Uswahili na kuficha ficha, mhhhhh..........
Enzi za uwazi hizi. Mbona wengine wanaweka bei zao kwenye EBAY, ALIBABA nk?
Wekeni picha, uwezo na bei na unaweza kuandika kama nyongeza, maelewano yapo. Hii inakuwa kwa wale tuseme wanachukua zaidi ya mbili, basi unampunguzia bei kidogo....... Sasa hii ya kuficha kila kitu hadi uulizwe, inaleta sana utata.....
Wewe piga mahesabu yako kama MCHINA na ukiandika bei basi iwe ni almost bei yako hasa unayotaka kuuza na kupata faida bila kupata HASARA. Mtu akiomba kupunguziwa bei na Mchina, huwa ni kasheshe maana huwa wanaweka bei almost ya wanayotaka kuuza na kifaida kidogo.
Unauza haraka na mzigo ukiisha, basi unarudi tena UK na kuchukua mwingine na si kukaa nao miaka kibao ili muradi uuze kwa faida kubwa sana...... JUST USHAURI. Kila la kheri. Ntawasiliana na kaka yangu ambaye ana mashine kama hizo kama kwa sasa anahitaji. Weka kila kitu wazi ili nikimpigia basi nampa kila kitu..............