mansoorsaid
JF-Expert Member
- May 31, 2014
- 1,498
- 286
Chama cha mpira wa miguu CACAFA mashindano yake ni sawa na mashindano ya kugombea mbuzi (ndondo) hawana huduma yoyote kwa timu shiriki hawatoi hata jezi viatu nk
Naishangaa TFF inavyoburuzwa na musonye sijamsikia weka hazina, kamati ya mashindano,sijasikia kamati ya maadili sijasikia mahakama ya CACAFA namsilia musonye.nashangaa hata vyombo vya habari hapa nchini havihoji vitu kama hivyo
Naishangaa TFF inavyoburuzwa na musonye sijamsikia weka hazina, kamati ya mashindano,sijasikia kamati ya maadili sijasikia mahakama ya CACAFA namsilia musonye.nashangaa hata vyombo vya habari hapa nchini havihoji vitu kama hivyo
CECAFA wamewakataa Yanga kwa sababu imepeleka timu B, na kwa hivyo kushusha hadhi ya mashindano ya Kagame. Tuwe wa kweli:
1. Mashindano gani yenye hadhi duniani huhusisha mabingwa wa mwaka uliotangulia?
2. Mashindano gani yenye hadhi duniani yanakosa nchi washindani wa kuyaandaa mpaka dakika za mwisho itokee nchi moja ya kuyaokoa?
3. Mashindano gani yenye hadhi duniani yanafunguliwa saa nane mchana wa siku ya kazi kwenye jua kali, sio kwa mechi moja ya ufunguzi bali na mechi ya pili baadaye kwenye uwanja huohuo?
4. Mashindanogani yenye hadhi duniani hushirikisha timu kutoka nje ya zilizoainishwa kwenye kanuni, ili kuyasaidia kuongeza mvuto?
5. Mashindano gani yenye hadhi duniani yanabadlishwa mfumo karibu kila mwaka?
6. Mashindano gani yenye hadhi duniani yanajali zaidi majina ya wachezaji ambao waandaaji wanajua fika hawakushiriki kwenye maandalizi ya timu yao, na kudharau mchanganyiko wa wazoefu wachache wasio maandalizi na vijana wengi walioandaliwa?
7. Mashindano gani yenye hadhi duniani yanashindwa kujipanga ili yasianze baada tu ya mechi za timu FIFA za timu za Taifa?
8. Mashindano gani yenye hadhi duniani yanaendana sambamba na mwanzo wa msimu wa Ligi kwa kalenda ya FIFA?
9. Mashindano gani yenye hadhi duniani hayahakikishi bingwa wake anakabidhiwa fedha zake siku ya fainali?
10. Mashindano gani yenye hadhi duniani hukabidhi fedha zake za washindi 'vichochoroni' kwenye bahasha za kaki, na kuwaacha wachezaji na viongozi wakikwapuana bahasha hiyo?
Mashindano gani yenye hadhi duniani huongeza timu wazipendazo, eti kwa sababu timu hizo zina washabiki wengi?Nionavyo, Yanga wako sahihi kujiandaa na mashindano yenye hadhi zaidi kuliko kun'gan'gana na ambayo waandaaji wake ni miongoni mwa vinara wa ubabaishaji duniani.
Haiwezekani kujiandaa kwa ligi kupitia kwenye ligi. Kisa cha timu za Ulaya kwenda Marekani na Asia kwamaandalizi ya Ligi zao ni kukimbia ligi za upinzani (competitive league/matches). Hata wakicheza Man U na Liverpool, kanuni zake ni za kishikaji zaidi, zinazoruhusu wachezaji wengi zaidi kwa kila timu, ili kupunguza uwezekano wa majeruhi. Ndivyo ilivyo Kagame?
Tutegemee Azam yenye majeruhi kabla ya kuanza ligi, labda kama watatolewa mwanzoni.