Masikitiko: CHADEMA pesa ya ruzuku ni kwa ajili ya nini? haitumiki kutibu viongozi?

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Nimekuwa mwanachama wa Chadema tangu 2000. Nimekuwa nafuatilia kwa karibu sana mwenendo wa afya ya Mwanachama kijana wa chadema ndugu Mhere Mwita aliyepata ajali 3.10.2016_ akiwa katika shughuli za kichama mkonai Dodoma.

Natambua wanachama wa chadema tulichanganishana toka mhere apatwe na tatizo mpaka kufikia hatua ya kuimarika na kuruhusiwa kuondoka muhimbili. Siku za hivi karibuni,kijana huyu alitangaza kuuza kiwanja chake ili apate matibabu zaidi ambayo yanagharimu 3.5M
Maswali yangu kwa uongozi wa juu wa chadema na Bavicha Taifa.

1. Ruzuku ya chama ni kwa ajili ya kuwawezesha viongozi wa chama Taifa kusafiri nje ya nchi na kufanyia harakati nchini?

2. Mchango wa chama uko wapi kwenye suala la afya ya Mhere Mwita?

3. Malisa Godlisten na wanachama wengine ndiyo pekee wanaratibu mipango ya kumtibu mwanachama mwenzao bila chama kuingilia kati?

4. Mbowe na uongozi wa juu hata kama mulichangia kiasi chochote katika matibabu ya Where Mwita,Tamkoa chama ni lipi juu ya matitababu zaidi ya kijana huyu ambaye anatakiwa kutibiwa kwa gharama ya 3.5m?

Chadema inawatumia vijana na kuwatelekeza baada ya kuvuna matokeo chanya?
51c8949e17413b1a08edff02bcfd3f0d.jpg

Nakumbuka Juliana shonza alipohamia CCM aliwahi kusema kuwa chadema inawatumia vijana na kuwatelekeza, hii nimeanza kuiamini kwa misingi kwamba katika swala la mhere Mwita,chama kama chama kimeshindwa kutoa japo msimamo wake namna ya kumshughurikia huyu kijana aliyeumia akiwa kazini kukipigania chama chake.

Matokeo ya chadema kutokuwa na kauli juu ya afya ya Mhere Mwita.
e3195d4d0ce39bacd98d0f25b7b673fd.jpg

Kiuhalisia,kutokana na viongozi wa Kitaifa wa Bavicha na chama kwa ujumla kushindwa kuonesha namna ya kuwasaidia vijana na wanachama wengine pindi wanapopata ajali kazini inaweza kukatisha moyo vijana kujitoa kukitumikia chama.

Mwisho.

Bavicha na uongozi wa juu wa chadema toeni pesa kwa ajili ya matibabu ya Mhere Mwita. Rudhuku ya chama siyo ya kufanyia ziara tu nchi za nje.

Mbowe na mwenyekiti wa Bavicha Taifa kama mumeshindwa swala DOGO tu la 3.5m kwa ajili ya matibabu ya Mhere Mwita bado mnajiita viongozi mathibuti wa chama?
Mbowe and katambi would you please stepdown.

Rais2020
Rais wa mioyo ya watu.
Rais arakayewafanya muishi kama malaika.
 
Hela za ruzuku za CHADEMA huliwa na Kibatala katika kesi za kuwatetea makamanda; iwe ni Lema kwa madai eti kamtukana Mkuu wa Mkoa au Tundu Lissu kusingiziwa uchochezi. Pia hutumika kusafirosha safu ya uongozi
William kumekucha bado una maluweluwe asubuhi hii mwanga umetoka sasa usiogope amka kuna watu nje, Kweli wewe akili zako Hakuna tofauti na matawi makavu ya mti muda wote hudondoka unawaza Chadema badala hata ya kuwaza Familia yako inayosoma shule za kata shame on you
 
Ina maana pesa za ruzuku ni kwa ajili kwa mambo kama hayo?! Ikiwa wewe ni Mwana-CHADEMA hudhani busara ingekuwa ni kuanzisha kampeni ya kumchangia huyo ndugu?! Kwanini usingeongea na Uongozi wa JF halafu ukapitisha harambee iliyobarikiwa na uongozi wa JF na kuwaomba wapenzi, wanachama na yeyote atakayeguswa kumchangia huyo nduyo bila kujali suala la itikadi? Hivi kwa jinsi Watanzania wanavyopenda kusaidiana na CHADEMA ilivyo na wafuasi wengi JF unadhani hilo jambo lingeshindikana?

Your ID is Rais2020. I can assume you're dreaming to be Mr. President one day! Lakini hata kama sio, je kuna initiative yoyote uliyowahi kuifanya kuhusu huyo ndugu badala ya kukimbilia kulaumu uongozi?! Hudhani busara ingekuwa ni kujitofautisha na wao kwa kuchukua initiative ya kumsaidia mwanachama mwenzenu?!

Halafu wanachama wa CHADEMA msiwe mnajitoa ufahamu kwa kuongea lugha zile zile za mahasimu wenu (CCM) dhidi ya chama chenu!!!

Inawezekana ni kweli viongozi wanatafuna ruzuku lakini kama akili yenu mnadhani mnapata mipesa kochokocho kutokana na ruzuku basi you've long way to go!! Hao CCM wenyewe ruzuku haiwatoshi itakuja kuwa nyinyi?! Pamoja na kwamba wana investment kila kona, ruzuku maradufu kuliko nyinyi lakini bado wanalazimika kupitisha mabakuli ya chini chini kwa wafanyabiashara!! What about you guys?!

Chama kina mikesi kila kona ya nchi, still mnaamini mna mipesa kochokocho?!

Msiwe kama watoto wadogo ambao kutokula kwao wali nyama wanadhani baba yao anafanya makusudi hata kama wanamuona baba yao akiamka asubuhi kazi yake ni kuokota chupa za maji kwenye majalala!!
 
Hivi wale wakuu wenu wa miko wastaafu wanaotembea na viraka kwenye nguo kule morogoro wanakoishi CCM inawafikiria kweli
 
Kuna wakuu wa mikoa wastaafu wa CCM morogoro huko nguo wameziba viraka mbona chama kiliwatumia hakiwasaidii
 
Ina maana pesa za ruzuku ni kwa ajili kwa mambo kama hayo?! Ikiwa wewe ni Mwana-CHADEMA hudhani busara ingekuwa ni kuanzisha kampeni ya kumchangia huyo ndugu?! Kwanini usingeongea na Uongozi wa JF halafu ukapitisha harambee iliyobarikiwa na uongozi wa JF na kuwaomba wapenzi, wanachama na yeyote atakayeguswa kumchangia huyo nduyo bila kujali suala la itikadi? Hivi kwa jinsi Watanzania wanavyopenda kusaidiana na CHADEMA ilivyo na wafuasi wengi JF unadhani hilo jambo lingeshindikana?

Your ID is Rais2020. Zamani nilipata kuwaambia watu hapa kwamba, kama kweli PK alisema kuhusu bandari ya Dar, atakuwa mjinga kusema endapo Bandari ya Dar es salaam ingekuwa Rwanda wangekuwa mbali! Hoja yangu ilikuwa kiongozi bora ni yule anayeweza ku-take initiative kutokana na raslimali alizonazo na sio kuota kile ambacho hana na katu hatakuwa nacho!!

Now coming back to your ID, I can assume you're dreaming to be Mr. President one day! Lakini hata kama sio, je kuna initiative yoyote uliyowahi kuifanya kuhusu huyo ndugu badala ya kukimbilia kulaumu uongozi?! Hudhani busara ingekuwa ni kujitofautisha na wao kwa kuchukua initiative ya kumsaidia mwanachama mwenzenu?!

Halafu wanachama wa CHADEMA msiwe mnajitoa ufahamu kwa kuongea lugha zile zile za mahasimu wenu (CCM) dhidi ya chama chenu!!!

Inawezekana ni kweli viongozi wanatafuna ruzuku lakini kama akili yenu mnadhani mnapata mipesa kochokocho kutokana na ruzuku basi you've long way to go!! Hao CCM wenyewe ruzuku haiwatoshi itakuja kuwa nyinyi?! Pamoja na kwamba wana investment kila kona, ruzuku maradufu kuliko nyinyi lakini bado wanalazimika kupitisha mabakuli ya chini chini kwa wafanyabiashara!! What about you guys?!

Chama kina mikesi kila kona ya nchi, still mnaamini mna mipesa kochokocho?!

Msiwe kama watoto wadogo ambao kutokula kwao wali nyama wanadhani baba yao anafanya makusudi hata kama wanamuona baba yao akiamka asubuhi kazi yake ni kuokota chupa za maji kwenye majalala!!
Mkuu nimesema toka mwanzo kuwa nimekuwa nikitoa mchango wa pesa kwa ndugu yetu na nimefanya jitihada kubwa sana kushawishi wenzangu kuchangia swala hili.imefikia mahala watu wamechoka maana chama kama chama kipo kimya. 3.5m ikose chama?. Huu ni ujinga.
 
Hoja yangu ni kwamba ni namna gani umetumia forum kama hii kuwashirikisha wanachama na hata wasio wanachama kumsadia huyo jamaa kwa sababu mimi si mtu ninayeamini katika malalamiko!?
 
Nadhani ule ugonjwa wako wa akili unakurudia itabidi tukuwahishe mirembe kabla hali haijawa mbaya
 
Hoja yangu ni kwamba ni namna gani umetumia forum kama hii kuwashirikisha wanachama na hata wasio wanachama kumsadia huyo jamaa kwa sababu mimi si mtu ninayeamini katika malalamiko!?
Mkuu to be honest,sijafanya hivo katika jf badala yake nimefanya hivo kupitia ukurasa Wangu wa Fb. Kutokana na taratibu na nature ya members wa jf sikuweza kuwashirikisha ukizingatia kuwa kuna Bavicha Taifa ambao wao ndiyo wenye jukumu la kufanya hivo kupitia jf. Personally sikufanys hivo maana watu wana perceptions tofauti tofauti ambapo majina kama tapeli ni common hapa.
 
Mkuu nimesema toka mwanzo kuwa nimekuwa nikitoa mchango wa pesa kwa ndugu yetu na nimefanya jitihada kubwa sana kushawishi wenzangu kuchangia swala hili.imefikia mahala watu wamechoka maana chama kama chama kipo kimya. 3.5m ikose chama?. Huu ni ujinga.

Sidhani kama malengo ya Chama ni kuwatibu wanachama wake.Swala la Tiba kwa wananchi linashughulikiwa na Serikali kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Wananchi wanalipa Kodi ili kusaidia upatikanaji wa Huduma bora za Jamii ikiwemo Matibabu bora.Kama kuna Mtanzania anayeteseka kwa kukosa huduma bora za Afya anayetakiwa awajibike ni Serikali.
 
Mtoa uzi hajielewi anaandika vitu Kama mtoto wa chekechea, Tatizo unapoandika propaganda kukisema chama fulani tumia akili sio unatumia utumbo kufikiri kisa njaa kali, Kazi ya ruzuku sio kutibu wanachama, Tatizo husomi vitabu na sheria mbalimbali usipende kusikiliza njaa inapokugonga tumboni itapelekea ulifanyiwe kitu mbaya
 
Sidhani kama malengo ya Chama ni kuwatibu wanachama wake.Swala la Tiba kwa wananchi linashughulikiwa na Serikali kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Wananchi wanalipa Kodi ili kusaidia upatikanaji wa Huduma bora za Jamii ikiwemo Matibabu bora.Kama kuna Mtanzania anayeteseka kwa kukosa huduma bora za Afya anayetakiwa awajibike ni Serikali.
Mkuu nazungumzia viongozi wa kitaifa wa chama(chadema)
 
Back
Top Bottom