Maskini Banzastone!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maskini Banzastone!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Jul 17, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 133
  Kama Mtanzania mwenye utu, pindi upatapo nafasi ya kumtia Banza machoni kwa kipindi hiki, yamkini utamlilia msanii huyo nembo ya muziki wa dansi ambaye anahitaji msaada wa hali na mali kuirejea afya yake.

  Gazeti lako pendwa la Ijumaa kwa kupitia waandishi wake, juzi (Jumatano) lilitia ‘maguu’ nyumbani kwao Banza, Sinza Kijiweni, Dar es Salaam na kujionea hali halisi aliyonayo staa huyo pamoja na mazingira anayoishi.

  Kwa mujibu wa ushuhuda wetu, afya ya Banza bado ni msamiati wenye utata ingawa ana maendeleo mazuri kiasi ukilinganisha na jinsi alivyokuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kinondoni (kitabibu), Mwananyamala, Dar es Salaam.

  Waandishi wetu walifika nyumbani kwao Banza majira ya saa tano asubuhi na kukuta mwanamuziki huyo amelala lakini walilakiwa na mama yake mzazi, Khadija Jebeli.

  Akiongea na gazeti hili nyumbani kwake, mama huyo alisema kwamba mwanaye bado yupo hoi kwa sababu hajapata matibabu ya kuridhisha kutokana na kukosa uwezo.

  Mama huyo aliongeza kwamba pia familia yake haipati ‘sapoti’ ya kutosha kutoka nje ili kumuwezesha kumuuguza vema mwanaye, ingawa alikiri kupokea misaada michache kutoka kwa wasamaria wema.

  Aliongeza kuwa kwa kipindi hiki ni kama mwanaye ametengwa kwani marafiki zake wamekata mguu kwenda kumuona wakati alipokuwa amelazwa Mwananyamala makumi ya ‘Watizedi’ walikuwa hawakatiki kumjulia hali na kumfariji.

  “Watu walikuwa wakimiminika Mwananyamala Hospitali lakini tokea tumefika nyumbani watu hao sijawaona, kumjulia hali mtu si lazima uwe na chochote,” alisema Khadija.

  Mama huyo aliongeza kwamba hivi sasa ndiyo Banza anajitahidi angalau kuanza kutembea, hivyo bado yupo ndani na kwamba mara chache huwa wanampeleka Hospitali ya Palestina, Sinza ambako hupata muendelezo wa matibabu.

  Wakati waandishi wetu wakiendelea kuongea na mama mtu, ililetwa taarifa kwamba Banza aliamka hivyo kuongozwa hadi sebuleni na kumkuta nyota huyo wa “Shoka moja mbuyu chini” akiwa ameketi ‘kochini’.

  Baada ya kuingia chumbani, waandishi wetu walifanikiwa kuongea na Banza ambaye alikuwa akizungumza kwa sauti ya chini yenye kuungaunga ambayo iliashiria wazi kuwa ndugu yetu bado anatesekea ugonjwa.

  Banza a.k.a Mwalimu wa Walimu alisema kuwa yeye bado yupo ndani, ingawa kuna mambo ambayo yanavumishwa na watu yenye lengo la kumchafua.

  “Watu wanasema mengi lakini ninyi waandishi mnaniona, andikeni hivi mnavyoniona, kwa sasa namshukuru Mungu naendelea vizuri,” alisema staa huyo wa nyimbo, Mtu Pesa, Hujafa Hujasifiwa, Mtaji wa Masikini, Elimu ya Mjinga na nyingine za kumwaga.

  Banza alipotakiwa kuongea chochote kuhusu muziki alisema: “Sitaki kabisa kuongelea muziki, kaandikieni kama mlivyoniona, mambo ya muziki yaacheni.”

  Kwa vyovyote iwavyo, Banza bado anahitaji msaada. Kama mdau wa muziki au unaguswa kwa maana moja au nyingine na afya ya mwanamapinduzi huyo wa muziki wa dansi na kizazi kipya kwa jumla, unaweza kumchangia kupitia akaunti ya benki ya mama yake.

  Unaweza kumchangia Banza kupitia Benki ya CRDB, jina la akaunti ni Hadija Jebeli, nambari ya akaunti ni 0IJ2022367600.

  SOURCE: IJUMAA.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 133
  Pole sana mama Hadija Jebeli ndiyo ulezi tupo pamoja.
  Haya Watz kutoa ni moyo na si utajiri, mwenye chochote hata kumjuulia hali na kumuombea Braza inatosha.
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,160
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Duuh jamaa bado hajatoka kitandani? Hivi huyu jamaa si alikuwa kaajiriwa na bend fulani....kama alikuwa na ajira na mwajiri wake angekuwa anachangia NSSF.....angetibiwa kiulaini!....Wasanii wengine wajifunze kutokana na hili!

  Get well soon Banza!
   
Loading...