Masikitiko yangu kuhusu Chama Changu

Ungemwongelea Mzee Mtei anagalau kidooooogo ningekuelewa, lakini huyu PADRI wala hanipi homa, hiyo kazi alikuwa anaichapia wapi?? shida hapa ni umri Muoa na muolewa nikama Mbigu na Ardhi impact lazima...
 
Bahati mbaya au nzuri MKUBWA huyo (ETI) nasikia aliwahi kuwachunga kondoo wa BWANA, kama nilikweli chonde chonde zingatia maneno ya bwana wako.....ASIYE NA DHAMBI AWE WA KWANZA KUMTUPIA JIWE....mwisho wa kunukuu!
 

Sio vizuri mtu mzima kuaminishwa bila kujua ukweli wa mambo. Nakushauri kwa dhati kabisa kaisome orodha ya mafisadi kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Sikiliza maneno aliyosema Lowassa siku anajiunga na chama. Sikiliza maneno ya viongozi wa chama wakimpokea Lowassa halafu fanya maamuzi sahihi.

Ukimya wa Dr Slaa katika kipindi hiki ndio unaosababisha yeye kurushiwa madongo. Embu fikiria, Tupo vitani tayari kuiteka ngome ya wapinzani, risasi na mabomu yanarushwa kila kona. Jemedari wetu ambaye alishiriki kikamilifu vikao vyote vya siri ambavyo kwa sauti ya pamoja walikubaliana kumkaribisha Lowassa, ghafla ameuchuna. Viongozi wengine wafanyaje? Inabidi wakupe maneno ya kukupa ujasiri ili na wewe usiweke silaha yako chini. Tusonge mbele. Tuombe Mungu Fikra sahihi zitamrudia, naye atajumuika na sisi huko mbele ya safari.
 
Pia kuna suala la collective responsibility.... kuna wakati inabidi ukubaliane na wengi sio wewe unacho amini ili kusonga mbele.... kama Dr atakuwa mtu wa kuzila (kama kweli amezila), je serikali wataiendesha vipi? Maana kwenye kuendesha serikali kuna mengi inabidi ukubaliane na wenzako ili msonge mbele hata kama huyaamini....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…