Maswali haya kuhusu ikulu na lema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali haya kuhusu ikulu na lema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mu-sir, Apr 5, 2012.

 1. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  wakuu ninajiuliza maswali haya kuhusu ikulu na kesi ya mheshimiwa Godbless Lema.
  Ikulu imekuwa ikikaa kimya sana mara nyingi au kujibu kwa kuchelewa sana inapoelekezewa shutuma mbalimbali juu ya maswala mbalimbali yahusuyo Taifa kwa ujumla wake.
  Mfano;
  Swala la Dowans na mmiliki wake, Swala la kutoroshwa kwa Twiga kutoka katika hifadhi zetu, Swala la ugonjwa wa Dr. Mwakyembe, Swala la mgomo wa madaktari na kadhalika. Haya ni mfano tu wa maswala machache ambayo kipindi yanahojiwa na wananchi yahlihitaji attention ya Ikulu na mheshimiwa Rais kutoa public statement haraka ilivyowezekana kwa nyakati hizo yalipoibuka na tena yalikuwa na interest kubwa kwa taifa kuliko hili suala la mh. Lema.
  Sasa ajabu ninayoiona ni hii. Leo Lema akihojiwa redioni ametoa shutuma moja kwa moja kuwa Ikulu na mhe. Rais wamehusika katika mwenendo wa kesi na hukumu. Kwanini Ikulu imelijibu hili swala kwa uharaka hivi? Je, lilikuwa na public attention kubwa kuliko hayo mengine? Yaani statement intoka saa tano saa kumi tayari tuna response ya ikulu mbona haijawahi kutokea hivi? Au madai ya Lema yana ukweli fulani kuhusu hili swala?
  Haya ni mambo ambayo ninajiuliza na naomba mwenye uelewa zaidi anieleweshe but I think there is something that the ikulu had done to influence the judgement. You are welcome great thinkers.
   
Loading...