Mrisho Ngassa ngoma nzito West Ham United | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrisho Ngassa ngoma nzito West Ham United

Discussion in 'Sports' started by Lucchese DeCavalcante, Apr 17, 2009.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Winga wa Yanga ya Dar es Salaam na timu ya soka ya taifa 'Taifa Stars', Mrisho Ngassa ameanza majaribio katika timu ya West Ham United ya nchini Uingereza, lakini kukiwa na wachezaji wengi wanaowania pia kusajiliwa na timu hiyo.

  Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Mohammed Sadick, ambaye ni Mtanzania anayeishi nchini humo, alisema pamoja na kuwa na matumaini huenda Ngassa akafanikiwa, lakini kazi ya ziada itabidi aifanye ili kuipata nafasi hiyo. "Niliposikia kuwa Ngassa anakuja huku, nilifuatilia mambo mbalimbali ndani ya timu anayokuja, nikagundua anatakiwa aongeze juhudi za ziada uwanjani ili kuwashawishi wamchukue.

  "Namfahamu Ngassa ana uwezo mkubwa, kinachotakiwa apambane, maana vijana wanaotakiwa ni wachache, wakati wao wapo wengi, huku wengine wakitoka nchi zenye majina makubwa kisoka Afrika na hata hapa Uingereza," alisema Sadick. Hata hivyo alisema katika siku mbili za mazoezi, ameonyesha mwelekeo, ingawa idadi kubwa ya wachezaji waliopo katika majaribio ambao wanazidi 20, huku wakitakiwa watatu inamtisha.

  Naye mchezaji mmoja wa Yanga, ambaye ni rafiki wa karibu wa Ngassa, alilieleza gazeti hili jana kuwa amezungumza na mchezaji huyo juzi na kumwambia ameanza vizuri, lakini idadi ya wanaotakiwa inamwogopesha. "Amenambia wapo wachezaji 20 wengine wanatoka Nigeria, Senegal, Afrika Kusini na sehemu nyingine, lakini wanatakiwa watatu, sasa nimemweleza asife moyo ndio mapambano yenyewe hayo, aongeze juhudi uwanjani.

  "Amenielewa, tunamtakia heri, huku pia wadau wengine naamini nao wanamtakia mafanikio mazuri, hakuna kisichowezekana chini ya jua, " alisema mchezaji huyo. Ngassa ambaye ni mtoto wa kiungo wa zamani wa Pamba, Simba na timu ya taifa 'Taifa Stars', Khalfan Ngassa 'Babu', aliondoka Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kwenda nchini Uingereza kufanya majaribio ya kucheza soka katika kikosi cha vijana cha timu ya West Ham ya huko inayoshiriki Ligi Kuu ya England.
   
 2. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  namsubiri hater kana ka nsungu
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Simba mnalooooooooo Henry Joseph vp mlitaka mlipwe $50,000/= nini?
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mtanzania, hatuangalii u Yebo Yebo wake. Kila la heri Ngasa, mafanikio yake yaweza kuwa chachu ya mafanikio ya watanzania zaidi.
   
 5. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Kila la kheri Mrisho Ngasa, tupo katika maombi ili ufanikiwe. Kufanikiwa kwako ni kufanikiwa kwa taifa zima
   
 6. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  mimi ni mnyama damu! lakini hili la Ngassa sio la ukandambili bali utaifa zaidi....!
  Ngassa keep it up for TZ ...!
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
 8. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Whoa whoa whoa.....timu ya vijana ya West Ham au timu halisia ya West Ham?

  Tunapeana mukari bin shauku kwa timu ya vijana?

  Na hata kama ni timu yenyewe, kuna kitu nimemsikia Ngassa anakisema nikamuona hana ari au sijui niseme uelewa wa mambo ya michezo ya kimataifa.

  "I have been receiving calls from different people, all congratulating me and urging me to work hard and remain in England," he told BBC Sport.

  The 20-year-old winger, said he is now trying to avoid injury and also training very hard.

  "I want to avoid injuries because I can't show my best if I am not fit," said Ngassa."

  Katika michezo ya kugusana, wachezaji huwa wanatakiwa kusifiwa kwa kutoogopa kuumia, ndio wanaonekana wako washindani. Ngasa unafahamu kwamba hata kwenye mipira ya mchangani kwenye magoli ya minazi ukijulikana unaogopa kuumia umia utakua unasugulishwa benchi, ni "kunguru."

  Na mpirani utaepuka vipi kuumia? Unawaonyesha wasaili wako huelewi mentality nzima ya contact sports.

  Una "train very hard," kivipi? Maana unaogopa kuumia. Una aspire kuwa mcheza wa kulipwa wa kimataifa wewe?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Apr 17, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Tayari umeshaanza.....
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...na mimi pia ni TAIFA KUBWA mpaka kuzikana, na jumapili tutalitumia pengo lake ipasavyo kuwafunza kandambili adabu!

  Stay away Mrisho Ngassa! Good luck!
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  yaa kazi ni kubwa sana maana unajuaa huku tz sisi ndio hatupeleki wachezaji wetu ila kwa nchi wenzzetu hasa west africa mbona majaribio kila siku watu wanaenda tuu.....wanashindwa Uk wanaenda Sweden,Denmark....asikate tamaa ila anajaribu nchi zingine sio lazima uk tuu......ingawa nawajua wa tz wengi hatuna confo kuamua kwenda ulaya kujaribu hata daraja la tatu etc....tukipata 200,000 na sifa kibao za ki bongo mtu anaota kitambi anakuwa faza soon misimu 4 tuu utakuta ameshakuwa faza anaenda kucheza mipira ya j2 apewe posho na waraabu....anakuwa anatummia jina kuomba bia kwenye ma bar....kwisha habari yaoo....
   
 12. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Habari nilizozipata hivi punde ni kuwa Ngassa ameshidwa kufuzu kwenye majaribio kwa nujibu wa wakala wake Yusufu Bakhresa ni kuwa ameshindwa kupita kwenye mchujo wa wachezaji wengine 14 waliokuwa wanawania nafasi 3 tu kujiunga na kikosi cha Gianfranco Zola. Hata hivyo Ngasa aliaenza majaribia hayo jumatatu iliyopita kwa kufanya mazoezi na reserve team ya West Ham United alipandinshwa siku ya Alhamisi iliyopita kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza kinachoshiriki ligi kuu Uingereza.Hizi ni habari sa kusikitisha lakini Ngassa anapaswa asife moyo kwani wakala wako yuko kwenye mazungumzo na team ya Fulham kuona kama anaweza kupata nafasi ya kufanya majaribio na team hiyo au hata timu nyingine nchini humo.Pia afahamu kuwa amefungua njia ya soka letu kukua na kujitangaza kimataifa maana hata kipindi cha Soccer Africa cha wiki hii walimzungumzia na kumtakia kila la kheri.
  Usife moyo Ngassa safari ndio kwanza imeanza na umri bado unakuruhusu.
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  tuache kudanganyana
   
 14. M

  Magehema JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nani mwenye taarifa sahihi kuhusu Ngassa? Kila mmoja anadai lake. Jana nilimsikia Saria from BBC alipokuwa akiongea na TBC1 kwamba Ngasa alishaachana na West Ham tangu tarehe 17 baada ya kushindwa majaribio ya awali. Tujuzeni wenye taarifa latest.
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Nadhani unapenda kusikia hivi (Amepewa muda wa wiki moja zaidi kaka!)na hupendi kusikia kwamba Ameshindwa majaribio West Ham
   
 16. M

  Magehema JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Misconception, niliuliza kwasababu moja tu, kumekuwa na kimya kingi kutoka kwa wakala wake na ngassa mwenyewe, nadhani taarifa sahihi/kuaminika nilitegemea zitoke kwa wakala au ngassa.
   
 17. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kimya kipi na wakati umesema jana TBC1 walitangaza, au huwaamini TBC1 au humuamini Saria. Umehakikisha kwamba TBC1 hawakupata taarifa kutoka kwa wakala!

  Kama vipi pitia mtandao wa West Ham

  Asante
   
 18. M

  Magehema JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wakala und Ngasa are nowhere to be reached!!!, neither by Saria nor by TBC1
   
 19. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Leo kwenye kipindi cha michezo cha BBC wakala wa Ngassa bwana Bakhresa amevunja fununu za issue ya hii. Ametabanaisha kuwa Mrisho Ngassa amefanya vizuri majaribio pale West Hama na Zola amemkubali ila wamempa muda wa miezi mitatu pamoja na program maalumu ya kuongeza stamina wakati mascout wa WH wakimfuiatilia kwa makini atakapocheza mechi mbili za kimataifa dhidi ya New Zealand and DRC. Ngassa atahitajika kurudi West Ham United hapo mwezi Julai kwa majaribio zaidi na ikiwezekena apewe deal ama la. Tusubiri yatakayojiri maana hata wakala mwenyewe hataki kuweka mambo wazi kuhusu suala hili.
   
 20. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nafkiri sasa nyota imeng'aa Tanzania, tunakula ugali sasaa na hatulii ng'aa! Mrisho wa Ngasa ndo huyoo anaelekea kupaa! msisikitike Watanzania wenzangu mbona wao waliwezaa! je Kabumbu wapigayo Wanaija si ndiyo hiyo yetu au wao wanapaa! sema ntashindaa, sema atashinda! wote pamoja tutashindaa! tuwe na imani,juhudi na umoja na tuache mawazo ya kikindaa! Je mnajua NBA DRAFT huko Tanzania hatushikiki, ni HASHEEM THABEET au 'HESHIMA THABITI' Hakunaa!
   
Loading...