Mwaka 1992, Athuman China akitokea Yanga aliweza kucheza katika Ligi za Uingereza...!
Na wengine wengi tu zaidi ya China. Edibily Lunyamila alishawahi ku testi zali Ujerumani. Mohamed Mwameja Uingereza pia. Ali Mayayi na Abdallah Sabebe walijaribu America Kusini.
Bahati mbaya, Kibunango, hawa wachezaji huwa wanarudi kimya kimya, hakuna mwandishi aliyekaa nao na kuwauliza kinaga ubaga, je watathmini wako wa huko walikupa feedback gani baada ya kushindwa?
Na wao wenyewe wachezaji wanadhani ni nini kiliwashindishwa? Baridi, kiingereza cha maelekezo, au mabio ya ligi ya UK, au hawakupata ushirikiano, au hawakuambiwa ni nini hasa kinachotafutwa, au hawakujua mifumo ya uchezaji wa Uingereza? Na hawa ma "agent wanaojulikana na FIFA" waeleze haya.
Ingekuwa vizuri kama Ngassa, badala ya kurudi Yanga na Simba na Manyema, na Kagera Rangers na Ashanti ya Ilala, angekubali hizo offers alizozipata sehemu nyingine zaidi ya UK, huko Marseille ya Ufaransa, na Uholanzi, kama ilivyoripotiwa magazetini, kama magazeti yanasema kweli. Kutoka hapo anaweza akajaribu kupanda kusajiliwa huko UK bila haya ma tryout yasiyo na kichwa wala miguu maana watakuwa wameshamuona akicheza kwenye higher caliber league huko huko kwao Ulaya.
Kwenye tryout kila mchezaji anacheza kuonyesha umahiri wake, hakuna cha team spirit. Sasa kama wewe ni midfielder, utakubali ukae kwenye tryout unagawa mipira wenzako wang'are? Au ndio utaanza kugenda na chaki weeee, mpaka ugonge kifimbo cha kona, usimame uelekee the other direction kinyume nyume ili kuji expose? Hakika utaonekana hujui u-midfielder. Forget these shoddy tryouts na hawa ma agenti "wanaojulikana na FIFA."