Masikini Haji Manara!

Simba ni kichaka cha wahalifu!!!

Aden Rage alishakula mvua kadhaa kutokana na uhalifu hata kama baadae alikata rufaa...

Zakaria Hans Pope huyu ndo kabisa manake alifikia hadi kufanya uhaini!!!

Haji Manara; huyu ni mjanja mjanja wa mjini... maneno meeeeeeeeengi kumbe tapeli tu!!!
 
....... Yalishapita hayo!..."Everyone has his/her own past dark side and don't allow your past to ruin your future"
 
LILE sakata la tuhuma za utapeli linalomkabiri Katibu Mwenezi wa zamani wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara, leo limeingia katika hatua nyingine baada ya katibu huyo kupewa dhamana kisha ghafla kudakwa tena na polisi wa kituo kikuu jijini Dar es Salaam nje ya Mahakama ya Kinondoni. Kamanda huyo wa zamani wa CCM alidakwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni ambako anakabiliwa na kesi ya utapeli wa magari. Alikamatwa na askari watatu ambao walijitambulisha wanatoka kituo kikuu, walimwambia Haji kuwa ana tuhuma zingine nzito za utapeli wa magari mengine matano na shauri lake limefunguliwa katika kituo hicho.




1266935433_manara.jpg

Manara akiwa amezungukwa na askari kanzu wa kituo kikuu cha polisi mara baada ya kutoka mahakamani.

1266935433_manara_2.jpg

Manara akiwa chini ya ulinzi akielekezwa kuingia kwenye gari.

1266935433_manara3.jpg

Gari lililombeba Manara likiwa tayari kuondoka kuelekea kituo kikuu cha polisi.

Wachezaji wa 5imba wachunge sana kutapeliwa pikipiki zao na Manara. Amebobea kwenye taaluma hiyo.
 
Simba ni kichaka cha wahalifu!!!

Aden Rage alishakula mvua kadhaa kutokana na uhalifu hata kama baadae alikata rufaa...

Zakaria Hans Pope huyu ndo kabisa manake alifikia hadi kufanya uhaini!!!

Haji Manara; huyu ni mjanja mjanja wa mjini... maneno meeeeeeeeengi kumbe tapeli tu!!!
Umemsahau Hasani Hasanoo alikamatwa na Copper za wizi,Golikipa wao Mambosasa aliiba godoro guest na Abdi Banda,Michael Paul na Christopher Alex wakiwa Simba walishapata misala ya wizi wa magari
 
Mimi ninachotaka kujua kama ni kweli jamaa ni tapeli au anaonewa. Mwenye adat azishushe basi humu
KATIBU Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara, amejiuzulu wadhifa huo baada ya kuhusishwa na tuhuma za utapeli. Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kirumbe Ng’enda, jana alilithibitishia gazeti hili kuwa wamekubali barua ya kujiuzulu kwa Manara iliyowasilishwa kwao juzi.

Manara aliyechaguliwa kushika wadhifa huo miaka miwili iliyopita, amekumbwa na kashfa ya kukodisha magari kwa watu mbalimbali yanayofikia 40, na kuyaweka rehani kwa watu mbalimbali Dar es Salaam na mikoa mingine nchini.

Anadaiwa kukodisha magari hayo kutoka katika kampuni tofauti za kukodisha magari nchini akitumia jina la CCM kwamba inayahitaji kwa kazi maalumu. Anadaiwa kuingia makubaliano ya kukodisha magari hayo kwa gharama ya Sh 60,000 kwa siku.

Tayari suala lake liko katika vyombo vya Dola baada ya wenye magari wanaotuhumiwa kutapeliwa na Katibu Mwenezi huyo kuwasilisha malalamiko yao kwa Polisi na sasa suala hilo linashughulikiwa na Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Lakini jana Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, alisema barua ya Manara ya kujiuzulu wadhifa wake imekubaliwa na suala lake linaachwa katika vyombo vya Dola vifanye kazi yake.

“Ni kweli jana (juzi) Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, ilikutana na mbali na ajenda nyingine, ilikutana kupokea na kujadili barua ya Haji Manara ya kujiuzulu wadhifa wa Katibu Mwenezi.

“Halmashauri Kuu ya Mkoa imekubali uamuzi wake wa kujiuzulu na haikutoa tamko lolote jingine, badala yake imeviachia vyombo vya Dola vifanye kazi yake kwa kuwa suala hilo limefikishwa huko,” alisema Ng’enda alipozungumza na gazeti hili kwa simu jana.

Alisema katika barua yake ya kujiuzulu, Manara amesisitiza kuwa hilo ni suala lake binafsi, na halina uhusiano na chama hicho, na atapata fursa ya kulielezea vizuri katika siku zijazo. Lakini kwa mujibu wa Ng’enda, Manara amewaomba radhi wana-CCM wenzake, viongozi na wakereketwa wa chama hicho kutokana na namna suala hilo lilivyowasononesha, na kwamba amejiuzulu ili kukisafisha chama na kashfa hiyo.

Katibu wa CCM Mkoa alisema kikao cha juzi chini ya Mwenyekiti wao, John Guninita hakikuwa na pingamizi na uamuzi wa Manara kwa sababu suala hilo linazungumzika. Kuhusu kama CCM ilikuwa na taarifa za utapeli unaodaiwa kufanywa na kiongozi wake, Ng’enda alisema mmoja wa walalamikaji alifikisha suala hilo kwao na baada ya kuoneshwa nyaraka zilizokuwa na nembo za CCM, lakini zikagundulika ni za kughushi, walimshauri aende katika vyombo vya Dola.

“Sisi ndio tuliomshauri aende katika vyombo vya Dola baada ya kumueleza kuwa CCM haihusiki na suala hilo na hata nembo zilizotumika, zimeonekana ni za kughushi.

Kwa hiyo, hatukuficha kitu na ndio maana tulimpa ushirikiano mhusika kwa sababu sisi sio chama cha kuficha madhambi,” alisema.

Aidha, alisema kwa ujumla CCM ni chama cha binadamu, na akafananisha na familia inayoweza kuzaa watoto ambao miongoni mwao wakawemo mchungaji, shehe au mwizi; kwa hiyo, lililomkuta Manara linaangukia humo, ingawa alisisitiza, ni Mahakama pekee inayoweza kusema kada huyo ni mkosaji.

“Haya yanatokea kwa sababu chama ni cha binadamu, sisi kama taasisi tuna watu wa aina mbalimbali, lakini la msingi ni kuzingatia maadili na miiko ya uongozi, na huo ndio mwito wetu kwa wana-CCM wengine.

Tuzingatie maadili ya uongozi,” alisema Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam. Manara hakupatikana jana kuzungumzia hatima yake baada ya kujiuzulu, lakini kijana huyo machachari alieleza wiki iliyopita anapanga kulizungumzia atakapozungumza na wanahabari.
 
Back
Top Bottom