Maswali 3 kwa Watanzania na wana CCM Wazalendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali 3 kwa Watanzania na wana CCM Wazalendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, Apr 16, 2011.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu waTZ na wana CCM wapenda maendeleo naomba mnisaidie kuyajibu maswali haya ya msingi ili taifa letu liweze kusonga mbele na kufika pale tunapopataka.

  1. Kuna majigambo ya siku za karibuni, hasa kwa viongozi wengi wa CCM wasioipenda nchi yetu wakidai lengo lao ni kumaliza ufisadi, hivi kwa nini mpaka watanzania wawanyime kura na kuwazomea kila mahali ndio wakubali kwamba kuna mafisadi wanaimaliza nchi hii? Hivi kwa nini wamechukua muda mrefu (4years) kukubali kwamba RA, EL, AC na wengine waliotajwa kwenye list of shame ni wezi wakubwa, wala rushwa wakubwa na mafisadi mapapa? Au kwa sababu waTZ waliitosa kwenye uchaguzi wa mwaka jana na kuhofia kwamba watakola ulaji milele inchi itakapochukuliwa na watu wema?

  2. Je tujiulize ni kweli RA, EL, AC wametoswa au walibembelzwa kuachia madaraka ndani ya Chama ili kuwahadaa watanzania? maana nawaona bado wapo wengi ambao ni mafisadi wakubwa lakini hawafanywi jambo lolote na wanaendelea kuitafuna mali ya nchi hii mfano ni waliotachukua pesa za EPA hadi leo wapo na wanajivinjari mitaani na maVX V8 za serikali.

  3. Ni kwanini CCM imekuwa ikiwahaa watanzania? kwa mfano katika muswada wa kutunga katiba mpya ni wazi kwamba CCM haina lengo zuru na mchakato wa waTZ kupata katiba mpya mfano ni pale Tambwe Hiza, Kamati ya sheria na UVCCM walipopandikiza mamluki wa kwenda kuwazomea watu wanaotoa michango inayoenda kinyume na mswada. Mbaya zaidi ni pale bungeni waliposikia muswa umeahirishwa wabunge wa CCM walianza kupiga makofi na kuimba CCM,CCM hivi wanafikiri lngo lao lilikuwa kuahirisha ule mswada au upite bila kupingwa? Au bado wanafikiri huo usanii wao hatuuelewi, nadhani wabunge wengi wa CCM wanashindwa kusoma alama za nyakati.

  PEOPLES POWER
   
 2. s

  smz JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili la muswada huu wa juzi, hakuna mwenye akili timamu ambaye hajui kwamba CCM walikuwa wanaupigia chapuo upite kama ulivyoletwa. Isingekuwa nguvu ya umma inayoongozwa na CDM kweli wangepitisha yale madudu yote.

  Nilimshangaa mama Kilango malecela eti anasema kwa uchungu: mara kuisifu serikali eti ni sikivu imesikia kilio cha wa TZ. Sina uhakika mama Malecela alichangia nini kwenye huo mswada, hata kama hakupata nafasi sina uhakika msimamo wake ulikuwa upi. Lakini kwa ninavyowajua ccm lazima angeunga mkono asilimia 100 kama wenzake wote wa ccm walivyounga mkono.

  Wanamdanganya nani sasa hivi wananchi wanaelewa mambo kuliko hao wabunge wa ccm wanaoshinda wamelala humo mjengoni - Capt Komba kama mfano wa hivi karibuni.

  Mama Kilango nilikuwa namuamini kwa upambanaji. Sitaki kuamini kwamba ghafla hivyo akili yake imeishiwa uwezo wa kupambanua mambo. Siyo kweli kuna kitu hapa. Achana na pesa mangi!!. wabunge wengi wa ccm wanajua fika kwamba wanawakilisha mawazo ya ccm, wala si ya kwao wala ya waliowatuma, aibu kubwa. Ila wakae wakijua idadi yao itazidi kupungua 2015 na wasishangae wakijikuta wamekuwa chama cha upinzani. Ushauri wangu wa bure, sitaki pesa!!
   
 3. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  CCM wote mavuvuzera tu hakuna wa kumfunga paka kengere hapo.
  Anna Kilango keshapigwa mrungula katuliza wenge.
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wanatudanganya sana watz,hembu fikiri ngeleja anawaambia wabunge mgodi wa kiwira umeshachukuliwa na serikali,kumbe mgodi upo rehani benki.na hasemi au kuomba msamaha kwa kudanganya wananchi
   
Loading...