Vizuri
Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Joseph Kimario ‘Master Jay’, ameweka wazi mpango wake wa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Sara Kaisi ‘Shaa’.
Master J amesema Shaa atakuwa mke bora kwake kwani tayari ameshaishi naye kwa miaka 10 bila matatizo yoyote.
“Miaka 10 niliyoishi naye nimemwelewa vizuri, anastahili kabisa kuitwa mke wa Master J hapa nafanya taratibu za kumuoa ili tuishi maisha ya mke na mume,” Master J aliliambia gazeti la Mtanzania.
Mtayarishaji huyo wa muziki alisema kwamba anampenda Shaa kwa sababu ni msichana anayejielewa, licha ya kuwa msanii hasahau jamii inayomzunguka huku akijituma sana katika kazi zake zote kwa ujumla
Alifiwa Na mume lini jaman?Kuchinguzana miaka 10 duh. Shaa awe makini asije vishwa pete ya uchumba nayo ikakaa kodoleni miaka 5. Amuulize mwenzie Maimatha alivalishwa pete akaa nayo miaka 6 hadi jamaa akafa bila ndoa. Bahati akaja ibuka mume akachukua mzigo jumla.
Ana mke na watoto nadhani, sina uhakika niko tayari kukosolewa. SI kama tu ndugu Mengi, alikuwa na mke na alipata mwingine, life is full of suprises sometimes dear.Hiyo probation nimeipenda, miaka 10 doh. Anyway, mbona nilisikia Master Jay anamke?
Ila Joachim Kimario ( MASTER J) jamaa anaonekana ni mstaraabu (gentleman) na ana akili, nasikia anataka kurudi kwenye gemu ya uproducer
Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Joseph Kimario ‘Master Jay’, ameweka wazi mpango wake wa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Sara Kaisi ‘Shaa’.
Master J amesema Shaa atakuwa mke bora kwake kwani tayari ameshaishi naye kwa miaka 10 bila matatizo yoyote.
“Miaka 10 niliyoishi naye nimemwelewa vizuri, anastahili kabisa kuitwa mke wa Master J hapa nafanya taratibu za kumuoa ili tuishi maisha ya mke na mume,” Master J aliliambia gazeti la Mtanzania.
Mtayarishaji huyo wa muziki alisema kwamba anampenda Shaa kwa sababu ni msichana anayejielewa, licha ya kuwa msanii hasahau jamii inayomzunguka huku akijituma sana katika kazi zake zote kwa ujumla.
Ni Joachim Kimario au Baba Nuru.Ila Eliakim Kimario ( MASTER J) jamaa anaonekana ni mstaraabu (gentleman) na akili, nasikia anataka kurudi kwenye gemu ya uproducer