Masikini elimu ya tan'ka, mwanafunzi sekondari hajui kuandika jina lake

WA MAMNDENII

JF-Expert Member
Jun 5, 2010
344
57
katika gazeti la mwananchi la leo tarehe 12 may kuna taarifa ya mkuu wa shule moja iliyopo kata ya majohe kuwa asilimia themanini 80% ya wanafunzi wanaopokelewa shuleni hapo hawajui kusoma wala kuandika majina yao ,na kwamba wengi wao walipata alama ya asilimia saba katika masoma ya hisabati na kiingereza. jamani mi najiuliza kama hii taarifa ni ya kweli yaani 80% hawajui
kusoma na kuandika? jamani hili taifa tunalipeleka wapi. elimu ya wanetu huko kwenye chimbuko la kukuza uelewa kwa bongo za watoto imezorota kwa kiasi kwamba walimu wameamua bora liende. Matokeo bora kwa wanafunzi imekuwa sio lengo na dhumuni la shule zetu za kina kayumba. Serikali sijui inaliona hili au sijui ina mikakati yoyote au ndio sera za elimu bora ipo kwenye mafaili na kuhubiri kwenye majukwaa ya siasa mipango isiyotekelezeka.

Sipati picha baada ya miaka kadhaa ijayo taifa letu lilojaaliwa tunu nyingi litakuwa katika mustakabali gani kwani kundi la vijana wengi watakaokuwa wanazagaa mitaani wakiangaika huku na huko wakitafuta namna ya kujikimu katika mazingia magumu huku wakishuhudia wachache wakifaidi kanchi ketu sote.
 
Back
Top Bottom