORIA....this generation haitakua watumwa wa Historia ukweli ndo Msingi wa kufanya maamuzi na Haki ni mzizi.

Majadiliano Baina Ya Makada Wawili wa Ccm Katika Kuangalia Bashrafu ya Uchaguzi Mkuu Wa CCM
 
Naomba umpelekee swali hili Bashe: Je ni kuwa hakuna rushwa?
 
Back
Top Bottom