maskini NGASSA ;wish u nyc trip back to home | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

maskini NGASSA ;wish u nyc trip back to home

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, Apr 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Habari nilizozipata hivi punde ni kuwa Ngassa ameshidwa kufuzu kwenye majaribio kwa nujibu wa wakala wake Yusufu Bakhresa ni kuwa ameshindwa kupita kwenye mchujo wa wachezaji wengine 14 waliokuwa wanawania nafasi 3 tu kujiunga na kikosi cha Gianfranco Zola. Hata hivyo Ngasa aliaenza majaribia hayo jumatatu iliyopita kwa kufanya mazoezi na reserve team ya West Ham United alipandinshwa siku ya Alhamisi iliyopita kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza kinachoshiriki ligi kuu Uingereza.Hizi ni habari sa kusikitisha lakini Ngassa anapaswa asife moyo kwani wakala wako yuko kwenye mazungumzo na team ya Fulham kuona kama anaweza kupata nafasi ya kufanya majaribio na team hiyo au hata timu nyingine nchini humo.Pia afahamu kuwa amefungua njia ya soka letu kukua na kujitangaza kimataifa maana hata kipindi cha Soccer Africa cha wiki hii walimzungumzia na kumtakia kila la kheri.
  Usife moyo Ngassa safari ndio kwanza imeanza na umri bado unakuruhusu.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  Ngasa we kaza buti nadhani umeona wenzako wamekuzidi nini kwa hiyo jitahidi ukamilishe hayo utafanikiwa, usife moyo!! mbona watu kama kanu walianza hivyo???
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kana Ka nsungu lazima afurahi......unajua kuna watu wana midomo mibaya wakiongea kitu unapata nuksi......
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Waswahili wasema, "kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi"... alipofikia ngassa hakuna katika historia yetu changa ya soka na tunamuomba mungu ampe imani

  ...lakini pia kwa nini akiwa huko asianzie pia kujaribu league one ya akina leeds na MK dons? REMBEMBER JUNIOR AGOGO AND THE REST OF AFRICAN PLAYERS STRUGGLING THERE

  DONT COME BACK HEAD DOWN BRO.... TRY AT LEAST SIX TEAMS BEFORE FLYING BACK...

  WANUGU HUPIGA KAMBI ULAYA HATA MWAKA KAMA KUNA POTENTIAL YA KUCHEZA... REMEMBER OBI MIKEL
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kama visa yake ni miezi mitatu unataka ajilipue?, huku hakufai kama huna makaratasi hasa lengo lako likiwa kuwa kwenye sports, bora kama unamshauri abebe box sawa ila ndiyo atakuwa amefunga milango kwa wengine. Mwacheni arudi bongo akacheze mpira wa "bagamoyo" mnaoshwa kwa damu ya paka ili mshinde mechi matokeo yake mkifungwa mnaambiwa mlivunja masharti
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sina maana hiyo

  nategemea hiyo miezi tatu achape zoezi na kuhangaikia hata timu ya leagues two.... fuatilia story ya obi mikel au junior agogo utanielewa

  three months may mean a lot to a man in need!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mwaka 1992, Athuman China akitokea Yanga aliweza kucheza katika Ligi za Uingereza...!
   
 8. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Na wengine wengi tu zaidi ya China. Edibily Lunyamila alishawahi ku testi zali Ujerumani. Mohamed Mwameja Uingereza pia. Ali Mayayi na Abdallah Sabebe walijaribu America Kusini.

  Bahati mbaya, Kibunango, hawa wachezaji huwa wanarudi kimya kimya, hakuna mwandishi aliyekaa nao na kuwauliza kinaga ubaga, je watathmini wako wa huko walikupa feedback gani baada ya kushindwa?

  Na wao wenyewe wachezaji wanadhani ni nini kiliwashindishwa? Baridi, kiingereza cha maelekezo, au mabio ya ligi ya UK, au hawakupata ushirikiano, au hawakuambiwa ni nini hasa kinachotafutwa, au hawakujua mifumo ya uchezaji wa Uingereza? Na hawa ma "agent wanaojulikana na FIFA" waeleze haya.

  Ingekuwa vizuri kama Ngassa, badala ya kurudi Yanga na Simba na Manyema, na Kagera Rangers na Ashanti ya Ilala, angekubali hizo offers alizozipata sehemu nyingine zaidi ya UK, huko Marseille ya Ufaransa, na Uholanzi, kama ilivyoripotiwa magazetini, kama magazeti yanasema kweli. Kutoka hapo anaweza akajaribu kupanda kusajiliwa huko UK bila haya ma tryout yasiyo na kichwa wala miguu maana watakuwa wameshamuona akicheza kwenye higher caliber league huko huko kwao Ulaya.

  Kwenye tryout kila mchezaji anacheza kuonyesha umahiri wake, hakuna cha team spirit. Sasa kama wewe ni midfielder, utakubali ukae kwenye tryout unagawa mipira wenzako wang'are? Au ndio utaanza kugenda na chaki weeee, mpaka ugonge kifimbo cha kona, usimame uelekee the other direction kinyume nyume ili kuji expose? Hakika utaonekana hujui u-midfielder. Forget these shoddy tryouts na hawa ma agenti "wanaojulikana na FIFA."
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks Kibunango.... Sikulijua hilo, nakumbuka ya akina marsha, mwameja, njohole, deo lukas ambao pia hawakupata high profile teams and publicity

  Hivi china alichezea timu gani?
   
 10. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  KWANINI,watanzania tusikubali kwamba apart from Filbert bayi,TANZANIA haijawahi kuwa na mwanamichezo yoyote-na hili tatizo i dont see light at the end of the tunnel in the near future
   
 11. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yeah kweli hakuna haja ya kukata tamaaa kwani hapo sio mwisho wa nafasi nyingine. Ila sasa najiuliza kwani huyu meneja wake lazima atafute timu za Premier League. Mbona kuna timu nzuri tuu kama za Coca cola Champions league mawazo tuuu unless meneja anatoa macho kwenye dau kubwa na sio kukuza kipaja
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Kina albert Sengo walizamia ujerumani...mpira ulaya ni tofauti kabisa kabisa....wakienda wanashindwa kwenye maaribio na hawataki kujaribu tena sijui kwa nini maana uwanja nimpana sana hata daraja 3 pia wanaweza kuanzia....
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwangu mimi sioni kama hiili ni la kusikitisha kwa sababu huu ni mwanzo. Kwamba kuna timu ya premier League ambayo imekubali kumjaribu mchezaji kutoka Tanzania ni hatua kubwa sana. Kushindwa kwake kwenye majaribio kunatakiwa kusikatishe tamaa kama ulivyoeleza, safari inaanza kwa hatua moja na hizi zinaweza kuwa hatua mbili zimeshapigwa na safaru ndio imeanza hiyo
   
 14. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kuntakinte, mimi nina wasi wasi na huyo "agenti anaetambuliwa na FIFA."

  Kwenye mambo ya procedure anaharibu. YANGA wamekasirika kwamba walikuwa wanaulizwa maswali kuhusu trade/tryouts za Ngassa wakati wao hawana taarifa rasmi zozote za hayo. Bhakressa hata hakujali kuwa contact YANGA. YANGA wakasema huyo Ngassa na timu yake mpya na yeyote yule at the end of the day itabidi warudi YANGA maana wao ndio wana mkataba nae mpaka 2011. Mpaka ikabidi WEST HAM ndio wawa contact YANGA moja kwa moja baada ya kuona imeshakuwa soo. Hizi zote ni kazi za agenti. Agenti ni watu ambao huwa tunawaita "mission town," watu wa ma contact, na kuunganisha madili, middle man. Bhakressa ameshindwa kui contact timu ya mchezaji unaetaka kumnyakua, "agenti anaetambulika na FIFA"?

  Halafu ni wazi Bhakressa alishindwa kumpa Ngassa taarifa za awali za hali itakavyokuwa kwenye tryouts. Ngassa amepiga simu nyumbani akieleza almost kushtushwa na hali ya watahiniwa 20 kugombea nafasi tatu. Haya mambo yote yalitakiwa yasiwe suprise kwake. "Agenti anaetambulika na FIFA" ilibidi atafute kuyajua yote haya before, not after, the fact. WEST HAM wangeweza kumwambia kuna vacancies ngapi, wanahitaji positions gani, wanatarajia watahiniwa wangapi, wanatathminiwa katika maeneo yapi. Agenti ayajue.

  Halafu Ngassa, hutakiwi kulipwa zawadi zawadi na bakshishi za hapa na pale na huyo Bhakressa. Wewe ndio unatakiwa umlipe pale dili litakapo itika. Unapoanza kulipwa, kupewa rides na mapozeo ya hapa na pale saa hizi - kama inavyoripotiwa magazetini, kama magazeti yanasema ukweli - basi unapoteza confidence ya maamuzi au input kwa agenti. Anakuwa kama kakuweka mfukoni, na utashindwa hata kum-fire ukiona hakufai, utamwonea aibu, after all, anakupa hela ya kula. Wewe ndio principal wa agenti. Vuta subra, mshiko utakuja tu.
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ligi ngapi? Timu gani?
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ngasa usife moyo kama bahati yako ipo ipo tu
   
 17. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Jamani tuwe realistic!!! Hata unapokwenda kwenye interview huwa ni mambo mawili, kupata au kukosa kazi. Ukikosa si kwamba hufahamu bali kuna ambaye alikuzidi points ndiyo maana kunakuwa na panel na chart ya maswali na point kwa kila swali. Na unapokosa kazi huwa kawaida si mwisho wa kuomba kazi mahali pengine, bali ni kuangalia pale ambapo unajua hukuweza kujibu proper uboreshe (hapa sizungumzii academic credits maana kama ziko chini wa juu atakupita tu) hapa nasemea kama unaamini you have the best academic credits ila tu katika kujieleza uliteleza.

  Pia Ngasa hapaswi kukata tamaa, yeye na huyo mdhamini wake wameshajua tatizo so walishughulikie ili next time aweze ku comptete tena. Kaza buti Ngasa, tuko nyuma yako.
   
 18. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Watu wengi wanasahau kuwa Kassim Manara (or was it Sunday Manara?) alicheza Austria (timu nimeisahau) na kukipiga mpaka Champions League! Vile vile alienda na kucheza in the defunct NAPSL, ile league aliyeichezea akina Pele na Bobby Moore.

  Meingine aliyecheza Austria daraja la pili alikuwa Nicodemus Njohole. Mdogo wake wa mwisho Renatus alichezea mpira wake Switzerland if I am not mistaken.
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Nyambui alishinda silver medal olyimpics za 1980 na Titus Simba (RIP) alishinda silver medal commonwealth games 1974.Na kwa sasa hivi,God willing,tutakuwa na shujaa mpya wa basketball Thabeet Hasheem.
   
 20. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mrisho bado anaweza akafanikiwa, kuna vitu vingi ambavyo wachezaji wetu wanakosa especial the whole knowledge of the game, wenzetu hawaangalii kama wajua kupiga chenga au danadana, wanaangalia health fitness, physique, knowledge ya football sheria zote 17,team work, speed n.k. na kucheza mpira wa kulipwa lazima tuanze kupanda kidogo kidogo ile ni kazi lakini hapa kwetu hatuko professional so tunamiss a lot of basic criteria, wachezaji wetu wafundishwe na waingie darasani. Ni time imefika ya kuwa na Proffesional Technical Director TFF wa maana sio mbabaishaji Kayuni
   
Loading...