Maskini Dereva huyu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maskini Dereva huyu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elli, Jun 3, 2010.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Juzi nikiwa nipo home ndo nimetoka kwenye ujenzi wa Taifa hili lisilojengeka, alinijia Mke wa Jirani yangu na akaanza kunieleza hadithi ndefu ambayo kwa hakika ilikuwa ni mwendelezo wa hadithi ya toleo lililopita tu.

  Kwa uchungu kaniambia; baba fulani amewekwa mahabusu baada ya mdhamini kutoweka...na hivyo atakua huko hadi tarehe 16 June, 2010. Nikajiuliza kwa uchungu, Ina maana jiarani yangu huyu sitamuona tena kwene Mechi za Kwanza za WC?

  Huyu jamaa, kesi yake eti, kakamatwa na Trafic wale pale Kibaha, taa moja ya mbele ilikuwa haiwaki vizuri, baada ya kukataa kumpa kile alichokitaka askarii yule, akampeleka polisi na kumbadilishia mashitaka; kuwa amekamatwa baada ya ku-overtake magari saba! Baada ya kupelekwa mahakamani, Askari huyu alionekana siku moja tu na baada ya hapo hajawahi kuonekana tena mahakamani, huku kijana huyu akiteseka kwa safari za kutoka Dar kwenda Kibaha kusikiliza kesi isiyokuwa na kesi

  Juzi, mdhamini wake kachoka na yeye akaamua kujitoa, Kule wanataka mdhamini ambaye anaishi Kibaha na si nje ya hapo, hivyo ikabidi apelekwe mahabusu huku askari yule akiwa haonekani.

  Siandiki ili kumtetea, ila swali la msingi ni hivi: Kwa wale wenzangu ambao na madereva, hivi unaweza ku-overtake magari saba yote yakiwa yanatembea na mtu aliesimama kando, ayahesabu? Nauliza hivi kwani, ku-overtake gari moja ambalo pia lina mwendo hukuchuku takribani mita si chini ya 75- hadi 100, hivyo ku-overtake magari saba ni kama mita 500 hivi. Nikajiuliza kuwa, huyu askari alimwonaje?
  Alikuwa hewani au wapi? Lakini, hivi na nyie Mahakimu, huwa hamuangalii logic ya makosa, au kwa sababu ni kosa tu basi halina mantiki?

  Siamini kuwa, kila dereva wa dala dala ni mhuni, ila wapo baadhi tu kama vile ambavyo wapo pia polisi wanaotunga kesi.

  Jioni njema
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  So sad indeed!
   
 3. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ndio maana nikijua sina kitu huwa nakimbia,kuliko ukristo wa kuja kukufikisha hapo alipo huyo bwana dereva.
  Maana kwa trafiki ni unazo kama huna ulitegemee hilo!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Only in Tanzania
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu bongo no balaaaa! Mi nafikiri kuna sababu ya kuwashughulikia kihuni zaidi!
  I have a plan.....it is coming and yu will see.
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Tupe na sisi hio plan ili wakitukwida tu, tunaitumia fasta.

  Utapata hati miliki ya kuwa mwanzilishi wake
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Jamani hakuna kosa la kuovertake magari saba kwenye sheria zetu. Huyu hakimu amuachie huru huyu bwana labda awe amewekwa ndani kwa kosa lingine.Halafu mahakimu wetu ni vichekesho kweli, makosa ya traffic mengi adhabu ni fine, kwa nini umnyime mtu kujidhamini mwenyewe kwa kosa ambalo akiwa convicted adhabu ni shs 50,000/=.
   
 8. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama hujui haki ni rahisi kuambiwa hii kesi adhabu ya ni miaka ishirini na ukitaka faini ni milion 20. Na watanzania wengi ndo tunapoliwa pale kwani traffic akikukamata anaanza kukusomea na makosa hata ambayo hayamo kwenye sheria na anachukua lesseni ya gari/dereva, anabandua number plates, etc. Lazima uteme mpunga, ukikomaa anakufungulia hata kesi ya kubaka au kukutwa na bangi kwenye gari
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Naombeni basi huo mwarobaini wa hawa jamaaa
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Just like that? Hatakiwi kuchukua lesseni wala kadi ya gari instantly, kubandua number plates nayo haruhusiwi kabisa. You can just as well drive without them( the number plates) so long as the vehicle is registred. Dawa always have a cerified copy of the registration card and driving licence and have a revenue stamp endorsed on it. Akichukua hiyo ni kama kulamba galacha kesho unatoa nyingine na unaendelea na maisha. Never give them original itakutesa sana.
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  hapo nimekupata saana
   
 12. M

  Mundu JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  DRC, Mozambique, Malawi pia ni hivyo hivyo!
  Lets say, only in Africa!
   
 13. bht

  bht JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Traffic offence na lupango kumbe eeh!!
   
 14. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  so, tutaishi hivi hadi lini???
   
Loading...