tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,883
- 18,299
Ni muda mrefu sasa Michael Wambura amekuwa akivutana na uongozi wa Simba kwenye issue ya uchaguzi wa viongozi ktk klabu hiyo. Hii ni mara ya pili Wambura anawekewa pingamizi baada ya kufanikiwa kuchomoa lile pingamizi alilowekewa mara ya kwanza. Nasikia kuna wanachama wamepeleka issue hii kunako CAS, na kuna hatari ya uchaguzi wa wa Klabu ya Simba kusimamishwa hadi kitendawili hiki kitakapoteguliwa.
Mtakumbuka kwamba mivutano kama hii imeanza kumuandama Michael tangu akiwa FAT (sasa TFF). Mimi sio mfuatiliaji mzuri wa mpira wa nyumbani Tanzania lakini namuomba Bw Maiko aachane na mambo ya mpira. Ndio. Kitumbua chake kwenye mpira kimeishaingia mchanga. Namshauri atafute kazi nyingine ya kufanya badala ya kung'ang'ania kwenye mpira tu miaka yote. Kwani yeye aliandikiwa kwamba riziki yake ipo kwenye mpira tu?
Bw Maiko achana na biashara kichaa hiyo, haina tija kwako. Muda unaoupoteza ni bora ukautumia kujiajiri kwenye sekta nyingine ya kiuchumi. Hii sekta ya mpira imeishaingia shubiri.
Nawasilisha.