Maskini Baba Diamond, azidiwa ghafla

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,807
34,193

Abdul Juma ‘Baba D’


Erick Evarist na Gladness mallya

DAR ES SALAAM: Maskini wee! Baba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma ‘Baba D’ anaumwa sana! Ndivyo Risasi Mchanganyiko linavyoweza kukuhabarisha baada ya mzazi huyo kuzidiwa ghafla na kukimbizwa hospitalini kutibiwa kwa msaada kutokana na kukosa fedha, twende hatua kwa hatua.

NI JUMAPILI ILIYOPITA


Tukio hilo la kusikitisha la baba mzazi wa msanii ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kutosha Bongo, lilijiri Jumapili iliyopita ambapo kwa msaada wa Dk. Fadhili Emily wa Kituo cha Tiba cha Fadhaget Sanitarium kilichopo Mbezi Beach-Africana, Dar, baba Diamond alifikishwa kutoka nyumbani kwake Magomeni-Kagera hadi hospitalini hapo na kupatiwa matibabu.



….Akiwa mapokezi.


CHANZO CHAVUJISHA

Awali, Risasi Mchanganyiko lilipokea taarifa za mzee Abdul kuzidiwa nyumbani kwake lakini ikaelezwa kwamba, hakuwa na msaada wowote hadi majirani walipopata mawasiliano ya daktari huyo na kumuomba amsaidie.

“Jamani baba D (baba Diamond) yupo hoi hapa nyumbani kwake Magomeni. Miguu inamuuma, anashindwa kutembea na ukizingatia hana kipato, anashindwa pia kwenda hospitali. Na bahati mbaya kwa muda mrefu hata majirani wamekuwa wakimsaidia lakini bado hajapata tiba sahihi.”

AUNGANISHWA NA DK. FADHILI

“Leo (Jumapili) kuna jirani yake mmoja hapa ndiyo amepata wazo baada ya kusoma Gazeti la Risasi Jumamosi (ndugu na hili), amepata namba za Dk. Fadhili katika makala anazoandika gazetini kuhusu afya. Akampigia na kumuomba msaada na bahati nzuri dokta huyo ameguswa na tatizo la mzazi huyu, amemtumia nauli ya teksi ili akimbizwe hospitalini kwake, sasa hivi ndiyo wanaelekea huko,” kilisema chanzo hicho.

MAKACHERO WAUNGA TELA

Licha ya kuwa muda huo ulikuwa umeyoyoma (saa 1 usiku), makachero wetu waliingia mzigoni kuelekea moja kwa moja Mbezi kwenye hospitali hiyo na kumkuta baba D akiwa anaingia mapokezi katika kliniki hiyo.



ASAIDIWA NA WAHUDUMU

Akiwa mapokezi, makachero wetu walimshuhudia baba Diamond akisaidiwa na vijana wawili ambao ni wahudumu wa hospitali hiyo, walimkalisha kwenye kochi kisha wakaanza kumpa huduma ya dharura ambapo walimpima presha na kumuita Dk. Fadhili atazame miguu yake.

KUHUSU MIGUU

Dk. Fadhili alipofika, alimvua soksi baba huyo na kuikagua vizuri miguu hiyo kabla ya kuingia naye ndani katika chumba maalumu cha vipimo na matibabu.



VIPIMO VINGINE

Ilibainika kuwa, miongoni mwa vipimo alivyopimwa baba D ni pamoja na kile cha Quantum Magnetic Analyzer ‘QMA’ ambacho kazi yake ni kutambua magonjwa mbalimbali ndani ya mwili wa binadamu. Hata hivyo, Risasi Mchanganyiko halikufanikiwa kujua kipimo hicho kilitambua nini!

BABA DIAMOND AFUNGUKA

Baada ya kupimwa na kupatiwa dawa za kutumia, baba Diamond aliliambia gazeti hili kuwa, anamshukuru daktari huyo kwani ameweza kugundua tatizo linalomsumbua na kwamba anaamini dawa alizopewa zitamsaidia.

“Kwa kweli ni Mungu tu, hali yangu ni mbaya, miguu inanisumbua kwa zaidi ya miaka nane sasa. Inauma, imevimba na inabadilika rangi kuwa myeupe. Inakuwa kama inatoka mabakamabaka. Kiuchumi siko vizuri kabisa.”



NGOZI IMEATHIRIKA

“Dk. Fadhili amenipima, amebaini ngozi yangu imeathirika vibaya. Amenitajia tatizo langu kitaalamu na amenipa dawa za kutumia, lakini pia amenielekeza mazoezi maalum ambayo natakiwa kuyafanya,” alisema baba Diamond huku uso wake ukijaa simanzi.



Dk. Fadhili akimpa mushauri Baba Diamond.


AMWAGA SHUKRANI

Baba Diamond alipoulizwa kama alimueleza mwanaye Diamond kuhusu suala hilo wakati alipozidiwa, alisema hakuona na haoni sababu ya kumwambia kwani analijua na hapendi kuendeleza malumbano na mwanaye lakini anamshukuru Dk. Fadhili kwa kujitolea kumsaidia bila malipo yoyote.



“Sipendi kuendeleza malumbano, ninachokiangalia kwa sasa ni miguu yangu. Nitamshukuru Mungu zaidi nitakapopona kabisa maana nimeshahangaika nayo sana. Kipekee, kutoka moyoni nimshukuru Dk. Fadhili kwa kusikia kilio changu na kunisaidia bure.

“Sikutegemea, mtu unaumwa, anakwambia anakutumia fedha ya teksi uende hospitalini kwake akakutibu bure. Ni upendo wa hali ya juu na Mungu amzidishie, pale alipotoa apabariki na apate zaidi,” alisema baba Diamond.

Diamond

DIAMOND ANASEMAJE?

Gazeti hili lilifanya jitihada za kutaka kumsikia Diamond anazungumziaje suala hilo la ugonjwa hadi kufikia mzazi wake kusaidiwa na mtu baki, simu yake haikuwa hewani lakini hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia Mtandao wa WhatsApp ulioonesha ameusoma, bado hakujibu chochote.



TUMEFIKAJE HAPA?

Baba Diamond amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo wa miguu ambapo awali, mzazi huyo alisema anasumbuliwa na kansa ya ngozi lakini hata hivyo, mwanaye Diamond amekuwa mzito kumsaidia kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni mwanaume huyo kumtelekeza mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ yeye akiwa mdogo.

MAJIBU YA DK. FADHILI

Juzi Jumatatu, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu daktari huyo na kumuuliza kuhusu tatizo la baba Dimaond na namna alivyolishughulikia, ambapo alijibu:

“Ha! Jamani, ugonjwa wa mtu ni siri kati yake na daktari, labda kama ataona sawa aseme yeye mwenyewe.”

chanzo.Maskini Baba Diamond, Azidiwa ghafla!
 

Attachments

  • Maskini Baba Diamond, Azidiwa ghafla!.jpg
    Maskini Baba Diamond, Azidiwa ghafla!.jpg
    25.5 KB · Views: 163
  • Akiwa mapokezi.jpg
    Akiwa mapokezi.jpg
    23 KB · Views: 154
  • ASAIDIWA NA WAHUDUMU.jpg
    ASAIDIWA NA WAHUDUMU.jpg
    27.5 KB · Views: 184
  • Diamond.jpg
    Diamond.jpg
    17.1 KB · Views: 172
  • Dk. Fadhili akimpa mushauri Baba Diamond..jpg
    Dk. Fadhili akimpa mushauri Baba Diamond..jpg
    23.3 KB · Views: 138
  • NGOZI IMEATHIRIKA.jpg
    NGOZI IMEATHIRIKA.jpg
    23.2 KB · Views: 124
  • TUMEFIKAJE HAP.jpg
    TUMEFIKAJE HAP.jpg
    27.8 KB · Views: 140
  • VIPIMO VINGINE.jpg
    VIPIMO VINGINE.jpg
    23.2 KB · Views: 137
  • Dk. Fadhili akimpa mushauri Baba Diamond..jpg
    Dk. Fadhili akimpa mushauri Baba Diamond..jpg
    23.3 KB · Views: 156
Kwa yeyote mdadisi, ni rahisi kugundua kwamba huyo baba wa diamond aliandaliwa kwamba achukuliwe picha huku akionekana kusaidiwa na wahudumu wa hapo hospital, ili kijana apakaziwe na magazeti ya udaku.
Alafu... iweje mzee aende kwenye matibabu huku akiwa amejiandaa na wapiga picha?
Alafu.... kama mzee alikwenda kupata matibabu, kwanini aliwaita makanjanja wa magazeti ya udaku ili wakipake kwa mwanae?
Agghhhh....
 
Kwani uyu mzee mtoto wake mi diamond tu. Kwann wasiandike baba wa Queen Dareen azidiwa. Wababa wanajitenga sana na watoto n Mungu hua wa ajabu watoto wa kutengwa hua wanafanikiwa mno. Hlf baadae wana play kua ni victim.
Ugua pole mzee lkn huo ni uchonganishi wa kwenda na waandshi wa habari hosptalini km sio kutaka kumchafulia Diamond ni nn.
 
Kama Mungu tunamkosea anatusamehe 7*70 naye ndiye aliyetuumba. Inakuwaje huyu Mondi kuona kosa alilofanya baba yake ni kubwa kiasi kwamba hawezi kumsamehe? Kama mtoto alipaswa kutambua hawezi pata baba mwingine zaidi ya huyo. Na asisubiri afe ndo aende kwenye msiba kwa mbwembwe. Namkubali Mondi ila kwa hili hapana.
 
Diamond anakosea sana. Yaani anahangaika na Zari halafu anamuacha babake anateseka
Omba Mungu awaweke mshuhudie kifo cha diamond siku moja..!

Ni mjinga sana! Angesamehe yaishe ila nadhani anajua kuwa anazo dhambi nyingi kuliko hii ya kuto msamehe baba yake ndiyo maana haoni umhimu.

Bila shahawa za huyu mzee uplatnum angeupata wapi? Anajifanya hajui mchango wa huyu mzee kwenye maisha yake! Shahawa zenyewe ni mchango kulijo kitu chochote kile klilicho changia uwepo wa diamond na jinsi alivyo..!
 
Diamond anakosea sana. Yaani anahangaika na Zari halafu anamuacha babake anateseka
usiangalie matokeo angalia na sababu ya matokeo pia...hawa wazee waliokula ujana enzi zao na kuwaacha watoto wao wakiteseka na mama zao huwaga siwaonei huruma kabisa.

Mimi pia yamenikuta kama hayo..naumwa nimelazwa Amana hospital na bi.mkubwa alikila pembeni uangu hana kitu baba yangu mzazi anashindana kuwatunza hela wakina Tx Moshi na Maalim Gurumo pale Amana Vijana center
 
usiangalie matokeo angalia na sababu ya matokeo pia...hawa wazee waliokula ujana enzi zao na kuwaacha watoto wao wakiteseka na mama zao huwaga siwaonei huruma kabisa.

Mimi pia yamenikuta kama hayo..naumwa nimelazwa Amana hospital na bi.mkubwa alikila pembeni uangu hana kitu baba yangu mzazi anashindana kuwatunza hela wakina Tx Moshi na Maalim Gurumo pale Amana Vijana center
Mzazi ni mzazi
 
Mgonjwa wa miguu kavaa mpaka soksi,nilitegemea angeenda hospitali na kandambili,au kabebwa chini hawezi kukanyaga,hapa ndio bongo movi zinaponiacha hoi.
 
Watoto msipende kuwasikiliza sana mama zenu hamuwezi jua nini kiliwatenganisha.....ni bora tu mondi ajitoe ufahamu amsaidie alafu huyu mzee malipo yake yawe kwa mungu.mwenyewe kwani yeye ndiye anayejua
Mwangalieni kanumba Naye alikuwa na kisasi kama mondi tu
LAKINI hata yeye alikufa na akamwacha baba yake na kinyongo chake moyoni...jiulizeniiii
 
Back
Top Bottom