Mashine ya kufyatua matofali ya kuchoma

ching'wa

Senior Member
Jan 2, 2015
182
137
Ndugu naomba yeyote anaejua mashine za kufyatua matofali matofali ya udongo Kwa Mfumo wa kisasa anielekeze na bei yake.

Mpaka sasa tofali za udongo za kuchoma ndzo zinatumika sana kwenye ujenzi na Mfumo wa ufyatuaji wake umeendelea Kuwa wa kienyeji sana na kuzifanya kukosa ubora.
 
Ndugu naomba yeyote anaejua mashine za kufyatua matofali matofali ya udongo Kwa Mfumo wa kisasa anielekeze na bei yake.

Mpaka sasa tofali za udongo za kuchoma ndzo zinatumika sana kwenye ujenzi na Mfumo wa ufyatuaji wake umeendelea Kuwa wa kienyeji sana na kuzifanya kukosa ubora.
Labda ukaulizie SIDO
 
Ni jana tu nilikuwa nawaza kuhusu hii mashine baada ya kuhangaika na tofali.

Zipo South Africa mkuu picha imekataa. Zinauzwa Rand 14 000 - 18000.

Ukizipata usisite kushare zilizpo
 
Kuna kubwa zaidi ya hii
Screenshot_2020-12-24-15-43-45-1.jpg
 
Sijawahi kuona ya mafuta wala umeme ila nimeona manual kama hiyo ambazo hata karakana za mitaani tu wanatengeneza.

SIDO lazima watakutengenezea tu.
 
Nikiwa mdogo miaka ya tisini niliona mashine hiyo kwambali PERAMIHO Songea kwenye shirika la Benedictine Father's. Nahisi ilikuwa ya kutengenezwa kwenye karakana za pale. So sikujali wakati huo sasa ndio naihitaji. Kama wapo wenyeji wa PERAMIHO Songea watujuzepia kama bado kile kiwanda kipo ikiwezekana nisafiri kwenda kujifunza. Naihitaji sana kwani ni fursa kubwa na itatoa ajira kubwa Kwa vijana.
 
Ahsante sana Kwa kujali ombi langu. Kwamba hizi zinapatikana SA na ili upate mpaka uagize kutoka huko? Pia naomba kujua Kwa chenji yetu ya bongo ni sawa na shida. NGAPI?
Mkuu chenji huwa inabadilika badili..kuanzia 170 hadi 150.

Kwa makadirio hiyo ni kama milioni 3 na kitu...hadi ikufikie inaweza fika 4 na kitu....
 
Kwa sasa deal kubwa ni matofali mfungamano mashine zake zinauzwa kati 1.5 mill. Hadi 2.

Faida zake.
Zina ujazo stahiki kwa vipimo stahiki.
Zinahamishika ikipita bomoa bomoa
Zahisi kuliko tofali za block 600-700 moja.
Muonekano mzuri wa jengo
Inaruhusu ukuta kupumua
Matumizi kidogo ya cement
Kuhimili kwa kiasi kikubwa matetemeko
Ujenzi wa haraka
Kuhimili uzito paa lolote kwa kuangalia msingi wake kwani zina kaa sawa na block nzito ukiilaza.

Sio mtaalamu nami nilipewa hizi sifa na wahusika na serikali kwa kiasi kikubwa wanahamia huku katika ujenzi hasa madarasa
 

Attachments

  • IMG_20201201_164510.jpg
    IMG_20201201_164510.jpg
    462.4 KB · Views: 90
Ndio tuko kwenye utafiti na mawazo Yako ni Sehemu muhimu ya utafiti.

Ukweli ni kwamba mpaka sasa tofali za kuchoma ndizo Zinatumika Sana kwenye majengo ya wananchi wa kawaida, taasisi na hata serikalini.

Shida kubwa sio ubora bali kiwango chake. Zinafyatuliwa kienyeji na zinachomwa kienyeji Sana. Uzuri wa mashine inazishindilia Kwa kiwango CHA Kutosha na kuzalisha tofali imara, bora na lenye kiwango.

Tofali unazo PENDEKEZA zipo na nzuri japo bado hazijapokelewa kwenye jamii. Zinahitajika uhamasishaji mkubwa. Kimazingira ni toleo rafiki kwani hazihitaji nishati ya moto.

Tushirikishane naamini hata ndani ya nchi yetu hizi mashine zipo hata Kama sio genuine.
FANYA UTAFITI SOUTH AFRICA ZINAATIKANA KWA WINGI NA BEI PIA INARIDHISHA
 
Back
Top Bottom