Mashindano ya Mamiss na njaa za wabongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashindano ya Mamiss na njaa za wabongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mgoyangi, Aug 11, 2009.

 1. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #1
  Aug 11, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Leo Asubuhi nilikuwa naangalia kipindi cha Tuongee nikaona mshiriki mmoja akikandia mashindano ya urembo.

  Kwamba yanawazalilisha wanawake licha ya viongozi na wanaharakati kuyashabikia, lakini pia hayana maana kwa sababu anatafutwa mrembo wa Kitanzania kwa sifa za kizungu.

  Pia kwamba waandaaji wanaganga njaa na kwamba kuna hila katika kutoa zawadi kwani kuna rushwa katika kutafuta mshindi na zawadi zinazotolewa sehemu yake hurudi kwa waratibu.

  Kwamba hicho kinachodaiwa umiss utalii, hakitangazi utalii wa kitanzania kwa sababu hata nywele za washiriki huwa ni yale maplastiki ya kuvaa ili washiriki waonekana kama wazungu. Pia akasema Mwendo wa Nyau -- cat walk -- wapi na wapi kwa wadigo na kuhusu uwezo wa kuzungumza washiriki wanatumia kiswahili chenye rafudhi ya kizungu.

  Kikubwa zaidi ni lile shairi lake ---

  Na hebu waone, wakapite mbele ya kadamnasi,
  wamekondeana kama vi bi Kikagula Mchawi
  Na angalia midobo yao ilivyo miekundu,
  Hii inanikumbusha hadith za alfu lela ulela
  Juu ya Jini Makata mnyonya damu.

  Mshiriki na mratibu wa Miss Utalii Bwana Chipungahelo, alikuwa akipinga haya yote.

  Hivi ni vema kweli kuiga kila kitu? Kisa kimetoka kwa wazungu.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ni bora kuwa na Mis Tz wa mambo yetu ya asili..yaani wowowo kubwa, mguu wa bia .n.k
   
Loading...