Mashindano ya kuchimba makaburi yanavyotikisa Ulaya

Mashindano ya kuchimba makaburi yanavyotikisa Ulaya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
UKISIKIA duniani kuna mambo basi malizia kwa kusema ‘tembea ujionee’. Wakati uchimbaji makaburi ikionekana ni kazi ya ajabu hata ikiwa ngumu kuwashawishi vijana wa kileo kujihusisha nayo wapo walioiona kuwa ni fursa kwa kuianzishia mashindano.

Kazi hiyo imeanza kujizolea umaarufu mkubwa katika mataifa mbalimbali ya Ulaya hasa kwa miaka ya hivi karibuni, kutokana na mashindano mbalimbali ya uchimbaji kaburi yanayofanyika.

Kwa kuanzia, hiyo utaipata huko Trencin nchini Slovakia ambako sasa wananchi wake hawashangai kusikia mashindano ya aina hiyo.

Ieleweke kuwa Slovakia si nchi pekee yenye mashindano hayo, kwani itakumbukwa kuwa hata Hungary nayo na lilipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2016, timu 18 zilishiriki mjini Debrecen.

Ni katika shindano hilo ambalo mshindi wake alikwenda Slovakia, jumla ya timu 18 zilishindana huko Hungary, ambapo kigezo kikubwa cha kaburi sahihi ilikuwa ni lenye upana wa futi 2 na inchi 7, urefu wa futi 6 na inchi 6 na kina cha futi 5 na inchi 3.

B.jpg
Kama ambavyo huwa kwenye mchezo wa tenesi wakati mwingine shindano la Slovakia kila timu huwa na watu wawili ambao kwa pamoja hushirikiana kuhakikisha kaburi linakamilika ndani ya muda mfupi.

Shindano linapoanza, kila timu huwa na mbinu zake za ushindi – kama mmoja atachimba na mwingine kuondoa udongo au watafanya vinginevyo ili mradi kuibuka washindi mbele ya wapinzani wao ambao nao watakuwa kwenye eneo lao.

Ukija kwa Slovakia, moja kati ya masharti ya kila timu ni kuhakikisha hakuna kifaa cha kisasa kilichotumika kuchimba zaidi ya chepe na sururu, tofauti na inavyokuwa Hungary kwani kule vifaa kama shoka huwa vinaruhusiwa, kwa mujibu wa gazeti la Guardian.

Ili kumpata mshindi kwa njia ya halali na kuepuka malalamiko kutoka kwa wenzao, shindano huwa na jopo la majajaji ambao kimsingi nao huwa si wageni kwenye kazi hiyo ya uchimbaji makaburi.

Majaji wanatakiwa kuwa na ujuzi wa kutosha juu ya kaburi bora, kigezo kikubwa ikiwa ni lenye kina cha futi 5, urefu wa futi 6.5 na upana wa futi 3. Hiyo ni kwa mujibu wa vigezo vya kule Slovakia, ambavyo vinatofautiana na ilivyo Hungary.

Mashindano ya Slovakia yanayotajwa kuwa ndiyo makubwa zaidi, hushirikisha timu kutoka nchini humo, pia zingine za Poland, Hungary na Jamhuri ya Czech.

Baada ya kuchimba, si tu majaji humtangaza mshindi, bali vigezo hivyo hufuatatiwa na mmoja kati ya watu waliopo kwenye jopo lao kujaribu kwa kuingia kaburini, kana kwamba mtu aliyefariki.

Aidha, katika shindano hilo ni kawaida kusikia yakiibuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya washiriki, hasa wale walioshindwa kufanya vizuri. Hao mara nyingi hulalamikia sehemu waliyopewa kuchimba, wakisema ilikuwa ngumu kutokana na kuwa na mawe na kokoto.

C.jpg
Ladislav mwenye umri wa miaka 43 na kaka yake Csaba Skladan (41), wamewahi kuibuka kidedea katika mashindano ya Slovakia mwaka 2016, wakitangazwa kuwa ndiyo wachimbaji bora wa makaburi barani Ulaya baada ya kutumia dakika 54 pekee kuchimba lenye vigezo sahihi vilivyotakiwa na majaji.

Baada ya kaburi lao kutajwa kuwa ndilo lenye mvuto zaidi kuliko mengine, Skladan alisema; “Nimefurahi tumeshinda ni jambo zuri kwetu baada ya miaka 15 kwenye kazi hii (ya kuchimba kaburi),”.

Lakini je, nini lengo la ujio wa mashindano hayo barani Ulaya? Ni kwamba kazi zimekwisha kiasi kwamba wamegeukia huko?

Msemaji wa shindano hilo la Slovakia, Christian Striz, anasema; “Lengo ni kujaribu kupunguza huzuni iliyopo kila watu wanapozungumzia msiba, badala yake lionekane ni jambo la kawaida tu kwamba linaweza hata kufanyiwa mzaha.

Striz anaongeza kuwa shabaha ya shindano hilo ni kuipa heshima kazi ya uchimbaji makaburi baada ya kubaini kuwa wanaofanya shughuli hiyo wamekuwa wakidharauliwa.

“Lengo ni kuonesha watu ilivyo kazi ngumu kuchimba kaburi.”

F.jpg
Julie Hillman, mmoja kati ya wanawake wachache nchini Uingereza wanaofanya kazi ya kuchimba makaburi anatilia mkazo kauli ya Striz akisema; “Watu wanafikiri kuwa uchimbaji makaburi ni ajabu lakini haiko hivyo.

Naye Iren Kari aliyeshiriki katika uandaaji wa shindano la Slovakia, aliliambia Shirika la Habari la AP kuwa wanataka kuyafanya mashindano hayo kuwa maarufu zaidi ulimwenguni ili kukabiliana na wale wanaoidharau kazi ya kuchimba makaburi.

Lakini, Kari anahitimisha makala haya kwa kuibua changamoto kubwa inayowakumba katika harakati zao za kuifanya kazi ya kuchimba makaburi kuheshimika kupitia mashindano wanayoandaa.

“Bado kuna changamoto ya kuwapata vijana wanaoweza kuchukua nafasi ya wale wazee wanaokaribia kuachana na kazi hii,” alisema Kari.
 
Ladislav mwenye umri wa miaka 43 na kaka yake Csaba Skladan (41), wamewahi kuibuka kidedea katika mashindano ya Slovakia mwaka 2016, wakitangazwa kuwa ndiyo wachimbaji bora wa makaburi barani Ulaya baada ya kutumia sekunde 54 pekee kuchimba lenye vigezo sahihi vilivyotakiwa na majaji.
________________

Kaburi gani linachimbwa kwa sekunde 54 tu na kukamilika? Ni kaburi tunalolijua au shimo?
 
Hii ngumu kumeza, Hata Medulla Oblongata angu imeshindwa kuiprocess 🙁
 
Ile kauli ya mshan kuwa kaburi halilali mdomowazi hapa haifanyi kazi Mshana Jr ?

Mambo yanabadilika sana zamani watu walikuwa hawakatizi hata makaburini, ila wakati niko primary tulikuwa tunacheza mpira eneo liko makaburini na tunakaa juu ya makaburi yaliyojengewa bila matatizo kabisa na wengine hadi usingizi wanauchapa juu ya kaburi.

Mara nyingi nahisi ni uoga tu wa Mwafrika kuogopa what will never happen.

Ukitaka jua hilo yani na waganga na uchawi wote wa Mnigeria bado mwingereza akamtawala hapo sielewi aisee.
 
Ile kauli ya mshan kuwa kaburi halilali mdomowazi hapa haifanyi kazi Mshana Jr ? Mambo yanabadilika sana zamani watu walikuwa hawakatizi hata makaburini, ila wakati niko primary tulikuwa tunacheza mpira eneo liko makaburini na tunakaa juu ya makaburi yaliyojengewa bila matatizo kabisa na wengine hadi usingizi wanauchapa juu ya kaburi.
Mara nyingi nahisi ni uoga tu wa Mwafrika kuogopa what will never happen.
Ukitaka jua hilo yani na waganga na uchawi wote wa Mnigeria bado mwingereza akamtawala hapo sielewi aisee.
nini kulala, watu wanafanya ngono juu ya kaburi.
 
Yani ina maana alikuwa anapiga koleo 20 kwa sekunde? Hii ni chai ya kiwango cha Masala from India
Jamaa waongo kuchimba kaburi sekunde 59 haiwezekani hata kwa tingatinga.
Hapo unachimba kwa sululu sekunde 39 na kutoa udongo sekunde 20!!
Shughuli yote hiyo chini ya dakika 1?
 
Sekunde 54? Hii ni chai aisee au labda walimanisha dkk54 mleta mada kajaza chumvi
 
sec. 54 huo udongo ama mchanga, huku tunatumia masaa 5 tena tuko zaidi ya 10
 
Ladislav mwenye umri wa miaka 43 na kaka yake Csaba Skladan (41), wamewahi kuibuka kidedea katika mashindano ya Slovakia mwaka 2016, wakitangazwa kuwa ndiyo wachimbaji bora wa makaburi barani Ulaya baada ya kutumia sekunde 54 pekee kuchimba lenye vigezo sahihi vilivyotakiwa na majaji.
________________

Kaburi gani linachimbwa kwa sekunde 54 tu na kukamilika? Ni kaburi tunalolijua au shimo?
Ni dakika sio sekinde mkuu
 
Ameandika dk siyo sekunde
 
Back
Top Bottom