Maswa wagomea Mkoa Mpya Wa Simiyu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswa wagomea Mkoa Mpya Wa Simiyu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMA POROJO, Jun 15, 2012.

 1. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  [h=2]source: kwanzajamii[/h]
  WANANCHI wa wilaya ya Maswa katika mkoa mpya wa Simiyu wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuiondoa wilaya hiyo katika mkoa huo mpya ili wabaki katika mkoa wa zamani wa Shinyanga kwa madai kuwa hawakubaliani na uamuzi wa makao makuu ya mkoa huo kupelekwa wilayani Bariadi.

  Wakizungumza jana mjini Maswa walisema kuwa wameamua kuchukua uamuzi huo kufuatia serikali kutozingatia vigezo vya mahali ambapo panafaa kuwa makao makuu ya mkoa huo mpya na badala yake imetumika rushwa na ubabe chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.

  “Sisi wananchi wa wilaya ya Maswa hatuko tayari kuwa miongoni mwa wilaya zinazounda mkoa mpya wa Simiyu na hivyo hatuwezi kushirikiana na wananchi wa wilaya ya Bariadi katika kuujenga mkoa huo kwani kila mara wamekuwa wakitubeza na kutudhihaki kuwa sisi ni maskini na ni lazima makao makuu yawe wilayani kwao jambo ambalo limetimia,” .

  Waliendelea kueleza kuwa licha ya kulalamika mara kwa mara juu ya ubabe uliotumika katika mchakato wa kupendekeza makao makuu ya mkoa huo katika kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa wa Shinyanga (RCC), hawajapatiwa majibu yoyote na Waziri Mkuu.

  “Serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu tumeilalamikia juu ya ubabe uliofanywa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Yohana Balele, uliofanyika wakati wa mchakato wa kupendekeza makao makuu ya mkoa huo katika kikao cha RCC lakini hadi sasa hakuna majibu yoyote yaliyotolewa juu ya malalamiko yetu,”
   
 2. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kwani wanyantuzu sio wasukuma?
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  ah..kila mtu hii nchi anagoma ttafika kweli??
   
 4. T

  Tenths Senior Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kiukweli Maswa ilikuwa na vigezo vingi vya kuifanya kuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Simiyu ikilinganishwa na Bariadi iliyopewa heshima hiyo.
   
 5. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  inategemea mkoa wa semiyu kwa ujumala naufahamu kwa undani sana na kwa kifupi location ya mkoa ulipo sio mbaya kuwa bariadi kwa kuwa bariadi ni mji uliojengwa kisasa sana ukilinganisha na maswa, pili kutoka na wilaya zingine kama busenga nivingumu kuamini kama wangeweka maswa watu wa busenga wangenyanyasika sana kuja mkoani. kwa kifupi maswa haina chakuishawishi serikali kuweka makao makuu ya mkoa pale.
   
 6. magosha

  magosha JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  maamuzi yako kwenu nyinyi wana simiyu wenyewe kaeni chini mlitafakari hilo.
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mara ya mwisho umefika lini Bariadi....? Maswa ndiyo iliyo izaa Bariadi, Meatu lakini haiendelee kivile.. acha yapelekwe Bariadi...hebu angalia hata location ilipo Maswa pamoja na wilaya zinazounda mkoa wa Simiyu!
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  serikali za majimbo ndilo suluhisho la maendeleo ya nchi yetu!
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ni wapemba wa bara.
   
 10. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  [​IMG][​IMG][​IMG]
   
 12. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  [​IMG][​IMG]
   
 13. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 14. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  not yet drawn mpaka pale wazungu watakapo jitotelea kuichora..
   
 15. m

  mkurugenz JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kazi kwao wandugu
   
Loading...