Masikini Wee Jiji la Dar es salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masikini Wee Jiji la Dar es salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kichankuli, Aug 24, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 857
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Jana kwenye kituo cha Runinga cha Chanel 10 walirusha habari ikionyesha uchafuzi wa mazingira wa hali ya juu ambapo kuna kiwanda kimoja kimeruhusu sumu kutiririka kwenye bonde la Mto Msimbazi na kusababisha mauaji ya Samaki ambao walionyeshwa. Lakini pia kuna Mama mmoja alieleza kuwa kuku wake kadhaa walikufa baada ya kunywa maji ya mto huo.

  Lakini kingine kilichojitokeza sambamba na hilo ni pale Mkuu wa Wilaya (wakati akitembelea eneo hilo kujionea uchafuzi wa mazingira huo) alipokutana uso kwa uso na Masela wakiendelea kuyasaka mahela kwa kuuziana Bangi na wengine wakilivita Bangi hilo kwenye Bonde hilo. Jamaa sijui ndo Bongi lilishawakolea au kutomfahamu mwenye himaya ya Wilaya hiyo wala hawakuonyesha msituko.

  Mh. Magufuli kuna tofauti gani ya hawa wenye Kiwanda na wale Wavuvi wanaotumia Makokoro na Baruti, au hawa Samaki siyo wa Wizara yako.

  Hili Jiji letu litaendelea kuwa chafu hivi mpaka lini/ Lukuvi uko wapi?
   
 2. B

  Bobby JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Ahsante kwa post kuhusu Dar. Uchafu ni kero mojawapo inayolikabili jiji letu. Kuhusu miundombinu hiyo ndio usiseme. Kuna mtaro mmoja hapo baada ya shoppers plaza kama unaenda Kawe unakaribia kukata barabara na no one cares mpaka ukate ndio watashtuka. Kuna kipindi ninajiuliza hata kama tunauongozi hapa Dar au, ama kama upo basi ni kwa ajili ya kukusanya mapato na kuyatumbua basi na si zaidi ya hilo. I'm sure baadhi yetu tumefika Nairobi ambayo ilivyokuwa miaka mi2 iliyopita si ilivyo sasa. Nairobi ni safi utaipenda. Kuna sababu nyingi lakini mojawapo ni kuwa serikali ya Kenya tofauti na ya kwetu inaelewa umuhimu wa kipekee wa Nairobi kama kioo cha Kenya. Nairobi wana Waziri maalumu kabisa anayehusika na ustawi wa jiji si madawani wa darasa la nne kama hapa kwetu. Wana mpango wa kulifanya Nairobi the best city in Africa nadhani by 2025 kama sikosei.

  Kituko ni hapa kwetu. Miezi kadhaa iliyopita jk aliwatukana madiwani kwamba hawako serious na jiji na mambo kibao aliyasema. So far hakuna kilichofanyika na huyo aliyewatukana yuko busy mikoani huko akifungua hotel na guest houses kisha anarudi kupumzika kwenye dampo dar na hakuna anachofanya. Me nadhani ifike mahali tuwe serious jamani kama madiwani wameshindwa kazi tutakaa tu chini na kuendelea kupata aibu kama nchi? Ni uwendawazimu kutarajia majibu tofauti kwa kile kile unachofanya kila siku. Dar sio Singida ya kuwaachia madiwani enyi wenye mamlaka mnatudhalilisha. Mwezi wa Saba nilipata mgeni toka South Africa, aliyosema kuhusu Dar ni aibu tupu japo ni ya kweli tupu.
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa Mkoa, Meya na wakazi wanasubiri KAMATI TEULE na TAMKO LA MH.RAIS ili kushughulikia tatizo hili!!!
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tunasubiri maafa zaidi yatoke ndipo tuunde tume ya watu 10 kwa muda wa miezi 3 tupeleke ripoti halafu ripoti ianze kusomwa kwa kipindi tena cha miezi3 ndipo majibu yatoke uchaguzi umewadia tupige kampeni kwenye bonde la mto msimbazi tushinde!!!
   
 5. w

  wasp JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katibu Mkuu wa SISIEM Mtukufu Yusuf Makamba anasema madiwani ni wa SISIEMU, Meya ni wa SISIEMU, DC na RC ni makada wa SISIEMU. Kwa hiyo uchafu ni jadi ya SISIEMU ndio maana wameshika hatamu. Kama kawaida sasa ni wakati wa kuunda tume ya kuchunguza hali ya uchafu wa jiji la DSM ili watu wapate mshiko wa mwezi mtukufu wa Ramadhani maana fedha ya futari inatakiwa.
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hii ni hatari kubwa. nakumbuka mto msimbazi si ule unaopita barabara ya port access kuelekea jangwani .

  basi wengi wataathirika maana yake umepita katikati ya makazi ya watu na watu wanautumia sana.

  Tuombe yasije tokea kama yale ya tarime
   
 7. K

  Kelelee Senior Member

  #7
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni aibu kusema unaishi dar es salaam. mimi ni mtumiaji mzuri sana wa kituo cha dala dala cha mwenge yaani hali ya pale ni mbaya mbaya ajabu ....the whole place stinks 24/7....na hiyo ni reflection tu ya maeneo mengi sana ya jiji la dar es salaam...shame shame shame.......sisi wakazi wa dar es salaam tujirekebishe..
   
 8. Koiya

  Koiya Member

  #8
  Aug 24, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa unafikiri matatizo kama hayo yatataliwa vipi wakiti viongozi wenyewe kuwaona mpaka zianze kampeni au yatokee maafa mimi binafsi yangu mkuu wangu wa wilaya simjui hata sura yake sasa matatizo yataisha vipi ila kwa sababu kampeni zinaanza wote nisio wajua nitawajua kuanzia mkuu wa Mkoa, Wilaya Mjumbe hata wa selikali za mitaa pia nitawaona.
   
 9. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kuna study ilifanyika recently kwa kweli mto msimbazi uko very polluted, kuanzia heavy metals n.k. Haufai kabisa kwani maji taka ya TBL, maji ya vyoo majumbani yote yanaelekezwa mto msimbazi and no body cares!!
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Tusisahau kuwa na maji yale yanamwagilia mbogamboga nyingi ambazo zinasambazwa maeneo mbalimbali Dar es Salaam. Kuna wakati pia ulifanyika utafiti na kukuta maji yale yana mabaki ya Zebaki ambayo ni hatari sana. Kumbuka pia shimo la taka maeneo yale ambayo uchafu wote ulitiririka ndani ya mto ule, unajua tena Dar hakuna dampo la taka hatarishi kila mahali zinatupwa. Tutakufa, cancer leo hii ni za ajabu hata watoto wadogo wanaugua cancer. Inatisha.

  Halafu ni kwa nini serikali kama kweli inajali wat wake isiamuru viwanda vyote vikahamishiwa maeneo ya mbali kama ilivyo kwa nchi nyingine?? Imagine kiwanda cha KTM, Serengeti brewaries, Chang'ombe eneo la viwanda limepitwa na wakati kabisa, vinatakiwa vihamishwe. Eti kuna waziri mwenye dhamana ya Mazingira na Baraza la Taifa la Mazingira, na vyote hivi vipi chini ya ofisi kubwa yenye madaraka!!!
   
 11. N

  Nacho cha Ruwa Member

  #11
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa mtizamo wangu Dar haikidhi ipasavyo kuwa kwenye hadhi ya jiji vile huduma muhimu za kijamii kama vile public toilets katikati ya jiji hazipo kabisa na cha kutisha zaidi kuna pavement kubwa tu maeneo ya posta mpya hapa inamwaga maji taka kando kando ya barabara ni mwaka wa pili sasa wala hakuna chochote kile kinachofanyika,hiyo harufu inayotoka hapo ooooohh! olee wao ndo wanatupunguzia life span yetu hizi hivi tu maisha yenyewe mafupi bado wanazidi kutumaliza tu.
  Yu wapi mwenye mamlaka,uwezo na sauti ya kutaka kutekeleza jambo jema kwa Watanzania?hela zetu lakini bado wanashindwa kuonesha dira!
   
 12. A

  Abdul Member

  #12
  Aug 24, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tatizo nchi hii watu wanapenda rushwa, wakaguzi wakienda kiwandani wanapewa kitu kidogo, sungusungu irudi lyatonga uko wapi?
   
 13. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Balaa jipya tena hilo tena ndani ya Dar. Serikali mpooooooooo? Lukuvi je?
   
Loading...