Masikitiko : Yanga kushuka daraja

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,649
218,102
Huku pazia la Ligi kuu ya Vodacom likikaribia kufunguliwa wachambuzi wengi wa soka nchini Tanzania wanatambua matatizo makubwa yanayoikabili timu ya Yanga , wengi wanaongelea chini kwa chini uwezekano wa Yanga kushuka daraja.

Mimi nimeamua kujitokeza waziwazi na kutamka hadharani kwamba timu kongwe nchini Tanzani , Yanga ya Dar es salaam msimu huu wa ligi ITASHUKA DARAJA na kusambaratika , Hii siyo ramli bali ni ukweli kwamba ili timu iendelee kubaki ligi kuu inahitaji ushindi , kwa sasa YANGA HAIWEZI KUIFUNGA TIMU YOYOTE YA LIGI KUU , na inakabiliwa na aibu ambayo haijawahi kupata pale itakapokumbana na Mnyama .

Kama huifuatilii hii timu unaweza kudhani uzi huu ni wa masihara lakini muda ni mwalimu mzuri , Endeleeni kufuatilia
 
Nazidi kukubali tunarafikiana kwa mengi
 
Mi ni simba ila yanga haijafika hicho kiwango,tusiwadharau sana wanaweza wakaleta changamoto kwenye ligi.

Madharau yanga kwenye ligi inaweza kufungwa na simba,Azam,Singida au Mtibwa lakini hao wengine watakaa tu
 
kwa yanga hii ambayo haiwezi hata kulipa mishahara wakimsubiri manji arudi wajiandae kushuka daraja labda wafanye uchaguzi na kuwapata viongozi wenye fikra mpya
 
Young africans hatuwezi kushuka daraja forever
Kwanza mimi ingawa sio mpenzi wa Yanga lakini nawalaumu sana baadhi ya viongozi na wachezaji wa Yanga.
Baadhi ya viongozi badala ya kuisaidia Yanga wakati huu wa mtikisiko wao wanakimbilia kujiuzulu uongozi.
Yanga kukiwa na neema haohao wanaomba kuiongoza Yanga. Wakati huu ndio ulikuwa wakati wa viongozi kuonesha weledi, mbinu za uingizi na mshikamano ili kuinusu timu,
kama kuna tatizo wawataarifu wadau wa Yanga ili kwa pamoja wafikie suluhisho fulani.
Penye wengi hapaharibiki neno, Yanga ina wanachama, washabiki, na wapenzi wa kada mbalimbali.
Hadi kocha katoa huu ushauri, kocha ambaye ni mgeni kabisa hapo Jangwani.
Wachezaji nao ni kama wamekata tamaa, wanacheza chini ya kiwango wakati uwezo wa kucheza vizuri wanao.
Kukwama kupo ila kusiwe kama ndio Kiyama kisicho na jinsi ya kujikwamua nacho.
Sasa ndio mda wa kufanya kazi na sio, kuifikiria Ajira.
 
Ni hivi , wote uliowaona wakija yanga katika kipindi cha Manji walifuata hela tu , hela zimekata sasa wasubiri nini ?
 
YANGA SC 2018/2019
IMG-20180722-WA0026.jpg
 
TFF wana nia mbaya na Yanga..unaanza ligi mechi tatu za mwanzo away..points 9 ziko mashakani..huyu msomali mahaba yake kwa mikia yanatia aibu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom