Tusisahau kuwa na maji yale yanamwagilia mbogamboga nyingi ambazo zinasambazwa maeneo mbalimbali Dar es Salaam. Kuna wakati pia ulifanyika utafiti na kukuta maji yale yana mabaki ya Zebaki ambayo ni hatari sana. Kumbuka pia shimo la taka maeneo yale ambayo uchafu wote ulitiririka ndani ya mto ule, unajua tena Dar hakuna dampo la taka hatarishi kila mahali zinatupwa. Tutakufa, cancer leo hii ni za ajabu hata watoto wadogo wanaugua cancer. Inatisha.
Halafu ni kwa nini serikali kama kweli inajali wat wake isiamuru viwanda vyote vikahamishiwa maeneo ya mbali kama ilivyo kwa nchi nyingine?? Imagine kiwanda cha KTM, Serengeti brewaries, Chang'ombe eneo la viwanda limepitwa na wakati kabisa, vinatakiwa vihamishwe. Eti kuna waziri mwenye dhamana ya Mazingira na Baraza la Taifa la Mazingira, na vyote hivi vipi chini ya ofisi kubwa yenye madaraka!!!