Mashujaa wa kweli upande wa ccm tunataka mchango wenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashujaa wa kweli upande wa ccm tunataka mchango wenu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngekewa, Apr 24, 2009.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Natowa wito kwa mashujaa wakweli katika kutetea maslahi ya nchi yetu. Ingawa sina tamaa kuwa wapo mashujaa wa kweli kwa upande huo lakini natowa nafasi kwa hao tunaowaita mashujaa wathibitishe kuwa dhana yangu kuwa hawako watu hao ndani ya chama hicho,si sahihi.Tamaa yangu yote iko kwao katika kuliokowa Taifa hili katika hili jambo linalotunyemelea.
  Hili la harakati za Serikali kuwanyamazisha wale wanaotanabahisha wananchi wapi kuna madudu kwa kisingizio cha kutunza siri za serikali lina lengo la kuturudisha huko nyuma tulikofisadiwa. Nasema nawategemea walioko CCM kwa vile historia imetuonyesha kuwa uwingi wao Bungeni,umiliki wao wa vyombo vya dola, na upeo wa kuvitawala vyombo vya habari una mchango mkubwa katika harakati za kupigana na Ufisadi.
  Ni hiki kipindi cha miaka miwili tu tuliposhuhudia Wabunge kuwa huru na msimamo mmoja wa Chama ndipo Mashujaa wa Upande wa upinzani walipoonekana wanachozungumza pale Bungeni kina maana. Hapo nyuma mashujaa hawa walikuwa wakikebehiwa wakati wakitowa michango yao na hata wengine kuchukuliwa hatuwa za kinidhamu "kwa kusema uongo".
  CCM katika kutaka kujitakasa waliamuwa kuteka nyara vita vya ufisadi pengine kutokana na shinikizo la wakubwa kutoka nje.Katika kufanya hivyo wakastage mashitaka yasio na lengo hasa la kupigana na ufisadi. Katika "VITA" yao hiyo ya kustage walikuwa hawana budi isipokuwa kuzishughulikia zile taarifa zilizokuwa ziko nje tayari. Taarifa hizi ni zile zile zilizofichuliwa na Mashujaa wa Upinzani. "VITA" hiyo ilitumika na Rais wetu kujisafishia jina huko nje, ilitumika kusafisha jina la CCM kuwa inapambana na Ufisadi. Makada mbali mbali wa CCM walijipatia ushujaa kwa kujitia katika "VITA" hivyo.
  Ghafla mambo yameanza kubadilika na vyanzo vya "VITA" hiyo imekuwa ni siri nzito inayotaka kuthibitiwa. Sababu zinazotolewa hazina maana yoyote. Eti zinatia aibu Taifa!! My foot! tuwadhalilishe na kuwafukarisha wananchi lakini isielezwe eti aibu kwa Taifa. Kwani si hao hao tunaowaficha waliotwambia kuwa tunahitaji kusafisha nchi? Eti watu wanatafuta umaarufu wa kisiasa!! Ndiyo kwani hata CCM imekazania katika hilo tofauti ni kuwa CCM inafanya tofauti na wanachokihubiri na hao wengine wanafichua "UOVU" huo na walio wengi wanawaunga mkono kwani angalau aibu inawaumbua watendaji wa maovu hayo.
  CCM mmeshindwa wenyewe kufichua maovu mnayodai yanafanywa na watendaji binafsi mliowapa madaraka, sasa kwa kuwafichia si mtakuwa mnatuonyesha kuwa si watendaji bali ni sera yenu kufanya ufisadi? Rais wetu aliyechini ya mwavuli wenu ameshachoka na ile sifa ya kupambana na ufisadi?. Uzoefu umeonyesha kuwa ufisadi hautolewi hadharani nanyi isipokuwa mnachukuwa hatuwa pale Wapinzani wanapoutowa nje na ili kuchukuwa hatuwa mnahitaji uthibitisho wa maandishi yenye saini zenu.
  Hili la Wabunge wengi wa CCM kujigeuza kasuku na kuwa ndumila kuwili kunavunja moyo. Ikiimbwa nyimbo ya kupinga ufisadi mna chorus na kusema kazi ya CCM na hafla mnakuwa tayari kuwasilibisha walewale walioleta nyimbo hiyo mliyoiteka nyara. Mmetugonganisha wananchi katika kukuteteeni baadhi yenu kuwa ni wapiganaji wa Ufisadi lakini sasa mnaingia mitini mnapoambiwa kutowa michango ya silaha ya mapambano hayo. Mnanyamaza kimya na wengine kwa haraka mnajiunga katika harakati muhimu za kutekeleza vita dhidi ya Ufisadi.
  Na ndio namalizia kwa kusema kuwa TUNATAKA MASHUJAA WA KWELI UPANDE WA CCM KUPINGA HILI LA SERIKALI KUWEKA MIKWARA KWA HARAKATI DHIDI YA UFISADI
   
Loading...