Maskini Azam....watasubiri sana!!

Maskini Azam....watasubiri sana!!

Anselm

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2010
Posts
1,710
Reaction score
291
Kama kuna kitu Mmiliki wa team ya Azam FC angependa kitokee ni kwa team yake kutwaa ubingwa wa soka wa nchi hii na kupata fursa ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Club Bingwa Africa. Pamoja na uwekezaji mkubwa alioufanya kuhakikisha anajenga kikosi imara cha uwanjani pamoja na kujenga mbinu za nje ya uwanja za kusaidia kupata matokeo mazuri(refer mechi kati yao dhidi ya Yanga na dhidi ya Polisi msimu uliopita) lkn kwa mara nyingine tena kikosi chake kinaelekea kushindwa kumaliza nafasi ya kwanza. Ni jambo linalohitaji moyo wa uvumilivu (kama ule aliou'apply wakati alipo introduce maji yake ya Uhai kwa mara ya kwanza sokoni na kupambana na product nyingine iliyokuwa inafanya vizuri katika soko ya Kilimanjaro) kuendelea kutumia pesa nyingi katika kukusanya wachezaji mahiri wa kutoka pembe tofautitofauti za bara hili la Africa pasipo kufikia malengo pangwa...licha ya kuwa na wachezaji wenye majina kama akina Brian Umony,Humphrey Mieno na the Kipres (Tchetche na Bolou) bado team hii inaonekana kushindwa kuendana na kasi ya Wakongwe Yanga na Simba ambazo zimeendelea kutawala anga la soka ya nchi hii,ninachojiuliza ni kuwa kama miujiza haitawabeba Azam msimu huu msimu ujao wataambulia kitu kweli kwa mikakati ya viongozi makini wa team ya Wananchi(Yanga) katika kuhakikisha wanaifikisha Yanga kwenye level za kina TP Mazembe na Simba kujenga team makini kupitia Vijana?
Jinsi ninavyoona mwenendo wa soka la hii nchi linavyokwenda,nachelea kusema kuwa kwa Azam kuteka soka la nchi hii itawabidi kusubiri sana,mkubali-mkatae.
 
Mie binafsi niliisha bwatuka sana humu na kuwaambia kwa 'style' ya U-simba/yanga wataishia kunawa mikono tu, ubingwa kwao itakuwa ndoto. Hawa wanapaswa kujua kuwa Simba na Yanga ni kitu kimoja kwa kutaka kuonekana ni vilabu vikubwa hapa nchini, Tenga mwenyewe kavitafutia TBL kuwa MDHAMINI wao.
Wanapaswa kucheza mpira na sio kutegemea kuvuna mashabiki toka Simba na Yanga.
 
Yaani azam kombe la mapinduzi na uhai cup ndo saiz yao huku kwingine baadae sana, na walichokosea zaidi kuunda uchumba na simba
 
Back
Top Bottom