Mashine za bakery zinauzwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashine za bakery zinauzwa

Discussion in 'Matangazo madogo' started by TZ biashara, Sep 3, 2012.

 1. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]Nauza mashine za bakery ambazo nilinunua uingereza zilizotumika.Mashine hizi nilinunua kwa ajili ya kuzifanyia kazi lakini sikufanikiwa kufungua kutokana na sababu zisizo zuilika na matokeo yake kupata hasara.Hivo naziuza zote kwa jumla ili kukamilisha bakery nzima na tayari kwa kuanzia kazi.Zinahitaji usafi kiasi na labda servise ili ziwe na uhakika zaidi kwa matumizi.Mashine hizi nimenunua katika hali yakuwa zinafanya kazi kutokana na kufungwa kwa bakery lakini sijawahi kuziwasha kwa muda wa miaka miwili kutokana na kutoelewana mtu ambae alitaka tufanye nae kazi.Na hivo kushindwa kuendelea na ndoto yangu.Tatizo kubwa ni picha sijaweza kuziweka lakini kama hajatokea mtu bado nita lirudisha tangazo hili na pengine nitafanikiwa kuziweka baadhi ya picha kutokana na sehemu zilipo sio rahisi kuzipiga picha.Kusema ukweli ni biashara nzuri sana hasa sehemu za mipakani kama Tunduma Mbeya ambapo ndipo nilikua ndoto yangu kufanyia na ushauri nilioupata kwa wenye uzoefu wa biashara.Mashine nilizonazo ni...

  -OVEN kubwa mbili zenye deki 4 na ni pana zenye kutumika kiwandani

  -MIXER mashine kubwa 2 za kukandia unga ambazo zina ukubwa tofauti na nitaweka vipimo baadae

  -MOULDER mashine moja ya kutengenezea au kukata na kupima kama sikosei scones( Record 30 piece automatic bun divider moulder)

  - MASHINE moja ya kukatia mikate

  -FRENCH BREAD MACHINE moja (kutengeneza mikate mirefu) au Turni Pinner Finger Moulder

  -MOULDER mashine moja ya kutumia mkono ya kuweka mezani

  -PROOVER mashine au kama chumba cha kuumulia unga yenye ukubwa wa fidge au kuizidi kidogo kwa urefu

  -Plastic za kuwekea mikate kama sikosei 20 au 25

  -TREYS za kupikia mikate ambayo idadi yake nimeisahau na nimeshindwa kuingia stoo kutokana na nafasi ndogo

  Hivi vitu vyote thamani yake ni kubwa kuliko bei ninayoiuza kwasababu ya hasara nahitaji milioni 35.Tatizo lingine ni OVEN moja lipo Dodoma na vitu vingine vipo DAR.Naomba kwa mwenye kuhitaji vifaa hivi anitumie ujumbe kupitia PM kutokana na kutokuwepo nchini na baadae nitaweza kumpa contact ya uhakika.


  MAONGEZI YAPO
  Last edited by TZ biashara; 29th August 2012 at 11:32. ​

  Wapo wanaopenda kuona na kusikia lakini wapo wanaojifanya vipofu na viziwi
  [​IMG] [​IMG] Edit Post [​IMG] Reply [​IMG] Reply With Quote [​IMG]

  [HR][/HR]
   
Loading...