Mashushushu wazima mamilioni ya mgombea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashushushu wazima mamilioni ya mgombea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jun 10, 2009.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  • Zacheleweshwa benki Dar zisivuruge kura Dpdoma
  • Ni fedha za kifisadi katika uchaguzi wa Wazazi  Na waandishi wetu Dar na Dodoma
  Raia Mwema Juni 10 – Juni 16, 2009


  MAMILIONI ya fedha zilizokuwa ziingizwe kwenye harakatui za kusaka ushindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa jumuiya ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), wiki ilyopita zimezua utata baada ya vyombo vya dola kuhakikisha haziingii Dodoma kuharibu uchaguzi, Raia Mwema limefahamishwa.

  Imefahamika kwamba fedha hizo zilizozuiwa na watu walioelezwa kuwa ni "maalumu" zilikuwa ziingizwe kwenye akaunti iliyopo benki moja maarufu nchini, tawi la Dodoma.

  Zilikuwa zimepangwa kugawanywa kwa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi. Wagombea katika uchaguzi huo walikuwa ni balozi Athumani Mhina, Abdallah Bulembo na Esther Nyawazwa.

  Habari zilizopatikana zinasema baada ya kampeni kuonekana kuwa ngumu kwa pande zote, mkakati wa mwisho wa mgombea mmoja ulikuwa ni kutumbukiza pesa (Sh milioni 400) ambazo zilikuwa ziingizwe kwenye akaunti moja ya benki hiyo tawi la Dodoma ili zigawiwe; hivyo kumalizia kazi ya kuwaweka sawa wapiga kura, na hatimaye kufanikisha ushindi wa mgombea husika.

  Hata hivyo, inaelezwa kuwa nyendo za kundi la mgombea husika zilikuwa zikifuatiliwa kwa karibu na vyombo vya dola vilivyohakikisha fedha hizo haziingii kwenye akaunti hiyo kutoka Dar es Salaam ili zisigawanywe kwa wapiga kura Dodoma na kuvuruga uchaguzi.

  "Watu walikuwa wamejipanga vizuri sana, sijui kwa maelekezo ya nani, lakini walikuwa makini sana kuhakikisha kasi ya mbinu chafu haitawali uchaguzi. Kwa hiyo, wakajua kuwa kuna fedhazimeingizwa kutoka kwa kundi fulani linaloshirikisha wanasiasa na wafanyabiashara wenye tatizo la kimaadili… ni fedha nyingi kwa hiyo kazi ikafanyika kuwa ni lazima kuhakikisha hizo fedha hazitoki benki kwa wakati uliokusudiwa na wahusika wa kundui hilo ili kwenda kugawa rushwa," alisema mtoa habari hizo.

  "Sasa hawa watu na hasa viongozi wao katika kufanikisha mkakati huo walikwenda benki kuchukuwa fedha lakini huko walikutana na kikwazo, fedha hazikutoka kwa wakati…wakahangaika lakini hawakufanikiwa.

  "Wakaamua kwenda kumuona meneja kujua kuna tatizo gani, huko wakakwama wakiwa wamejibiwa kwamba kulikuwa na matatizo ya kawaida ya shughuli za kibenki hivyo fedha hizo zingechelewa kuchukuliwa," kinasema chanzo cha habari za mkakati huo uliofeli.

  Habari ndani ya vyombo vya dola vimethibitisha kwamba wahusika waliotoa fedha hizo jijini Dar ves Salaam kwa kutumia uzoefu wao katika sekta ya fedha walikuwa wameweka mkakati wa kukiuka taratibu za kibenki ili fedha hizo ziwahi kuingia katika akaunti iliyokusudiwa mjini Dodoma, lakini baada ya dola kuingilia kati fedha hizo zikalazimika kupitia ‘chekeche' la kawaida la fedha.

  "Kwa kawaida fedha nyingi kama hizo (milioni 400) haziwezi kupitishwa kwa haraka haraka katika mfumo wa kibenki hasa kama mmoja wa wahusika hana kawaida ya kupokea ama kuingiza fedha nyingi kiasi hicho, kwa hiyo ni lazima ufuate utaratibu wa kuzingatia Sheria ua Uthibiti wa Fedha Haramu kupitia kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU), na ndicho kilichowaponza hao jamaa," kinaeleza chanzo cha habari ndani ya serikali………..

  ………habari zaidi ziko katka Raia Mwema ya leo UK wa 3.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hiyo benki, siyo ile ile ya kifisadi iliyofanikisha utolewaji wa malilioni ya fedha za Kagoda -- fedha taslim over the counter? Nadhani wahusika wale wa Kagoda ni hao hao waliojaribu kufanikisha uhamishaji na utolewaji wa fedha hizii milioni 400. Bahati nzuri mara hii walikwama kwani hiyo benjki bila shaka imejirekebisha.

  Pili, hizo pesa, milioni 400 zitachunguzwa ni za nani, na uhalali wa upatikanaje wake uko sawa? Ni lazime ufanyike uchunguzi. Kama mnafikiria RA anahusika hapa, basi nami nafikiria hivyo hivyo.

  Tatu, na hapa nataka nielimishwe kidogo -- ni sawa kwa vyombo vya dola kutumika katika mienendo ya chaguzi ndani ya vyama vya siasa? Hapa nina maana kuna uwezekano wa vyombo hivyo kutumika vibaya -- yaani iwapo safari hii vilitumika kuzuia rushwa isitendeke kwa kundi moja, siku nyingine vinaweza kutumika kufanikisha rushwa katika kundi jingine.

  Inavyoonekana hapa makundi ndani ya CCm ndiyo yamejinyakulia uwezo wa kuviamuru vyombo hivyo kufanya vinavyofanya.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Mashushushu wazima mamilioni ya mgombea

  Mwandishi Wetu Juni 10, 2009

  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  Zacheleweshwa benki Dar zisisivuruge kura Dodoma

  Ni fedha za kifisadi katika uchaguzi wa Wazazi
  MAMILIONI ya fedha zilizokuwa ziingizwe kwenye harakati za kusaka ushindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), wiki iliyopita, zimezua utata baada ya vyombo vya dola kuhakikisha haziingii Dodoma kuharibu uchaguzi, Raia Mwema limefahamishwa.

  Imefahamika kwamba fedha hizo zilizozuiwa na watu walioelezwa kuwa ni "maalumu" zilikuwa ziiingizwe kwenye akaunti iliyopo benki moja maarufu nchini, tawi la Dodoma. Zilikuwa zimepangwa kugawanywa kwa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi. Wagombea katika uchaguzi huo walikuwa ni Balozi Athuman Mhina, Abdallah Bulembo na Esther Nyawazwa.

  Habari zilizopatikana zinasema baada ya kampeni kuonekana kuwa ngumu kwa pande zote, mkakati wa mwisho wa mgombea mmoja ulikuwa ni kutumbukiza pesa (Sh. milioni 400) ambazo zilikuwa ziingizwe kwenye akaunti moja ya benki hiyo tawi la Dodoma ili zigawanywe; hivyo kumalizia kazi ya kuwaweka sawa wapiga kura, na hatimaye kufanikisha ushindi wa mgombea husika.

  Hata hivyo, inaelezwa kuwa nyendo za kundi la mgombea husika zilikuwa zikifuatiliwa kwa karibu na vyombo vya dola vilivyohakikisha fedha hizo haziingii kwenye akaunti hiyo kutoka Dar es Salaam ili zisigawanywe kwa wapiga kura Dodoma na kuvuruga uchaguzi.

  "Watu walikuwa wamejipanga vizuri sana, sijui kwa maelekezo ya nani, lakini walikuwa makini sana kuhakikisha kasi ya mbinu chafu haitawali uchaguzi. Kwa hiyo, wakajua kuwa kuna fedha zimeingizwa kutoka kwa kundi fulani linaloshirikisha wanasiasa na wafanyabiashara wenye tatizo la kimaadili...ni fedha nyingi kwa hiyo kazi ikafanyika kuwa ni lazima kuhakikisha hizo fedha hazitoki benki kwa wakati uliokusudiwa na wahusika wa kundi hilo ili kwenda kugawa rushwa," alisema mtoa habari huyo.

  "Sasa hawa watu na hasa viongozi wao katika kufanikisha mkakati huo walikwenda benki kuchukua fedha lakini huko walikutana na kikwazo, fedha hazikutoka kwa wakati...wakahangaika lakini hawakufanikiwa. Wakaamua kwenda kumwona meneja kujua kuna tatizo gani, huko wakakwama wakiwa wamejibiwa kwamba kulikuwa na matatizo ya kawaida ya shughuli za kibenki hivyo fedha hizo zingechelewa kuchukuliwa," kinasema chanzo cha habari za mkakati huo uliofeli.

  Habari ndani ya vyombo vya dola zimethibitisha kwamba wahusika waliotoa fedha hizo jijini Dar es Salaam kwa kutumia uzoefu wao katika sekta ya fedha walikuwa wameweka mkakati wa kukiuka taratibu za kibenki ili fedha hizo ziwahi kuingia katika akaunti iliyokusudiwa mjini Dodoma, lakini baada ya dola kuingilia kati fedha hizo zikalazimika kupitia ‘chekecheke' la kawaida la fedha.

  "Kwa kawaida fedha nyingi kama hizo (milioni 400) haziwezi kupitishwa kwa haraka haraka katika mfumo wa kibenki hasa kama mmoja wa wahusika hana kawaida ya kupokea ama kuingiza fedha nyingi kiasi hicho, kwa hiyo ni lazima ufuate utaratibu kwa kuzingatia Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu kupitia kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU), na ndicho kilichowaponza hao jamaa," kinaeleza chanzo cha habari ndani ya serikali.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, uhakiki uliokuwa ukifanywa na vyombo husika vikiongozwa na FIU ulisababisha uchelewesho mkubwa wa fedha hizo kuingia kwenye akaunti husika mjini Dodoma, hadi uchaguzi ulipokamilika na imeelezwa kwamba fedha hizo zinaweza zisiingizwe tena katika akaunti hiyo kwa maelekezo mapya kutoka kwa wahusika ambao wamefahamishwa kuhusu utaratibu huo.

  Mbali na tukio hilo lililozimwa kwa mbinu za kishushushu, vituko vingine vilivyoibuka katika uchaguzi huo ni pamoja na kuvunjwa kwa vioo vya gari la upande mmoja kati ya kambi zilizokuwa zikichuana vikali, pamoja na kuumizwa kwa baadhi ya wapambe na wana-CCM, ikidaiwa kuwa vurugu hizo zilifanywa na kundi la mgombea Abdallah Bulembo dhidi ya kundi la Balozi Athuman Mhina, ambaye hata hivyo ndiye aliyeshinda uchaguzi huo kwa kura 60 zaidi ya mshindani wake wa karibu, Bulembo.

  Habari zinasema matukio hayo ya ugomvi yalimkera sana Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kiasi kwamba katika hotuba yake ya kufungua mkutano wa uchaguzi huo, mwishoni mwa wiki iliyopita, alisema wahuni walikuwa wameshirikishwa kwenye kampeni hizo na kuonya siku nyingine wagombea wasichukue au kushirikisha wahuni katika kampeni zao.

  "Ninyi wagombea acheni kuleta wahuni katika uchaguzi kama huu, angalieni mlivyotia aibu kwa chama chenu, yaani mmeufanya uchaguzi siku hizi kuwa kama vita, tunakwenda wapi ndugu zangu.

  "Ndiyo maana siku zote jumuiya hii imekuwa ikifanya mabadiliko ya viongozi kila kunapokucha, kwa mfano, ndani ya miaka minne mmebadilisha wenyeviti wawili, makatibu wanne na makamu wenyeviti wawili, hii si aibu jamani? Mbona jumuiya nyingine kuko shwari," alisema.


  Aliwataka wanachama wa jumuiya hiyo kuwachagua viongozi wa wazazi kwa utashi wao na si kwa kuzingatia maneno ya wapambe akitumia kauli mbiu kuwa "maneno ya kuambiwa ni lazima mtu achanganye na akili yake mwenyewe."

  Uzoefu unaonyesha kuwa chaguzi mbalimbali za jumuiya za CCM zimekuwa zikiandamana na malalamiko mengi yakiwamo matumizi ya rushwa katika kuwashawishi wapiga kura kumchagua mgombea na hasa atakayetoa fedha nyingi kuliko mwenzake au wenzake.

  Kati ya chaguzi zilizozua malalamiko ya wazi ni wa Mwenyekiti na viongozi wengine wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambao Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Sophia Simba, alichaguliwa akichukua nafasi aliyoachwa wazi na Anna Abdallah aliyestaafu.

  Wakati wa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa uchaguzi huo uliomhusisha Rais Jakaya Kikwete, Anna Abdallah katika hotuba yake ya kumkaribisha Kikwete kufungua uchaguzi huo aliweka bayana kuwa "hajawahi kuona uchaguzi wenye matumizi makubwa ya fedha (rushwa) kama huo," lakini hata hivyo, kauli yake hiyo ilibaki tu katika hotuba.

  Uchaguzi mwingine uliobua malalalmiko ya matumizi ya rushwa ni wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), ambamo Rais Kikwete alilazimika kuwaeleza vijana kuwa ni vema wakachagua viongozi wao bila kuingiliwa na wanasiasa wengine nje ya umoja huo kwa kutumia mbinu zozote zikiwamo za matumizi ya fedha. Kwa matatizo hayo aliyotaja Rais Kikwete, baadhi ya wagombea walilazimika kuenguliwa na hatimaye kiti cha Mwenyekiti kikamwendea Masauni Yusuf Masauni.

  Matumizi makubwa ya fedha katika chaguzi za CCM na jumuiya zake yameongezeka kwa kasi katika miaka ya karibuni kiasi cha kuwafanya watu wasio na fedha kutofikiria kabisa kuingia katika siasa na kwa upande mwingine hali hiyo imesababisha watu wenye fedha watumie mwanya huo kusimika viongozi kwa maslahi yao.

  Pamoja na malalamiko hayo kuhusu rushwa ndani ya chaguzi za CCM na jumuiya zake, hakuna hatua zozote nzito za kisheria zilizowahi kuchukuliwa kwa kuwafikisha wahusika mahakamani ama kuwasimamisha uongozi.
   
 4. I

  Ipole JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyo mtoa habari hakusema ni nani aliyehusika kutoa hayo mamilioni na angeyarudishaje?
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mafisadi si wanajulkana? Hatuna haja kuwataja majina maana wote wanajulikana tena kwa majina,wengine watagombea urais mwakani.Thanks JK kwa kuwa thibiti
   
 6. I

  Ipole JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante ndugu yangu wa tukuyu kwa maelezo hayo mafisadi wanajulikana ni wengi sasa walitoa wote na ukiwataja kwa majina kuna tatizo gani wana JF tukiwajua kwa majina?
   
Loading...