Maskini Magufuli........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maskini Magufuli........

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Dickson Ng'hily, Mar 23, 2011.

 1. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Magufuli matatani
  • JK naye amshambulia waziwazi

  na Betty Kangonga


  [​IMG]
  SIKU chache baada ya Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, kudaiwa kwamba alikusudia kujiuzulu kwa madai ya kuingiliwa katika utendaji wake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, jana Rais Jakaya Kikwete naye aliigeukia wizara hiyo akiitaka iache ubabe katika kutekeleza zoezi la bomoabomoa huku akitoa kauli ya kumshambulia moja kwa moja waziri huyo.
  Hali hiyo inaweza kutafsiriwa kuwa Magufuli bado anakabiliwa na shinikizo la kuingiliwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kiuwaziri.
  Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia zoezi hilo la bomoabomoa ambalo mara kadhaa alinukuliwa akisisitiza azma yake ya kuhakikisha nyumba na majengo yaliyoingilia hifadhi za barabara yanabomolewa ili kupisha miradi kadhaa ya ujenzi ukiwemo ule wa miundo mbinu kwa ajili ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam.
  Mbali na Magufuli, Profesa Tibaijuka ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pia ni mmoja wa mawaziri ambao wamekuwa wakitekeleza zoezi la bomoabomoa, lakini katika hali ya kutiliwa shaka, Rais Kikwete amejikuta akimruhusu waziri huyo kutekeleza operesheni za wizara yake bila kumhofia mtu yeyote wala “cheche” zozote.
  Kikwete alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Wizara ya Ujenzi na baadaye kutembelea Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa ajili ya kuzungumza na watendaji wa idara zilizo chini ya wizara hizo na mashirika yake.
  “Lazima uangalie historia ya barabara imetoka wapi….siyo kuja na kubomoa maana hakuna mtu anayeweza kubomoa nyumba yake kwa saa 48,” alisema Rais Kikwete akionekana dhahiri kumlenga Magufuli aliyekuwepo hapo.
  Alisema ni kweli zipo sheria zinazowataka wananchi waliojenga katika hifadhi ya barabara wahame lakini kuna ubabe unaofanywa na wizara hiyo ya Magufuli katika zoezi la bomoa bomoa.
  Alisema wapo baadhi ya wananchi wamekaa kwa kipindi kirefu katika maeneo hayo na kuweka vitu mbalimbali hivyo unapowabomolea leo ni kutaka kuwafanya waichukie serikali.
  Akitolea mfano barabara ya Chalinze mpaka Segera katika eneo la Msata ambapo kuna barabara kuu inayoelekea Bagamoyo, alisema katika eneo hilo la barabara ya asili kuna nyumba za zamani za wakoloni ambazo zimewekwa alama ya X inayoashiria kuwa zitabomolewa na kuielezea hatua hiyo kuwa ni uonevu.
  Alisema huo ni uonevu kwa kuwa barabara inayotaka kujengwa ndiyo iliyofuata wananchi hivyo wathaminiwe na walipwe fidia kitendo cha kupiga X ni uonevu hivyo aliitaka wizara hiyo iache ubabe.
  Aliitaka wizara hiyo kuhakikisha inaweka utaratibu maalumu na kuzifanyia upembuzi barabara zote muhimu na siyo kusubiri mpaka fedha zipatikane au bajeti.
  Alitaka fedha za barabara zinazotengwa kuhakikisha zinatumika kikamilifu hasa kwa zile za halmashauri na kuunda kitu kitakachoitwa Bodi ya Wakaguzi ambayo itapitia hifadhi zote za barabara na kuepusha suala la bomoa bomoa.
  “Unakuta watendaji wanapita katika barabara hiyo wanaona watu wanavyojenga bila kuchukua hatua…mtu akimaliza nyumba yake mnafika na kumbomolea huku wengine wakipoteza maisha kutokana na shinikizo la damu …hapana hili lazima tulisimamishe,” alisema.
  Alisema kuwa serikali imechota fedha kutoka katika bajeti za wizara mbalimbali jumla ya sh bilioni 250 kwa ajili ya kuipa Wizara ya Ujenzi ili kuweza kuongezea katika kulipa madeni mbalimbali yanayowakabili.
  Alisisitiza wazo la kuanzishwa kwa usafiri wa reli akitolea mfano treni inayoweza kuanzishwa kwa kuanzia stesheni mpaka Kimara Temboni ambayo inaweza kupunguza msongamano wa foleni barabarani.
  “Msitegemee sana usafiri wa mabasi yaendayo kasi, yanaweza kusaidia katika kipindi hiki lakini kumbukeni kuwa idadi ya watu inaongezeka kila kukicha hivyo kwa miaka 10 ijayo tatizo linaweza kuwa kubwa jaribuni kuangalia na njia nyingine,” alisema.
  Kwa upande wake, Magufuli alisema wizara yake inakabiliwa na changamoto balimbali ikiwa ni pamoja na kiasi cha fedha wanachotengewa kutotolewa kwa wakati.
  Alisema hatua hiyo imesababisha makandarasi 35 kutoa notisi kutokana na ucheleweshaji wa malipo ambayo ni sh bilioni 454 zinazodaiwa. Kwa upande wake Profesa Tibaijuka alimuahidi Rais Kikwete kusimamia na kutekeleza yote anayoagiza ikiwa ni pamoja na kurudisha maeneo ya wazi lakini alimuomba pindi maneno yanapokuwa makali dhidi yake amlinde. Alisema wizara yake imepungukiwa wataalamu kwa asilimia 74 katika halmashauri na waliopo hawana sifa stahili.
   
 2. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Ni vile mimi sio MAGUFULI, ila ningekuwa ni YEYE, NINGEACHANA NA LISERIKALI LA HUYU MTANI WANGU (MKWELE)
   
 3. O

  Ome Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 79
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Jk hajamshambulia magufuli, Jk kasema sheria ifatwe waliojenga kwenye hifadhi wabomolewe ila na ubinadamu utumike, kwamba kama barabara haijengwi mwaka huu basi watu waendelee kukaa mpk itapohitajika na pia notes ya masaa 48 haitoshi iongezwe.
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  HIyo ndo CCM, waziri yeyote anayefanya kazi kwa kasi na ari mpya wao wanampunguza, mnakumbuka Mrema enzi zake? na sasa Magufuli. grrrrr hiki si chama cha wananchi ni Cahama Cha Mafisadi!!!
   
 5. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,268
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280
  Betty Kangonga ni mwongo au ni mwandishi wa habari kanjanja.
   
 6. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama ukweli ni huo there is little sense added.
  Tatizo: Kama barabara haijengwi leo watu waachwe waendelee kukaa, mimi sioni akili hapa maana (1) sheria hairuhusu (2) hao unaoonyesha kuwaonea huruma hauwapendi maana ujenzi wa barabara utakapoanza kazi ya kuwaondoa itakuwa kubwa kwa serikali na kwao kwa sababu wengine watakuwa wamepanua ujenzi na idadi ya wakuhamishwa itakuwa imeongezeka na wapi hela ya walipa kodi kuwafidia na itakuwa ni maudhi kwa watu wengi zaidi wa kuhamisha. Au huu utakuwa mfano mbaya wa wengine kuiga.
   
 7. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  katika maagizo ya Rais wetu nimeokota moja tu la kufanyia kazi nalo ni lile alilosema kwamba mtu anapoanza kujenga viongozi humuona na kuacha aendelee na halafu baadaye ndipo wanakuja na bomoabomoa. Nakubaliana kuwa kutokana na mtandao au mfumo wa wa serikali yetu hakuana anayeanza kjenga bila serikali kujua maana kuanzia serikali ya mtaa (ambayo pia hutumia viongozi wa ma shina), kata hadi wilaya kwa nini serikali ishindwe kuzuia ujenzi wa wazi holela? Ukweli tunaachia mambo yaende hivyo kunufaisha mafisadi.
  Tatizo ni kuwa na sheria ya kukataza lakini kwa makusudi bila ya kuweka adhabu kama ilivyo sheria ya kuvuta sigara kwa mfano huu utakuta sigsra zinauzwa stand ya basi na pembeni kiberiti cha kuwashia hapo hapo katika mkusanyiko wa watu kiasi hata polisi asifanye kitu kwa sababu akimshika atamshitaki kosa gani ambalo hakimu atatoa adhabu.
   
 8. D

  DONALD MGANGA Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri inapashwa iwe Hongera Magufuli. Sasa nimeelewa siku zote waandishi wa habari wataandika wanachotaka wao sisi tujue, na si kilichosemwa. Nasikitika tu kwamba Rais hakumwelewa Magufuli na ndo maana alisema alichosema akisahau kuwa Ndugu yake alisimamia Wizara hiyo kwa miaka mitano kabla ya Magufuli na ujengaji holela ulikuwa umekoma wakati wa Mkapa na ukashamili wakati wa vijisenti na Dr. Sasa huyu kasafisha Ardhi akatoka, akasafisha Uvuvi katolewa sasa anataka kusafisha miundombinu wanambana bana. Nasema aendelee nawakitaka wamfukuze wao na si yeye kujiuzulu. Defence wapo wamejaa tele sembuse mchapa kazi. Fanya Kazi ngánawane, achana na wazushi.
   
Loading...