Maswali juu ya mchezo wa NGUMI (boxing )

Maswali juu ya mchezo wa NGUMI (boxing )

Mkalibari

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2012
Posts
659
Reaction score
400
Jamani naomba kuuliza kuhusu huu uzito wa haya mapambano ya ngumi

KUHUSU UZITO.
Heavyweight, middle weight light weight na uzito mwengine? Wanatumia vipimo gani mpaka kujua huu ni uzito wa juu na huu ni uzito mwengine?

KUHUSU UBINGWA.
hua nasikia kuna bingwa wapi sijui mwingine yuko nchi
Gani huko lakini kila mtu anajitapa ni bingwa wa dunia, sasa nini kinafanya kuwe na mabingwa wa dunia ktk angle tofaut tofaut.

KUHUSU UZITO
hivi vipimo vya uzito wa kupigana na mwenzio vinatakiwa visizidiane kwa kiasi gani?

KUHUSU TYSON NA MOHAMMED ALLI
hivi ktk hali ya kawaida nani apaswa kua mfalme wa hizi boxing maana kwa mtazamo wangu Tyson alikua ni mkali sana japo ni wapiganaji ktk nyakati tofauti

KUHUSU MAY 2
hivi karibuni mwezi mei tarehe 2 kuna pambano kubwa na la kihistoria kati ya may weither vs Pacquiao, nimeaangalia clips nyingi YouTube za hawa jamaa nimewaona ni wakawaida sana ukilinganisha na akina Tyson na mudi Ali, sasa kwann hawa jamaa wamechukua attention ya media kiasi hiki? Kwanza mbavu zenyewe hawana wala nini, ni vijamaa vidogo vidogo na nikama vyote viwili ukiviunganisha una pata Evander mmoja.

Naomba kusaidiwa hayo maswali yangu kwa anaefaham vyema huu mchezo!
 
Mohamed Ally Alikuwa Kiboko Zaidi Ya Tyson Record Yake Amepgwa Na Mtu Mmoja Tu Na Hapo Hapo Akastaafu
 
Mohamed Ally Alikuwa Kiboko Zaidi Ya Tyson Record Yake Amepgwa Na Mtu Mmoja Tu Na Hapo Hapo Akastaafu

Kwahyo ukali unapimwa kwa kushinda na kushindwa tu au kuna vitu vingine? Basi kama ndo hivyo kuna huyu jamaa anajiita jafet kaseba nae ajiuzuru maana anapigwa kila siku...

Alafu mkuu nao unisaidie na hayo majibu mengine basi
 
Mohamed Ally Alikuwa Kiboko Zaidi Ya Tyson Record Yake Amepgwa Na Mtu Mmoja Tu Na Hapo Hapo Akastaafu

Kijana, Ebu Wacha longo longo! Mohammed Ali aligongwa na miamba hii: 1. Joe Frazier 2. Ken Norton 3. Leon Spinks 4. Larry Holmes na 5. Trevor Berbick.
 
Kijana, Ebu Wacha longo longo! Mohammed Ali aligongwa na miamba hii: 1. Joe Frazier 2. Ken Norton 3. Leon Spinks 4. Larry Holmes na 5. Trevor Berbick.

Kumbe jamaa alikua ametudanganya
 
Back
Top Bottom