Masikini CCM! Mbeleko tegemezi ya polisi yazidi kukatika, kipi cha kufanya isizidi kuadhirika?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Ni baada ya RPC Mwanza kukataa agizo la kamati ya ulinzi ya wilaya (kamati za fitina) kuwakamata wabunge wa Chadema.

Nawaomba CCM wakae kitako na kutafakari (soul searching) angalau wawe wanajenga hoja za msingi kujibu zile za Chadema, hasa kuhusu wizi na ufisadi dhidi ya Watanzania! Acheni polisi wafanye kazi zao halisi kwa umma!

 

Hawana habari kwamba vya chee vinaumiza -- in fact vinaibisha.
 
Mabavu yao na sasa wafikia ukingoni. Nimesikia wameangukia pua huko Mwanza tena, yule diwani msaliti waliompitisha kuwa Meya kwa mabavu katimuliwa na mahakama! Aibu ilioje hiyo!

Huyu PM ni mfu -- anaruhusu madudu katia halmashauri ambayo yanakuja kuiaibisha ofisi yake!
 
Hali ni mbaya sana kwa CCM hapa Mwanza
1/Wameshindwa rufaa ya jimbo la Ilemela
2/Diwani Matata kashindwa mahakamani.
3/RPC kagoma kuwakamata wabunge wa CHADEMA
 
WOKOVU UNAKARIBIA........Muda si mrefu polisi nao watachoka, maana wataona wanabeba lidude ambalo halibebeki, wataamua kulitupa chini hapo ndio utaona kuwa CCM hawana pumzi ya kumaliza mchezo kaitka dakika 90, ni wepesi mno na ushindi 2015 njia ni nyeupe.
 
Big up sifongo, ccm ni TUFE ZITO twasubiri litupwe chini, then tulisahau kama lili-exist in the universe.
 
Hali ni mbaya sana kwa CCM hapa Mwanza
1/Wameshindwa rufaa ya jimbo la Ilemela
2/Diwani Matata kashindwa mahakamani.
3/RPC kagoma kuwakamata wabunge wa CHADEMA

Yule Shabab Kinana kaanza na gia mbaya - au nuksi inamuandama kutokana na ufisadi wake.
 
Mkuu ndicho walichobaki nacho ccm na heko kwako RPC kwani inaonyesha wewe unajua nini maana ya kiapo ulichokula maana wenzako wanaapa kishahi tu. Pia ccm mjue mwisho wa ubaya ni aibu nayo aibu ndo imewakaribia sasa
 
Friday, December 14, 2012


Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Evarist Mangu, amesema kuwa hawezi kumkamata Mbunge wa Nyamagana kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ezekiah Wenje, kwa kuwa hajapata taarifa rasmi.

More... See 1st post

 
Naona RPC anashuhudia UNYAMA wa CCM Inavyowafanyia CHADEMA Mkoani MWANZA; Yeye kama POLISI anaona Sasa ATUKUZE na KUFUATA SHERIA... zaidi ya Unyama wa CCM
 
Kwa nini mwandishi hakumuliza kamanda wa Polisi wa wilaya ya Nyamagana ambaye aliagizwa na Kamati ya usalama ya wilaya ambaye ndiye anawajibika na maelekezo haya. Kinyume chake ameenda kumuuliza kamanda wa mkoa alitarajia jibu gani zaidi ya alivyjibiwa?
 
Muone huyo meya wa kichina bwana matata kama vile kachaguliwa kwa uwazi na haki ; shame on him
 
Kuna post humu ilisema matata katimuliwa!! Mara tena hii hapa!!inanichanganya,ngoja niirudie ile post kama bado itakuwepo.
 
Na ujue kwamba mbeleko ya polisi hutengenezwa kwa nguo ya turubai. sasa kama hii inakatika, basi imekula kwao CCM. I hate that party!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…