Mashushushu wavamia wanahabari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashushushu wavamia wanahabari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 10, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]

  • WACHUKUA PICHA ZA MAREHEMU HOTELINI

  na Waandishi wetu


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]KUNDI la watu wanaoaminika kuwa maafisa wa Usalama wa Taifa limevamia hoteli kadhaa jijini Dar es Salaam walizofikia viongozi wa klabu za waandishi wa habari kutoka mikoa yote hapa nchini wanaohudhuria mkutano mkuu ambao utatumika kutoa tamko rasmi juu ya mauaji ya mwandishi Daudi Mwangosi aliyeuawa na polisi hivi karibuni.

  Habari za kuaminika zimebainisha kuwa zaidi ya maafisa
  usalama nane walivamia hoteli kadhaa walizofikia waandishi hao, ikidaiwa kusaka kila aina ya taarifa na nyaraka zinazohofiwa kuwa mikononi mwao na ambazo zinaaminika kuwa zitaiumbua serikali ikiwa zitachapishwa katika vyombo vya habari.


  Imedaiwa kuwa, hadi sasa maafisa hao wamefanikiwa kunasa lundo la picha za marehemu Mwangosi alizopiga wakati wa uhai wake, zikiwemo zile zinazoonesha matukio yote yaliyotokea kwa siku nzima, kabla na wakati wa vurugu na tukio zima la kupigwa na kuuawa kwake.


  Maafisa hao inasemekana wanatafuta pia picha hasa za waandishi wa mikoa ya Iringa na Mbeya ambazo zilipigwa kuonesha jinsi polisi walivyokuwa tayari na kuanza kuwaandama waandishi wa habari watatu ambao inadaiwa kuwa walikuwa walengwa pia wa tukio hilo.


  Upelelezi huo unakuja kukiwa na taarifa kwamba, waandishi wa habari walifanikiwa kunasa mazungumzo ya polisi mkoani Iringa yanayoanika waziwazi kile kilichoongelewa na kukubalika kifanyike katika mikutano ya CHADEMA itakayofuata.


  Kitu kingine kinachosakwa na maafisa hao ni madai kwamba waandishi wa habari, kutoka mkoani Mbeya na wale wa Mwanza, wanazo nyaraka na vielelezo sahihi vinavyoonesha mauaji yenye utata ya aliyekuwa mtangazaji wa ITV, John Lubungo na mwandishi wa habari wa Mwanza, Richard Masatu ambaye awali alikuwa mwandishi wa habari wa kujitegemea kabla ya kuanzisha gazeti la kasi mpya.


  Inasemekana kuwa Masatu siku ya kifo chake alipigiwa simu akiwa anarudi mjini Mwanza kutoka kwenye maonesho ya Nanenane mwaka jana yaliyokuwa yanafanyika mpakani mwa vitongoji vya Igoma na Kisesa, na kukutana na afisa mmoja wa polisi na wa serikali ya wilaya katika baa moja, na baada ya kuachana nao, muda mchache aliokotwa mtaroni eneo la Igoma akiwa mahututi na alifia katika hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.


  Maafisa usalama hao, sasa imedaiwa kuwa wanasaka nyaraka za kifo hicho ambacho kama kilivyokuwa kile cha Mwangosi, polisi walitoa ripoti iliyokinzana kwa kiwango kikubwa na ile ya madaktari wa hospitali ya rufaa ya Bugando.


  Katika ripoti ya polisi, ilidaiwa kuwa Masatu alikufa baada ya kugongwa na gari, lakini ile ya madaktari inadaiwa kuonesha kuwa alipigwa na kitu kizito kifuani, kutobolewa na kitu chenye ncha kali chini ya kidevu na kutokeza kwa nyuma na kuharibiwa kwa jicho la kushoto.


  Aidha, baadhi ya mashuhuda walikiri kutotokea tukio lolote la ajali kama ilivyoelezwa na polisi, kwa vile eneo hilo lina shughuli nyingi za kijamii, na hivyo kama ajali ingetokea ingefahamika kwa wengi.


  Maafisa usalama hao, wamegundulika baada ya wanne kati yao, kukutwa katika hoteli kadhaa zilizoko maeneo ya Sinza ambako waandishi wengi wamefikia.


  Hata hivyo, mmoja wa maafisa hao alidiriki kujitambulisha akiomba waandishi wasiogope kuwapa kile wanachokijua kwa madai kuwa mauaji ya Mwangosi yamewaumiza hata wao.


  Mwanausalama huyo katika hali iliyozidi kuwashangaza baadhi ya waandishi waliokuwepo katika eneo hilo, alidai kuwa wanahabari wasifikiri kuwa serikali imefurahishwa na
  tukio hilo, ndiyo maana wanalifanyia kazi suala hilo, hivyo ni vizuri waandishi wa habari watulie na waache kuropoka ovyo.


  Waandishi wa habari zaidi ya 70 kutoka mikoani wamekutana jijini Dar es Salaam chini ya umoja wao wa klabu za waandishi wa habari hapa nchini (UTPC) katika mkutano wao wa nane ambao pamoja na kufanya uchaguzi wa bodi, utatoa tamko zito lililohusu mauaji ya Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi yaliyotokea Septemba 2, mwaka huu Nyololo Mkoa wa Iringa kwa kuuawa na polisi.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  LOL, Mashushushu Sijalisikia hilo JINA toka Enzi za SOKOINE na UHUJUMI UCHUMI... Nakumbuka Dar Mnakwenda Ettien's Hotel

  Wazazi Wanakunywa Bia 2 na Sisi Kuku na Soda Moja na kwenda Nyumbani, kisa Mashushushu Wanatuchunguza eti tukiagiza Sana...

  Wazazi JELA...

  LOL.. POLENI Sana WAANDISHI WA HABARI na HAO MASHUSHUSHU...
   
 3. eumb

  eumb Senior Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haki hupatikna kwa umoja, shikamaneni na kamwe msikubali kurubuniwa, kile mnachofanya sasa kitakumbukwa na vizazi vingi vijavyo. Wapo watako sema mengi kama vile, mnatumiwa na CDM, mmehongwa na makundi ya wanasiasa nk, lakini yote hayo muweke kando maana ukweli upo wazi hasa baada ya mauaji ya kusikitisha ya mpiganaji Daudi Mwangosi.
  All the best!!
   
 4. commited

  commited JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Inasikitisha sana yaaani, haya mashushu yapo kuua raia tu, wezi wa rasilimali zetu na hayo majizi marafiki zake jk yanazidi kutanua tu mitaani na kupora ardhi zetu na kutuzidishia umaskini kila kukicha... Ewe mungu tenda kazi yako dhidi ya mashetani haya.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mashushu walikua zamani bhana,,,sasa hivi kuna waganga njaa
   
 6. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  wameshatumwa ukiwauliza "tupo kwenye mission" kwa maslai ya taifa mhhhhhhhhh
   
 7. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Hapa pazuri! wapigeni picha na record sauti zao hao mashushu tumpelekee Dr. Ulimboka kwa atambulisho wa watekaji wake
   
 8. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Yaani mpaka hapo, kama kweli hao ni mashushushu, basi nahofia kuwa they are ill-trained.
   
 9. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mashushu wanakazi gani nchi hii??wanawajibika kwa nani??kazi yao kurusha vitu vizito/flying objects???????
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Mbaniani mbaya kiatu chake dawa...staili za mwaka 47 zinaendelea kutumiwa na hata watu wa leo?
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mashushushu wa siku hizi hamna kitu! Waisilamu wamejipanga na kuandamana hadi wizarani wao walikuwa wapi. Upuuzi mtupu!
   
 12. A

  August JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  wanacho taka kufanya ni kuharibu ushahidi, na hiui ina maanisha hata uundwaji wa kamati ya uchunguzi ni changa la macho au kwa kuwa kitu kimekuwa wazi saana. mbona tukio la Ulimboka hawakufanya hivi? kwa sababu wana amini bado hakuna ushahidi wa kutosha.
   
 13. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Nawahurumia sana hao mashushushu wanaohangaika kutafuta hard copy. Siku hizi watu wanaweka document zao katika hali soft copy, tena kwa kutumia saver za Yahoo, Google, Facebook, Youtube na nyingine nyingi kama hizo ambazo saver zake zote hizo hazipo hapa nchini. Wao wakusanye tu hizo hard copy lakini watashangaa zinaprintiwa nyingine kama hizo. Sipendi kuamini kuwa wamepitwa na wakati kiasi hiki! Kama ndio hivyo basi tumekwisha, hakuna inteligensia hapa bila Information Technology. Wako kizamani sana.
   
 14. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #14
  Sep 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  moja kati ya fani zinazotumiwa na wanausalama wenye akili duniani ni waandishi wa habari. Usione wanaripoti mambo ya vita au wanatafuta habari, wako kazini wale. Mi nilijua tiss nao wako katika std za kimataifa kumbe wako kizembe zaidi.
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Hao mashushushu nao njaa sana siku hizi wanatumikishwa hata kwenye vitu visivyowezekana!hii karne huwezi kufuta kila kitu,maana ziko online!wanafukuza vivuli vyao!
   
 16. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hizo ni bla bla tu
   
 17. t

  thatha JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  siku hizi hata udaku unawekwa kwenye jukwaa la siasa na wadaku wanaendelea tu kujadili bila kujiuliza kuwa huu udaku umekujaje hapa kwa great thinker
   
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  kwani kazi ya shushu ni kuzuia maandamano???
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  najuta kufungua na kusoma udaku huu
   
 20. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #20
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  Wanapoteza muda bureee, nasikia Kikwete yuko mbioni kuburuzwa The Hague
   
Loading...