Ryan The King
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 2,788
- 2,690
Hellow wanajamvi.
Nina mchumba wangu yupo chuo fulani hapa jiji la Bashite. Kiukweli Mchumba wangu huyu ni mzuri kiasi na ninampenda sana kutokana na moyo wake wa kujitolea. Nipo nae huu ni mwaka wa tatu.
Rafiki zake na huyu mtoto ambao ndio mashemeji zangu wamekuwa wakinitongoza. Hali hii ilifanya Mpenzi wangu kugombana na marafiki zake tokea akiwa kidato cha sita. Kila rafiki akimpata lazima anitongoze. Kutokana na kumheshimu Mchumba wangu sijawahi kumsaliti kwa kutoka na rafiki yake yeyote.
KILICHONIFANYA NIANDIKE:
Mwezi wa pili alipata rafiki yake mmoja ambaye wanasoma Kozi moja lakini Vyuo tofauti hapa hapa Dar.
Siku ya kwanza nilipoongea na Shemeji yangu mpya alinambia kuwa nina sauti yenye kumvutia mwanamke yeyote. Hilo sikushangaa kwani ilikuwa ni kawaida yangu kusikia hivyo kwa wanawake wengi niliopata kuongea nao kupitia Simu. Alinambia anataka akutane na Mimi aweze kuniona. Mimi nikamjibu asijali Shem wake nipo tuu na amwambie Mchumba wangu aje naye.
Shemeji akanizoea sana. Ikafikia hatua anaanza kuntumia picha za uchi kupitia What's app. Nilishtuka siku ile.
Niliona ninapaswa nizuie jambo lile mapema kabla halijakomaa.
Kuna siku nyingine alinipigia Kupitia Video call ya kwenye What's app akiwa anaoga bafuni. Alikuwa kavaa bikini huku maji ya bomba la mvua yakimmwagikia. Niliuona uzuri wake.
Moyoni pia nilikiri kuwa Yeye ni mzuri kupita Mchumba wangu ambaye ni Rafiki yake.
Baada ya kukataa kwa zaidi ya mwezi mmoja kukutana naye, Jana niliruhusu yeye kuja Ghetto. Shemeji alikuja na Mkoba(hand bag) ambapo ndani aliweka nguo. Alipofika alibadili na kwenda kuoga. Mimi nikaingia jikoni kukorofisha. Alitoka bafuni Mimi nikiwa Jikoni. Nilisikia Shem akiongea na simu wakati niko Jiko.
Mazungumzo nilioyasikia;
" (Jina la mchumba wangu) kuanzia Leo uachane na Michaelray, ananipenda na Mimi ninampenda. Umesikia (jina la mchumba Wang)"
Niliingia ndani kumfuata na kukuta ameshika simu yangu akiwa ameshaikata. Nilijua ameshampigia mchumba wangu kupitia simu yang.
Nikiwa namuangalia kwa hasira akiwa na kanga amejilaza kitandani Mara simu yangu ikaita. Kuangalia alikuwa Mchumba wangu. Tuliangaliana kisha nikamnyang'anya simu mikononi mwake na kukuta namba iliyokuwa ikiita kwenye simu yangu ilikuwa ya Mchumba Wang.
Nilibaki nimeishika mpaka ikawa imekatika. Akapiga tena ila sikupokea. Sikujua cha kusema muda ule.
Mara message ikaingia
"Nashukuru kwa yote Michael"
Ilikuwa ni message iliyosomeka kwenye simu ambayo ilipasua moyo Wang. Nilimkamata Shemeji na kumchapa makofi mawili mfululizo.
"Unanipiga kwa sababu nakupenda Michael?"
Shemeji aliongea akiwa ameshika mashavu yake yaliyolegezwa na makofi yangu.
Nikiwa nawaza nimfanye nini Mara bodaboda ikawa imesimama hapo nje ya geti. Punde mlango wa chumbani ukafunguka na Mchumba wangu akaingia akiwa rafu kiasi. Alisimama ukimya ukiwa umetawala kwa nukta kadhaa. Harufu Kali ya kitu kinachoungulia jikoni ndio ikawa ufunguo wa kufungua kufuli la kimya kile.
"Aaa! Nimeunguza"
Niliongea nikiondoka upesi kwenda jikoni. Nilienda kuepua mboga nilizozikuta katika hali mbaya.
Nikiwa jikoni. Nilisikia vishindo vya ngumi vikitoka chumbani. Nilirudi haraka na kuwakuta wanapigana.
Niliwakania.
"Unamtetea Malaya wako"
Mchumba wangu aliongea.
"Usiniite Malaya"
Shemeji alijibu akiwa anajifunga kanga kwani alikuwa kabaki na chupi tuu.
Nilipata wakati mgumu sana. Ilikuwa sio rahisi kumuaminisha Mchumba angu kuamini kuwa sijatoka na rafiki yake.
Swali ambalo nililiogopa ni kuwa;
Shemeji amepajuaje juaje ninapoishi kama sikumuita Mimi?
Swali jingine ni kuwa;
Shemeni atakujaje kwangu bila mchumba wangu kujua?
Nilichokifanya nilimwambia shemeji avae aondoke. Alikataa nilimpiga kofi la kichwa bila dalili ya huruma. Alianza kuvaa akilia huku akiapa kuwa Mimi na mchumba wangu tutaona. Nilotaka kumuongeza Kofi lakini mchumba wangu akaniwahi kunishika.
Shemeji aliondoka nikabaki na mchumba wangu ambaye bado usoni niliona sura ya mbogo aliyejeruhiwa wakati wa ukame. Alikuwa amekasirika mno.
Nilitaka kumueleza akataka kunizaba Kofi. Kwa bahati nikamdaka mkono.
Nikamuuloza unataka kunipiga Kofi?
Akawa amekaa kimya akiwa anahema kwa hasira.
"Ondoka kama hutaki kunisikiliza tusije zua mengine humu ndani"
Niliongea nikimaanisha.
Alitoka na Mimi nikarudisha mlango.
Mpaka Jana inaisha hakuja text wala call kutoka kwake.
Leo asubuhi kanitumia text
"Usinitafute"
Nikamjibu
"Sawa"
Akatuma nyingeni baada ya Masaa mawili.
"Ulikuwa hunipendi Michaelray"
Nikamijibu
"Sawa ila ukihitaji kunisikiliza nikuelezee unaweza kuja"
Akajibu.
"Sitakuja"
Nikamjibu
"Kila la kheri"
Jioni akapiga sijapokea, ametuma text kila kona. Sio What's app, sio Facebook si wapi.
Sijamjibu.
Akanitumia barua moja hivi niliyomuandikiaga akiwa kidato cha sita niliyomuahidi sitomuacha isipokuwa kwa kosa la Usaliti.
Nikampigia nikaongea maneno mafupi
"Ukiwa tayari kunisikiliza tukutane. Kwa sasa bado unahasira. Nakupenda mke wangu"
Mwisho.
My take: wanawake wenye tabia za kutongoza mashemeji zenu na kuharibia rafiki zenu na dada zenu muache