Master plan ya Arusha itakuwaje?

gogo la shamba

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
6,669
2,165
nimejaribu kufuatilia bomoabomoa ya Dar inavyofanyika naiuliza hivi itakuwaje watakapoanza kuangalia Arusha?maana katika miji isiyopangwa Arusha ni mmoja wapo sehemu iliyopimwa Arusha ni Niro tu, sehemu zote zilizobakia ni watu wamejijjengea tu,majumba baada ya kuuziwa viwanja ikiwa ni sehemu ya mashamba yao
kwa mfano: Mianzini,Ngusero,Mbauda,Kwa Mrombo,kwa Iddi, Sakina,Mwanama,Moshono,Sanawari,Azimio,Kisongo sasa kweli kama serikali inampango wowote wa kupanga mji wa Arusha afadhali waweke mambo wazi kuliko kusubiri yaje yatokee kama yale yanayofanyika Dar
 
Nimesikia kuwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Ardhi wanaenda huko field kuanza kazi ya hiyo MasterPlan ya Jiji la Arusha. Hawa vijana kwa kawaida huwa wanafanya kazi hizo kwa umakini mkubwa hasa ukizingatia ni sehemu ya masomo yao, tatizo liko kwenye Halmashauri za majiji,miji na wilaya wanazoenda kufanya kazi hizo hawawathamini kabisa.
Hawa vijana wengi wao hawana hata mikopo ya masomo na hata wanapokwenda field wanajigharamia na kuishi maisha ya taabu wakati utakuta Hizo Halmashauri zimetenga fedha za shughuli hizo na zinashindwa hata kama hawawalipi kuwahudumia kwa chakula na malazi bora ili wafanye kazi hizo kwa ufanisi zaidi. Wakurugenzi wengi wanaona kama vile hapo wamepata huduma ya bure na fedha hizo watumie kwa mambo mengine au wazipige watakavyo.
Natumaini kama Arusha inataka kujipambanua kuwa ni Halmashauri makini wasiache kuwahudumia vijana hao na kazi nzuri wataiona.
 
nigefurahi kama ningepata namba ya simu ya mmoja wa hao vijana
 
Mkuu ungeweka wazi malengo yako. Hili jambo sio dogo na kuwajali hawa vijana wetu ndio utanzania wenyewe. Vijana wanapoona wanajaliwa na serikali wanajenga moyo wa utumishi uliotukuka hapo baadae.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom