Maskini wanaongoza kupiga wake zao na watoto

Maskini wanaongoza kupiga wake zao na watoto

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,804
Reaction score
60,650
Napoishi Mimi Nina jirani yangu mmoja Ni maskini tu Kama mimi anaishi maisha ya kuunga unga Sana kapanga chumba kimoja na ana mke na watoto wawili.sasa huyu jamaa ana hasira Sana,nadhani ipo siku atakuja kuua mke au mtoto.juzi niliamka asubuhi nikakuta anampiga mwanae wa kiume kisa alipoteza hela shilingi 1000.sasa kweli imagine unampiga mtoto wa darasa la tano fimbo Kama 20 na mazoezi ya kijeshi push-ups.mambo hayo nakumbuka Ni vijijini tu ndo mtu ukipoteza hela unachezea kichapo.jana mchana saa Saba akawa anampiga mke wake kampiga Sana ngumi.akawa anamwambia mke wake "unasema Mimi nakubaka una akili wewe".akampiga Sana na libao mke wake naye anaonekana Ana kiburi badala akimbie ye ametulia tu anamwambia mumewe nitakupeleka polisi mbona ulivonitongoza hukuwa hivi ulikuwa unanipa maneno matamu.jamaa akawa haelewi anamchezeshea tu Tena mbele ya watoto anamwambia nitakubaka kweli na polisi nakusindikiza.akampiga sana akamchania hadi nguo akawa anamwambia mke wake kwanini kuna meseji anatumiwa na wanaume wengine.mimi hapo nikawa nachungulia tu kwa mbali nashuhudia yote huruma ilinishika lakini nikaona nitulie Sina la kufanya.leo nimekutana na huyu jamaa asubuhi akawa anajifanya ananilalamikia kuwa arsenal jana kamchania mkeka alikuwa ale laki mbili na sabini.me nikawa hata Sina hamu ya Kuongea naye nikikumbuka alivyompiga mkewe na mtoto nikaona sio rafiki mwema nikamwambia ndo hivo Bhana ipo siku utakula tu Kaka usijali akawa anajichekesha chekesha.akiwa na sisi kijiweni anaonekana Ana cheka Ana furaha lakini kumbe akiwa nyumbani Ni Simba.kweli nyumba zinaficha mengi hasa nyumba za masikini.kwa matajiri wao familia zao naona Zina amani watoto wanacheza Hawana wasiwasi hawamuogopi baba.
 
Juzi nilisikia habari kuna mzazi kapiga mtoto kwasababu alimwaga chakula kwa bahati mbaya, kapiga sana mtoto.
Mwingine kapiga hadi kauwa kwasababu mtoto kadokoa nyama.

Nikawaza sometimes umaskini unachangia wazazi wawe wakorofi.
 
Hakuna kitu kibaya kama umasikini
255782001030_status_3e42532358f94f3694db307d6dc20768.jpeg
 
Kwa sababu matajiri ni wachache pia, mzani haujabalance hapo labda tutumie uwiano
 
Sijasoma bandiko ...so nina comment kwa mujibu wa heading inavyosema
.
Sababu kubwa haswaa -- ni msongo wa mawazo " unaochangiwa na hali ngumu ya utafutaji ambayo wanaipitia. .. pia Sababu nyingine ni -- kundi kubwa la masikini lina beba watu wasiojitambua (baadhi ) so hiyo huwa inasababisha watu hao kushindwa kutambua haki za ki-binaadamu na kutafasiri kila mistake inayo fanywa na binaadamu wenzao haswaa members wa family.. huwa wanapaswa kuadhibiwa iwe kwa fimbo .kipigo cha ngumi mateke .matusi .kejeli ama dharau etc

kwakuwa hawajitambui wanashindwa kuyatizama makosa ya watu wanao wazunguka kuwa yanaweza kuwa fursa ya watu hao kujifunza na hatimae kubadilika na kuwa watu bora "

Ili ufanikiwe ni lazima ukosee katika jambo either kitu fulani .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umasikini mbaya tufanyen kazi kwa bidii

2019 hatua 1 yenye mafanikio zaidi
 
najikuta napata hamasa ya kukwambia kuwa umkumbuke yule mhenga alie sema"mke na mme wakipigana, shika jembe ukalime" kitendo cha mwanamume mtu mzima kuchungulia wanandoa wakipigana ni sawa na kuwashwa na pilix2 ambayo haukuila..[emoji41][emoji41] fanya kazi achana na vitu visivyo kuhusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijasoma bandiko ...so nina comment kwa mujibu wa heading inavyosema
.
Sababu kubwa haswaa -- ni msongo wa mawazo " unaochangiwa na hali ngumu ya utafutaji ambayo wanaipitia. .. pia Sababu nyingine ni -- kundi kubwa la masikini lina beba watu wasiojitambua (baadhi ) so hiyo huwa inasababisha watu hao kushindwa kutambua haki za ki-binaadamu na kutafasiri kila mistake inayo fanywa na binaadamu wenzao haswaa members wa family.. huwa wanapaswa kuadhibiwa iwe kwa fimbo .kipigo cha ngumi mateke .matusi .kejeli ama dharau etc

kwakuwa hawajitambui wanashindwa kuyatizama makosa ya watu wanao wazunguka kuwa yanaweza kuwa fursa ya watu hao kujifunza na hatimae kubadilika na kuwa watu bora "

Ili ufanikiwe ni lazima ukosee katika jambo either kitu fulani .

Sent using Jamii Forums mobile app
sawa[emoji118]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom