Maswali ambayo sijapata jibu kwenye kona iliyozaa goli kwenye mechi ya Liverpool na Barca

Baba Mtakatifu

JF-Expert Member
Dec 31, 2017
1,324
2,435
Ukiangalia kwa haraka haraka Huwezi ona cha ajabu, Ila ukitathmini kwa kina utatoka na maswali mengi tu .

Kipindi ile kona inataka kupigwa kwanza kulikuwa na mipira miwili uwanjani, wakati mmoja unatolewa wakati huo huo mchezaji ambae alikuwa kwenye ile position ya kupiga kona (Alexender Anorld)akawa anaondoka ili mchezaji mwingine aje apige(Shakiri), wakaki huo huo Shakiri akiwa anatazama chini akawa anaelekea kupiga ile kona.

Wakati huo si wachezaji wa Liver wala wa Barca waliokuwa tayari wamejiandaa kucheza kona ile maana mpigaji ndio alikuwa anaelekea kwenda kupiga.

Mara ghafla yule mchezaji aliyekuwa anaacha kona aje apige Shakiri Mara akarudi ghafla huku akiwa hajajiandaa akaipiga ile kona Kama vile anatoa pass , ambayo ilimkuta Origi ambae alikuwa katikati kabisa na kufunga goli rahisi.

Maswali amabayo sijayaptia majibu ni haya:-

1 - Alexander Anorld alijiamini vipi mpaka kupiga ile kona kivile huku akiwa hajajiandaa, Jee ile kona ingetoka nje , au ingezuiliwa na wachezaji wa Barca na kuokolewa, ukizingatia sehemu ya kupiga kona na alipokuwa Origi pana umbali na kuna kundi la wachezaji walikuwepo.

2-Hakuogopa kulaumiwa na wenzake endapo ingefeli, maana Shakiri alikuwa anaenda kuipiga kabla hata hajafika yeye akaipiga tena kwa uharaka bila umakini wowote.

3- Je Origi alijuaje kwamba jamaa atarudi na kuipiga ile kona na kumpasia yeye, kiasi akajiposition vizur paka ikamkuta yeye na kufunga, wakati wenzio wote bado hawajajiandaa...je kulikuwa na mawasiliano kati yao..

Maswali ni mengi Ila kweli mpira una ma ajabu yake
 
Kama unamjua Arnod Vizuri ni mtu ambaye haitaji maandalizi yoyote pale anapopiga cross,miguu yake imezaliwa hivyo anauwezo wa kupiga mpira vyovyote anavyotaka
 
Muda mwingine akili inakutuma tuu ufanye hivi.
Kama uliangalia vizuri. TAA alikuwa anaondoka lakini Kama alikuwa anapanga kitu kichwani. alirudi ghafla baada ya kutoka kuangalia chini na kumcheki origi yupo free na barca wamezubaa.. halafu cha ajabu alipiga pasi ya chini! 😂😂😂

Ndo kawaida yake yule mtu
 
Alisema mwenyewe nia ilikuwa ni kumuacha shakiri apige kona ila wakati anaondoka akamwona origi anamkonyeza palepale akarudi akatoa pasi goli likaingia..

Kwenye soka huwa hamna kitu kuogopa lawama kupata ama kukosa ni matokeo tu....
 
Mim kama refaa lile goli nalikataa hadharani

Unapiga vip kona bila watu kujiandaa???

Ule ni uhuni wa hali ya juuu
 
Wakati anaweka mpira kwenda kupiga kona akawa anauacha na uangalie kulikuwa na Ball Boy upande wa kulia kwake wakati anatoka Ball Boy akamtonya kuwa Origi yuko peke yake piga mpira haraka na kama hujui huyo Ball Boy Kapewa tiketi na Anold ya kwenda kushuhudia mpambano wa fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya na kama hiyo haitoshi LIVERPOOL wamempa ruhusa ya kuangalia mechi zote za mpira kwenye maisha yake zinazoihusisha Liverpool kwa kitendo chake cha kumwambia Anold.
 
Back
Top Bottom