MASKINI NI MTAJI KWA MATAJIRI.

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,372
54,909
Salaam !

Leo nimeona niandike kidogo juu ya hawa watu ambao wamejitahidi kuvuka daraja la umaskini na kusogea mbele kidogo kwenye mafanikio, Japo nafahamu ya kuwa kila aliyepata huwa katafuta kwa jasho muda mwingine kudharauliwa hadi kufikia malengo yake.

Katika dunia ya leo hii sio watu maskini tu wamekuwa wakitumiwa kama mtaji bali hata nchi tajiri zimediriki kutumia nchi maskini kama sehemu ya siasa zao (maskini ni mtaji kwa tajiri), Mara nyingine tumeona maskini wakitumiwa katika vinywa vya watu kama sehemu ya kuhakikisha mambo yao yanafanikiwa kiurahisi.

Katika jukwaa moja lililoezekwa mabati na kushikiliwa na nguzo nne nilisikia sauti ya kuwatumia maskini ikizidi kutetema masikioni mwao kwa dhana ya kuwa watasongeshwa mbele kwa misaada pale watakapokubali kuchagua "NDIO", upole wao na kukata tamaa kumewafanya wawe wepesi wa kuamini binadamu kuliko hata utekelezaji wa majukumu yao ili wapate kile wanachotaka.

Watoto wao ambao ni taifa changa wamerithishwa tayari dhana ya kuwa kuna mtu atakuja na neema kwao na wao kwa muda mrefu wamekaa wakisubiri neema hizo adimu katika dunia ya leo.

Sio katika siasa ila bali hata katika mahekalu ya kuabudia wamekuwa ni wa kwanza kuingia kwa maneno matamu ili mradi tu mtaji wao mdogo walionao waupeleke mikononi mwa mtu mmoja atimize mambo yake kiurahisi.

Maskini mwenye itikadi kali huwa anaamini kuwa mafanikio yake huja kwa jitihada zake binafsi na Wala sio kwa vinywa vya watu wenye nia ya kuwadharau na kuwaona sio lolote katika dunia hii.

Msitutumie kama mitaji ya mambo yenu tafadhali najua matajiri ni wagumu sana kutapeliwa ila hata kile kidogo chetu mnakitaka tena !!!!.
 
Back
Top Bottom