Watanzania wametakiwa kuwakataa wale wote wanaohamasisha au kuunga mkono mikakati inayolenga kuingiza nchi kwenye machafuko, vurugu au migawanyiko ya kisiasa.
Hayo yamebainishwa na kijana mjasiriamali na mdau wa masula ya siasa nchini, Masoud Mambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema watu wanaofanya hayo ni wapinga maslahi ya taifa na ustawi wa wananchi, hivyo wanapaswa kukataliwa.
Amesema kuwa bila amani hakuna haki, bila utulivu hakuna maendeleo na kwamba bila umoja wa kitaifa hakuna Tanzania imara, na kwamba nchi yetu imekuwa kimbilio la watu waliokimbia machafuko ya kisiasa katika mataifa yao, hivyo tusikubali historia hii tukufu ibadilishwe kwa matakwa ya kisiasa ya muda mfupi.
“Watanzania tukumbuke tukiruhusu siasa za kuvuruga amani zitawale, waathirika wa kwanza tutakuwa ni sisi wenyewe sio hao walioughaibuni au wanasiasa wenye viza tayari kukimbilia ughaibuni. Maendeleo yatasimama, uchumi utadorora na ajira zitapotea hivyo gharama ya kuyajenga upya itabebwa na sisi wananchi,” amesema
Amefafanua kuwa, Tanzania ni nchi inayotawaliwa na sheria, kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, vyama vyote vilivyosajiliwa kisheria ni sawa mbele ya sheria bila ubaguzi wowote, hivyo basi jaribio lolote la kubeza, kudharau au kupuuza ushiriki wa vyama fulani vya siasa katika chaguzi, mijadala au majukwaa ya kitaifa kwa hoja kwamba chama au vyama vingine vimesusa ni kinyume cha msingi ya demokrasia, haki na usawa,” amesema.