Maswali kibao juu ya Tego| Password

Maswali kibao juu ya Tego| Password

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,508
Reaction score
13,974
Habari za mchana wa leo?

Katika siku hizi kumekuwapo na tatizo SUGU sana la usaliti hasa kwa walioko kwenye mapenzi/mahusiano.Wengi hupenda kuita michepuko au nyumba ndogo.kidumu nk

Kuna jamaa yangu yupo Kigoma ameniambia kuwa kuna mtaalamu wa kuweka TEGO a.k.a PASSWORD hii inasema itanisaidia kujua mwizi wangu wa mke wangu kama ifuatavyo:

#1 .Ipo dawa ya kutega ili niweze kumkata mwizi wangu wangu IKIWA anatembea na mke wangu,hii inamaanisha watang'ang'aniana.

#2 .Ipo dawa ya kufanya mtu akose NETWORK/HISIA za mapenzi pindi watakapo kuwa faragha na huyo mwizi/dowezi

#3 .Ipo dawa ya kutegana wote wawili kila mtu kutokuwa na mawazo ya kuchepuka,na ikitokea kuchepuka niliyotaja hapo juu,moja laweza kutokea.

Nimejiuliza maswali kadhaa je vipi kuhusu imani yangu? Nimejipa moyo wa kufanya hilo kwani hata Mungu hapendi wezi,alisema hayo kupitia maandiko yake,pia hapendi na Uzinzi nk.

Wadau jamaa anazidi kunishauri niende akanipe hiyo dawa BURE,na anasema inachukua chini ya dk5 kukamilisha zoezi.
Sina shaka na my wife ila dunia ya sasa inapelekea kufikiria tahadhari ni bora.

Wadau naomba mawazo yenu juu ya wito wa jamaa yangu wa kwenda Kigoma kufuata tego a.k.a password.
 
nendo mkuu tupate news kwenye media. si umesikia huko kagera police wanapiga mabomu haspitali kuzuia watu wasiende kushuhudia watu waliogandana?
 
Hebu nielekeze niende... mi ila nataka mwizi akimsogelea swirl hanibo tu anuke mavi gafla
 
Shida ya hizo password za Kigoma ni hi, inaruhusu kuingia ila kutoka ndio inabidi uwe na password, so haizuii kuibiwa cause utakua umeisha ibiwa na utamkamata mwizi akiwa kaisha IBA, swali JE? Utamuacha mkeo? Umesema we ni mtu wa maandiko, hivi maandiko si ndio yanazuia kuachana? Na pia nadhani maandiko yanazuia kwenda kwa hao watu!?

Mkuu, ndoa za wazee wetu zilikua zinadumu kwa vile walikua hawapelelezani sana, mzee akirudi toka safari anapiga story kwa majirani weeeee, tena kwa sauti kubwa ili kama kuna mwizi wake atokee hata dirishani, jifunze hiyo mkuu, mambo ya password achana nayo, kumdahlilishia wife sio kabisa!
 
Kama nilivyoeleza hapo juu jamaa ameniambia kuna aina kadhaa za password/tego kwa hiyo mimi nitachagua ila ya kuzuia,kabla mwizi hajafanya uharibifu apoteze network/hisia (dushe lilale lisiwe na uhai tena hapo eneo la tukio,ila akifika home kwake dushe linaweza kufanya kazi)
Maandiko yanasema kila mtu alinde mali zake,ndio maana hata makanisani/misikitini kuna milango yenye kufuli,pamoja na walinzi hiyo yote ni kuimarisha ulinzi,dawa itakayotumika ni ya miti shamba kwa hiyo bado naamini itakuwa si kosa kiimani.

Shida ya hizo password za Kigoma ni hi, inaruhusu kuingia ila kutoka ndio inabidi uwe na password, so haizuii kuibiwa cause utakua umeisha ibiwa na utamkamata mwizi akiwa kaisha IBA, swali JE? Utamuacha mkeo? Umesema we ni mtu wa maandiko, hivi maandiko si ndio yanazuia kuachana? Na pia nadhani maandiko yanazuia kwenda kwa hao watu!?

Mkuu, ndoa za wazee wetu zilikua zinadumu kwa vile walikua hawapelelezani sana, mzee akirudi toka safari anapiga story kwa majirani weeeee, tena kwa sauti kubwa ili kama kuna mwizi wake atokee hata dirishani, jifunze hiyo mkuu, mambo ya password achana nayo, kumdahlilishia wife sio kabisa!
 
Habari za mchana wa leo?

Katika siku hizi kumekuwapo na tatizo SUGU sana la usaliti hasa kwa walioko kwenye mapenzi/mahusiano.Wengi hupenda kuita michepuko au nyumba ndogo.kidumu nk

Kuna jamaa yangu yupo Kigoma ameniambia kuwa kuna mtaalamu wa kuweka TEGO a.k.a PASSWORD hii inasema itanisaidia kujua mwizi wangu wa mke wangu kama ifuatavyo:

#1 .Ipo dawa ya kutega ili niweze kumkata mwizi wangu wangu IKIWA anatembea na mke wangu,hii inamaanisha watang'ang'aniana.

#2 .Ipo dawa ya kufanya mtu akose NETWORK/HISIA za mapenzi pindi watakapo kuwa faragha na huyo mwizi/dowezi

#3 .Ipo dawa ya kutegana wote wawili kila mtu kutokuwa na mawazo ya kuchepuka,na ikitokea kuchepuka niliyotaja hapo juu,moja laweza kutokea.

Nimejiuliza maswali kadhaa je vipi kuhusu imani yangu? Nimejipa moyo wa kufanya hilo kwani hata Mungu hapendi wezi,alisema hayo kupitia maandiko yake,pia hapendi na Uzinzi nk.

Wadau jamaa anazidi kunishauri niende akanipe hiyo dawa BURE,na anasema inachukua chini ya dk5 kukamilisha zoezi.
Sina shaka na my wife ila dunia ya sasa inapelekea kufikiria tahadhari ni bora.

Wadau naomba mawazo yenu juu ya wito wa jamaa yangu wa kwenda Kigoma kufuata tego a.k.a password.

angalia usije ukammilikisha jamaa mkeo pasi na kujua aseee nakonea huruma
 
Muwekee software ya kutrack maongezi yake kwenye simu na GPS kwenye simu.

Itasaidia sana

Mimi nakula full updates hapa kwenye mail yangu
 
Taaluma ya bure kwa wanaohitaji, kwa wale wanaotumia simu za androids, nenda google play, kwenye sehemu ya search andika neno "sms forwarding", hii kitu ni free kabisa hakuna kulipia, nilimdaka x wangu kupitia njia hii, download hiyo program kwenye simu yake bila yeye kujua, kisha download program nyengine inaitwa "apps lock" ili kuifunga sms forwarding ashindwe kujua nini kinaendelea kwenye simu yake, sms forwading unapoingiza namba yako tu ya simu kwenye hiyo programu itaanza automatically kutuma meseji zote zinazoingia na kutoka kwenye hiyo simu kuja kwenye simu yako, na itakuonyesha namba mtu aliyetuma meseji na aliyetumiwa meseji kama una moyo mdogo unaweza kuvunja simu yako kwa hasira, wanawake si wa kuwawekea muamana, ushauri kama unampenda sana mkeo usije ukajaribu njia hii, ndoa yaweza sambaratika ndani ya sekunde tu. NI HATARI SANA.
 
presha zote za nini hizo! life should be simple and we should live as free as electrons.....you just have to play your part...hayo mengine God will always be in control!
 
Usimuwekee mkeo mtego wa kumfumania mkeo kama huna uwezo wa kumuacha
 
Kama nilivyoeleza hapo juu jamaa ameniambia kuna aina kadhaa za password/tego kwa hiyo mimi nitachagua ila ya kuzuia,kabla mwizi hajafanya uharibifu apoteze network/hisia (dushe lilale lisiwe na uhai tena hapo eneo la tukio,ila akifika home kwake dushe linaweza kufanya kazi)
Maandiko yanasema kila mtu alinde mali zake,ndio maana hata makanisani/misikitini kuna milango yenye kufuli,pamoja na walinzi hiyo yote ni kuimarisha ulinzi,dawa itakayotumika ni ya miti shamba kwa hiyo bado naamini itakuwa si kosa kiimani.

maaniko pia yanasema AMELAANIWA YULE AMTEGEMEAE MWANADAMU kutegemea msaada wa mganga ni chukizo kwa Mungu, maandiko hayao hayo yanasema MIMI NI BWANA MUNGU WAKO USIABUDU MIUNGU MINGINE unganga na uchawi ni ibada kwa miungu..kaka kama wafata maandiko yafate yote na si yale tu yanayokupa kile utakacho
 
Taaluma ya bure kwa wanaohitaji, kwa wale wanaotumia simu za androids, nenda google play, kwenye sehemu ya search andika neno "sms forwarding", hii kitu ni free kabisa hakuna kulipia, nilimdaka x wangu kupitia njia hii, download hiyo program kwenye simu yake bila yeye kujua, kisha download program nyengine inaitwa "apps lock" ili kuifunga sms forwarding ashindwe kujua nini kinaendelea kwenye simu yake, sms forwading unapoingiza namba yako tu ya simu kwenye hiyo programu itaanza automatically kutuma meseji zote zinazoingia na kutoka kwenye hiyo simu kuja kwenye simu yako, na itakuonyesha namba mtu aliyetuma meseji na aliyetumiwa meseji kama una moyo mdogo unaweza kuvunja simu yako kwa hasira, wanawake si wa kuwawekea muamana, ushauri kama unampenda sana mkeo usije ukajaribu njia hii, ndoa yaweza sambaratika ndani ya sekunde tu. NI HATARI SANA.
kama wanatumia voice call kama njia ya maongezi? or social netwrk kama viber, whatsapp n etc
utafanyaje kujua? bora muaminiane tu
 
Back
Top Bottom