Masheikh wa Lowassa feki

Masheikh wa Lowassa feki

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,337
Masheikh wa Lowassa feki

Waandishi Wetu

Toleo la 398
25 Mar 2015

Edward%20Lowassa_0.jpg

UKWELI kuhusu wanaodaiwa kuwa viongozi wa dini ya Kiislamu waliomtembelea Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, mjini Dodoma wiki iliyopita umebainika.
Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kwamba katika watu wanaokadiriwa kufikia 50 waliomtembelea Lowassa ili kumshawishi achukue fomu ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, waliokuwa na hadhi ya kuitwa masheikh hawafiki hata watatu.

Kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislamu, neno Sheikh humaanisha mtu mzima, muungwana na kiongozi. Kwa mujibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh ni miongoni mwa majina yanayotumika kutofautisha viongozi wa dini hiyo na watu wa kawaida.

Ndiyo sababu hata kiongozi wa Bakwata hufahamika pia kama Sheikh Mkuu wa Tanzania.
Mara baada ya kuibuka kwa habari za Lowassa kufuatwa na ‘Masheikh' hao, Raia Mwema lilifanya uchunguzi na kubaini ukweli kuhusu viongozi hao waliotangazwa katika tukio hilo.
Ziara hiyo inadaiwa kupangwa na Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Kapuya, ambaye anadaiwa kutembelea Bagamoyo kupanga mpango huo wa safari hivi karibuni.
"Mheshimiwa Kapuya alikuja hapa Bagamoyo katika siku za karibuni kwenye tamasha la nyama choma na hapo ndipo alipoanza mipango yake ya kuandaa safari hii ya ‘masheikh'.

Mtu aliyeshirikiana naye kwa karibu kwenye kazi hiyo ni Kassim Mwinyigogo, ambaye ni mmoja wa viongozi wa CCM hapa Bagamoyo na swahiba wa zamani wa Rais Jakaya Kikwete.
"Hao watu waliokwenda Dodoma si viongozi wa Waislamu wa Bagamoyo. Sheikh wa Bagamoyo ni Abdulkadir Ramiya na hakwenda kwenye hilo tukio na wala hakuwa na taarifa ya safari hiyo.
"Ngoja nikuulize swali moja ndugu yangu. Hivi inawezekanaje kwa viongozi 50 wa eneo kama Bagamoyo waondoke na kwenda mbali kama Dodoma pasipo mkubwa wao (Ramiya) kujua? Hapo ndipo waandishi mlipotakiwa kuanza kuuliza maswali," alisema mmoja wa viongozi wa CCM Bagamoyo aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina.

Gazeti hili limeambiwa kwamba wakati watu hao walipokwenda Dodoma, kila mmoja inadaiwa alipewa kiasi cha shilingi 100,000 na wakati wanarudi walipewa kiasi cha shilingi 400,000 walipoondoka Dodoma.
"Walipoondoka Bagamoyo walipewa shilingi laki moja kila mmoja na taarifa zilikuwa kwamba wanakwenda Dar es Salaam. Lakini ghafla wakaambiwa safari ni ya kwenda Dodoma na labda ndiyo sababu waliongezwa na kupewa laki nne," kilidai chanzo hicho.

Mwinyigogo anayetajwa katika taarifa hii ni yule mwanasiasa ambaye aliwahi kuwa kada maarufu wa chama cha NCCR-Mageuzi na akitajwa kuwa mmojawapo wa maswahiba wa kisiasa wa Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema.

Katika picha zilizosambazwa, mmoja wa ‘viongozi' hao alionekana akimkabidhi Lowassa kiasi cha shilingi 700,000 ukiwa ni mchango wao wa kumsaidia aingie katika kinyang'anyiro hicho.
Hata hivyo, Raia Mwema limeambiwa kwamba aliyemkabidhi Lowassa kiasi hicho cha fedha, Yusuf Surulu, aliwahi kuwa kiongozi wa Bakwata Bagamoyo lakini aliondolewa katika wadhifa huo miaka minne iliyopita kwa sababu ambazo gazeti hili haliwezi kuziweka wazi kwa sasa.

Pia, katika picha ambayo Lowassa anaonekana akipokea fedha hizo, huku akiwa na Kapuya; zaidi ya Surulu pia yuko mzee mwingine, Ally Mtumwa, ambaye naye imeelezwa si kiongozi wa Waislamu.
"Huyu Mzee Mtumwa zamani alikuwa miongoni mwa watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha hapa Bagamoyo. Lakini katika miaka ya karibuni amekuwa na hali mbaya kifedha na inawezekana sababu za kifedha ndizo zilizosababisha afunge safari hiyo.

"Ukizungumza na watu wa Lowassa wanasema anachofanya yeye ndicho alichofanya Kikwete wakati akiwania urais mwaka 2015. Lakini, basi atumie maarifa kidogo. Mwenzake alikuwa akiwasiliana kwanza na maofisa usalama wa wilaya au mikoa kujua kama anakutana na watu sahihi.

"Sasa huyu bwana aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na ni lazima anajuana na maofisa usalama hawa ambao wako wengi tu. Anakubalije kuingizwa mkenge kiasi hiki? Mbona masheikh wa Bagamoyo wanafahamika? Hivi siku hizi ushehe ni kuvaa kanzu, koti na baraghashia?" alihoji mmoja wa masheikh maarufu wa Bagamoyo aliyezungumza na gazeti hili Jumatatu, wiki hii.

Duru za kiuchunguzi za gazeti hili zimebaini katika msafara ule uliokwenda kwa Lowassa, wako watendaji wa Bakwata Bagamoyo waliokwenda lakini walifanya hivyo kwa siri na si masheikh kwa sababu yoyote ile.

Wakati akizungumza nao, Lowassa aliwaambia; "Nyie ni maalumu, mnatoka Bagamoyo na inajulikana kwa historia na ni nyumbani kwa Rais Kikwete. Na mimi nimepata baraka zake na nyie mmemuwakilisha," alisema Lowassa.

"Niseme kwamba ujumbe umefika, mkikutana naye msikitini pelekeni salamu kwa mheshimiwa Rais. Mwambieni mlikuja Dodoma. Mimi nimesema nitaendeleza pale alipomalizia kama Mwenyezi Mungu atanijalia," alisema.
Mara baada ya kutembelewa na kundi hilo la Bagamoyo, siku iliyofuata Lowassa alitembelewa na kundi lingine la watu wanaodaiwa kuwa wanafunzi kutoka katika Vyuo Vikuu vitatu mkoani Dodoma.

Jumatatu wiki hii, Lowassa alitembelewa na watu wanaodaiwa kuwa viongozi wa makanisa ya Pentekoste hapa nchini; ingawa taarifa nyingine zinadai kuwa ni wafuasi wa Askofu Josephat Gwajima ambaye anatajwa kuwa mfuasi wa Lowassa. Lowassa alishiriki kuzindua helikopta ya Gwajima miezi kadhaa iliyopita.
Wakati gazeti hili likienda mitamboni, kulikuwa na taarifa kwamba kundi lililokuwa linafuata katika ‘ratiba' iliyopangwa ni Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Bagamoyo. Eneo hilo la Mkoa wa Pwani linatajwa kuwekwa kimkakati kwa vile mpango unatajwa kuwa kuwaaminisha Watanzania kwamba Lowassa anaungwa mkono na Kikwete.

Akizungumza juzi Jumatatu, Lowassa alikana madai ya yeye kutumia fedha kuwahonga watu wanaokwenda nyumbani kwake kumshawishi, akidai kwamba hana uwezo huo kifedha.
"Ninyi mmekuja huku kwa sababu ya mapenzi yenu kwa Mungu wenu na taifa lenu. Wanaodai kwamba mimi ninawapa watu hela ili waje wanaeneza upuuzi tu," alisema mbunge huyo wa Monduli.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Sheikh Ramiya alizungumza na waandishi wa habari mjini Bagamoyo na kuwaambia kwamba hawatambui viongozi hao waliokwenda Dodoma kwa vile si viongozi wa Waislamu kama ilivyodaiwa na kambi ya Lowassa.
Hatua hiyo ya Lowassa tayari imeanza kuibua maswali miongoni mwa wana CCM ambapo tayari Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, amehoji kuhusu ukweli wa ziara hizo za kumuomba mwanasiasa huyo agombee.

Katika toleo lake la juzi Jumatatu, gazeti dada la hili, Raia Tanzania lilimnukuu Makamba akisema; "Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba ugombee ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa".

http://www.raiamwema.co.tz/masheikh-wa-lowassa-feki

CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, Ablessed, Michelle, Ntuzu, KikulachoChako, kill 3, Daudi Mchambuzi, everlenk, MziziMkavu, Ablessed, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Shark, mirisho pm, Camp 05, Ngoami, Kamakabuzi, jerrytz

Hata huyo muheshimiwa simuamini sana...anaonekana ni muigizaji mzuri sana
 
Attachments

  • 1427417334598.jpg
    1427417334598.jpg
    38.4 KB · Views: 754

Raia Mwema - Masheikh wa Lowassa feki

CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, Ablessed, Michelle, Ntuzu, KikulachoChako, kill 3, Daudi Mchambuzi, everlenk, MziziMkavu, Ablessed, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Shark, mirisho pm, Camp 05, Ngoami, Kamakabuzi, jerrytz

10429468_659292887510762_7377129408655324307_n.jpg
 
Haa haa kumbe jk alitumia mbinu hii ya lowasa! Duh ndo maana teuzi zinafanyika kila siku ikulu kwa marafiki na ndugu! Watanzania tuamke ndani ya ccm hakuna jipya!
 
Kuelekea kwenye uchaguzi mkuu....waTANGANYIKA tutashuhudia vioja vingi sana....vingine vya kushangaza na vingine ni vya kustaajabisha....lakini lengo likiwa ni moja tu....kuupigania ufalme...kuna baadhi ya viongozi wanaowania huo ufalme wanatupa mashaka na wasi wasi kutokana na haraka na pupa zao kuelekea kwenye kiti cha Enzi.....tunatakiwa tutumie fikra zetu kujua kuwa kwanini...wana haraka sana..?? Hiyo haraka inatokana na nini...?? Je ni huruma walionayo juu ya matatizo yetu ndio inayowafanya kuwa na haraka sana kuelekea kwenye kiti cha Enzi......na kwanini huruma hiyo hiyo iwe katika kipindi hichi na sio kipindi kingine....?? Wengi wao si wageni katika uongozi, wamewahi kushika nyadhifa mbali mbali hapa nchini....je uongozi wao ulikuwa na tija gani kwetu kama wananchi...?? Kwanini leo waonekane kuguswa sana na matatizo yetu ambayo wanayafahamu tangu miaka mitano iliyopita na mengine wameyaongeza wao wenyewe.....??.....Ndugu zangu WATANZANIA ,walala hoi wenzangu , wakina baba kabwela wenzangu, wakina pangu pakavu wenzangu, hichi ni kipindi ambacho tunapaswa kutumia akili zetu na ufahamu wetu bara bara....mateso tuliyopitia kwa kipindi cha miaka mitano kama vile ,huduma duni za afya, miundo mbinu mibovu, kutokuwa na umeme wa uhakika hivyo kusababisha shughuli nyingi za kimaendeleo kusimama mara kwa mara....., usimamizi mbovu wa rasilimali zetu unaopelekea tuzidi kuwa mafukara na kugeuka kuwa omba omba ndani ya nchi yetu wenyewe huku tukishuhudia wageni wakineemeka vilivyo kutokana ukiritimba unaofanywa na viongozi wetu, huduma duni za ulinzi na usalama wa raia na mali zake na kukithiri kwa rushwa kwenye idara hiyo nyeti hali inayofanya kupatikana kwa haki kwa sisi wanyonge kuwa ni kitendawili.....wizi unaofanywa kwa wazi wazi wa kodi zetu......hapa naongelea mambp ya ESCROW na mambo mengine yanayolifanya taifa lichechemee.......Mateso hayo yatupelekee sisi kufanya maamuzi ya busara siku ya uchaguzi hapo oktoba.......uamuzi ni wetu kuamua yale mateso na mahangaiko yajirudie kwa kuwachagua wale wale waliotusababishia matatizo hayo...au kuwachana nao na kuwaweka wengine..wanaoonyesha kuguswa na matatizo yetu......tukumbuke kuwa kosa tutakalolifanya kipindi hiki...litatughalimu miaka mitano ijayo......AMKA MTANZANIA,..........
 
Ni wapi ambapo hao mashehe walisema wao ni viongozi wa waislam Bagamoyo au wanawakilisha BAKWATA?

Wanadaiwa katika watu 50, mashehe wa ukweli walikuwa watatu tu, kwani wao walisema walikuwa mashehe mia mbili?
 
Ndio maana wakifika huko sinema inaendelea. Waigizaji sisi na watazamaji sisi, hata sinema ikiwa mbaya hakuna wa kusema ni mbaya wote tumeamua kuwa waigizaji. Tunashusha hadhi na viwango vya viongozi sisi wenyewe ndio maana tunaishia kupata makapi.

Ninaimagine ni nguvu na muda kiasi gani umetumika kuaandaa haya maigizo, watu tumekosa mambo muhimu ya kufanya, tumefikia hatua ya kujisanii wenyewe?

Wacha sinema iendelee.. Hata wale wachungaji watakuwa mamluki tu. Hili zee sijui linataka likafanye nini ikulu
 
Na sisi huku mpakani tunaaubiri zamu yetu ili tupate mapema mgao wetu. Tutakuwa kundi la wana CCM kutoka mikoa ya pembezoni.
 
Rais wa awamu ya tano ni Dr. Slaa, wengine wote wanahangaika bure tu!
Kila moyo wa mpenda haki na mabadiliko nchini lazima awaze hivyo.....wakati mwingine huwa najiuliza kuwa wananchi huwa wanatumia kiungo gani cha mwili kuchanganua mambo na hatimaye kuhalalisha kuendelea kuwaweka CCM kwa kipindi cha miaka yote ya mateso na adhabu........maana kwa kutumia tu fikra za kawaida huwezi kuona uhalali wa hawa jamaa kuendelea kuongoza taifa hili kwa madudu waliyoyafanya katika kipindi chote cha uongozi wao.........
 
Na sisi huku mpakani tunaaubiri zamu yetu ili tupate mapema mgao wetu. Tutakuwa kundi la wana CCM kutoka mikoa ya pembezoni.
Serikali sikivu itasikia kilio chenu....vuta subira mkuu...zamu yenu yaja.........
 
Majukumu ya wananchi ninavyofikiri mimi katika uchaguzi ngazi yoyote ile ni kusikiliza sera za alietangaza nia akiwa anajiamini na kupiga kura. Sidhani kama wwnanchi wanatakiwa kushawishi mtu kugombea nafasi ya uongozi tena kwa mbwembwe kiasi hiki. Haijalishi nani alienda na alitoka wapi, hiyo sio kazi ya wananchi.

Ni wapi ambapo hao mashehe walisema wao ni viongozi wa waislam Bagamoyo au wanawakilisha BAKWATA?

Wanadaiwa katika watu 50, mashehe wa ukweli walikuwa watatu tu, kwani wao walisema walikuwa mashehe mia mbili?
 
labda tungejiuliza tangu lini BAKWATA ambayo ni NGO kama NGO zingine za kidini ikawa na mandate ya kuwa mzungumzaji wa waislam wote?

TEAM MEMBE jipangeni upya. BAKWATA inawakilisha viongozi wao na si waslam wote tanzania au bagamoyo
 
Kila moyo wa mpenda haki na mabadiliko nchini lazima awaze hivyo.....wakati mwingine huwa najiuliza kuwa wananchi huwa wanatumia kiungo gani cha mwili kuchanganua mambo na hatimaye kuhalalisha kuendelea kuwaweka CCM kwa kipindi cha miaka yote ya mateso na adhabu........maana kwa kutumia tu fikra za kawaida huwezi kuona uhalali wa hawa jamaa kuendelea kuongoza taifa hili kwa madudu waliyoyafanya katika kipindi chote cha uongozi wao.........

Hata yeye lazima aje na sera. It is not given eti kwa kuwa ametokea chama pinzani basi tutamchagua. Eti kwa kuwa tumeichoka CCM basi yeyote yule tutamchagua.

Nimechoka na siasa za vyama. Ni wakati Watanzania kuchagua mtu kutokana na sera zake na historia ya utendaji wake katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwezekana kufuatiliwa hata shule ya msingi kama aliwahi kuwa 'class monitor' na alikuwaje.

#tubadilikeWatanzania ...
 
Masheikh wa Lowassa feki

Waandishi Wetu

Toleo la 398
25 Mar 2015

Edward%20Lowassa_0.jpg

UKWELI kuhusu wanaodaiwa kuwa viongozi wa dini ya Kiislamu waliomtembelea Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, mjini Dodoma wiki iliyopita umebainika.
Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kwamba katika watu wanaokadiriwa kufikia 50 waliomtembelea Lowassa ili kumshawishi achukue fomu ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, waliokuwa na hadhi ya kuitwa masheikh hawafiki hata watatu.

Kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislamu, neno Sheikh humaanisha mtu mzima, muungwana na kiongozi. Kwa mujibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh ni miongoni mwa majina yanayotumika kutofautisha viongozi wa dini hiyo na watu wa kawaida.

Ndiyo sababu hata kiongozi wa Bakwata hufahamika pia kama Sheikh Mkuu wa Tanzania.
Mara baada ya kuibuka kwa habari za Lowassa kufuatwa na ‘Masheikh’ hao, Raia Mwema lilifanya uchunguzi na kubaini ukweli kuhusu viongozi hao waliotangazwa katika tukio hilo.
Ziara hiyo inadaiwa kupangwa na Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Kapuya, ambaye anadaiwa kutembelea Bagamoyo kupanga mpango huo wa safari hivi karibuni.
“Mheshimiwa Kapuya alikuja hapa Bagamoyo katika siku za karibuni kwenye tamasha la nyama choma na hapo ndipo alipoanza mipango yake ya kuandaa safari hii ya ‘masheikh’.

Mtu aliyeshirikiana naye kwa karibu kwenye kazi hiyo ni Kassim Mwinyigogo, ambaye ni mmoja wa viongozi wa CCM hapa Bagamoyo na swahiba wa zamani wa Rais Jakaya Kikwete.
“Hao watu waliokwenda Dodoma si viongozi wa Waislamu wa Bagamoyo. Sheikh wa Bagamoyo ni Abdulkadir Ramiya na hakwenda kwenye hilo tukio na wala hakuwa na taarifa ya safari hiyo.
“Ngoja nikuulize swali moja ndugu yangu. Hivi inawezekanaje kwa viongozi 50 wa eneo kama Bagamoyo waondoke na kwenda mbali kama Dodoma pasipo mkubwa wao (Ramiya) kujua? Hapo ndipo waandishi mlipotakiwa kuanza kuuliza maswali,” alisema mmoja wa viongozi wa CCM Bagamoyo aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina.

Gazeti hili limeambiwa kwamba wakati watu hao walipokwenda Dodoma, kila mmoja inadaiwa alipewa kiasi cha shilingi 100,000 na wakati wanarudi walipewa kiasi cha shilingi 400,000 walipoondoka Dodoma.
“Walipoondoka Bagamoyo walipewa shilingi laki moja kila mmoja na taarifa zilikuwa kwamba wanakwenda Dar es Salaam. Lakini ghafla wakaambiwa safari ni ya kwenda Dodoma na labda ndiyo sababu waliongezwa na kupewa laki nne,” kilidai chanzo hicho.

Mwinyigogo anayetajwa katika taarifa hii ni yule mwanasiasa ambaye aliwahi kuwa kada maarufu wa chama cha NCCR-Mageuzi na akitajwa kuwa mmojawapo wa maswahiba wa kisiasa wa Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema.

Katika picha zilizosambazwa, mmoja wa ‘viongozi’ hao alionekana akimkabidhi Lowassa kiasi cha shilingi 700,000 ukiwa ni mchango wao wa kumsaidia aingie katika kinyang’anyiro hicho.
Hata hivyo, Raia Mwema limeambiwa kwamba aliyemkabidhi Lowassa kiasi hicho cha fedha, Yusuf Surulu, aliwahi kuwa kiongozi wa Bakwata Bagamoyo lakini aliondolewa katika wadhifa huo miaka minne iliyopita kwa sababu ambazo gazeti hili haliwezi kuziweka wazi kwa sasa.

Pia, katika picha ambayo Lowassa anaonekana akipokea fedha hizo, huku akiwa na Kapuya; zaidi ya Surulu pia yuko mzee mwingine, Ally Mtumwa, ambaye naye imeelezwa si kiongozi wa Waislamu.
“Huyu Mzee Mtumwa zamani alikuwa miongoni mwa watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha hapa Bagamoyo. Lakini katika miaka ya karibuni amekuwa na hali mbaya kifedha na inawezekana sababu za kifedha ndizo zilizosababisha afunge safari hiyo.

“Ukizungumza na watu wa Lowassa wanasema anachofanya yeye ndicho alichofanya Kikwete wakati akiwania urais mwaka 2015. Lakini, basi atumie maarifa kidogo. Mwenzake alikuwa akiwasiliana kwanza na maofisa usalama wa wilaya au mikoa kujua kama anakutana na watu sahihi.

“Sasa huyu bwana aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na ni lazima anajuana na maofisa usalama hawa ambao wako wengi tu. Anakubalije kuingizwa mkenge kiasi hiki? Mbona masheikh wa Bagamoyo wanafahamika? Hivi siku hizi ushehe ni kuvaa kanzu, koti na baraghashia?” alihoji mmoja wa masheikh maarufu wa Bagamoyo aliyezungumza na gazeti hili Jumatatu, wiki hii.

Duru za kiuchunguzi za gazeti hili zimebaini katika msafara ule uliokwenda kwa Lowassa, wako watendaji wa Bakwata Bagamoyo waliokwenda lakini walifanya hivyo kwa siri na si masheikh kwa sababu yoyote ile.

Wakati akizungumza nao, Lowassa aliwaambia; “Nyie ni maalumu, mnatoka Bagamoyo na inajulikana kwa historia na ni nyumbani kwa Rais Kikwete. Na mimi nimepata baraka zake na nyie mmemuwakilisha,” alisema Lowassa.

“Niseme kwamba ujumbe umefika, mkikutana naye msikitini pelekeni salamu kwa mheshimiwa Rais. Mwambieni mlikuja Dodoma. Mimi nimesema nitaendeleza pale alipomalizia kama Mwenyezi Mungu atanijalia,” alisema.
Mara baada ya kutembelewa na kundi hilo la Bagamoyo, siku iliyofuata Lowassa alitembelewa na kundi lingine la watu wanaodaiwa kuwa wanafunzi kutoka katika Vyuo Vikuu vitatu mkoani Dodoma.

Jumatatu wiki hii, Lowassa alitembelewa na watu wanaodaiwa kuwa viongozi wa makanisa ya Pentekoste hapa nchini; ingawa taarifa nyingine zinadai kuwa ni wafuasi wa Askofu Josephat Gwajima ambaye anatajwa kuwa mfuasi wa Lowassa. Lowassa alishiriki kuzindua helikopta ya Gwajima miezi kadhaa iliyopita.
Wakati gazeti hili likienda mitamboni, kulikuwa na taarifa kwamba kundi lililokuwa linafuata katika ‘ratiba’ iliyopangwa ni Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Bagamoyo. Eneo hilo la Mkoa wa Pwani linatajwa kuwekwa kimkakati kwa vile mpango unatajwa kuwa kuwaaminisha Watanzania kwamba Lowassa anaungwa mkono na Kikwete.

Akizungumza juzi Jumatatu, Lowassa alikana madai ya yeye kutumia fedha kuwahonga watu wanaokwenda nyumbani kwake kumshawishi, akidai kwamba hana uwezo huo kifedha.
“Ninyi mmekuja huku kwa sababu ya mapenzi yenu kwa Mungu wenu na taifa lenu. Wanaodai kwamba mimi ninawapa watu hela ili waje wanaeneza upuuzi tu,” alisema mbunge huyo wa Monduli.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Sheikh Ramiya alizungumza na waandishi wa habari mjini Bagamoyo na kuwaambia kwamba hawatambui viongozi hao waliokwenda Dodoma kwa vile si viongozi wa Waislamu kama ilivyodaiwa na kambi ya Lowassa.
Hatua hiyo ya Lowassa tayari imeanza kuibua maswali miongoni mwa wana CCM ambapo tayari Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, amehoji kuhusu ukweli wa ziara hizo za kumuomba mwanasiasa huyo agombee.

Katika toleo lake la juzi Jumatatu, gazeti dada la hili, Raia Tanzania lilimnukuu Makamba akisema; “Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba ugombee ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa”.

http://www.raiamwema.co.tz/masheikh-wa-lowassa-feki

CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, Ablessed, Michelle, Ntuzu, KikulachoChako, kill 3, Daudi Mchambuzi, everlenk, MziziMkavu, Ablessed, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Shark, mirisho pm, Camp 05, Ngoami, Kamakabuzi, jerrytz

Pasco Njoo umjibie mamvi na hili pia.
 
Last edited by a moderator:
Hata yeye lazima aje na sera. It is not given eti kwa kuwa ametokea chama pinzani basi tutamchagua. Eti kwa kuwa tumeichoka CCM basi yeyote yule tutamchagua.

Nimechoka na siasa za vyama. Ni wakati Watanzania kuchagua mtu kutokana na sera zake na historia ya utendaji wake katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwezekana kufuatiliwa hata shule ya msingi kama aliwahi kuwa 'class monitor' na alikuwaje.

#tubadilikeWatanzania ...
Amini maneno yangu..kama ilivyokuwa ngumu kutambua rangi halisi ya kinyonga....ndivyo ilivyokuwa kwa kuwatenganisha wana CCM na ufisadi kwani kwao ni tukio lenye heshima.........by the way.....akili kumkichwa...........
 
Waandishi Wetu
Wakati akizungumza nao, Lowassa aliwaambia; "Nyie ni maalumu, mnatoka Bagamoyo na inajulikana kwa historia na ni nyumbani kwa Rais Kikwete. Na mimi nimepata baraka zake na nyie mmemuwakilisha," alisema Lowassa.

"
Niseme kwamba ujumbe umefika, mkikutana naye msikitini pelekeni salamu kwa mheshimiwa Rais. Mwambieni mlikuja Dodoma. Mimi nimesema nitaendeleza pale
alipomalizia kama Mwenyezi Mungu atanijalia," alisema.
Mara baada ya kutembelewa na kundi hilo la Bagamoyo, siku iliyofuata Lowassa alitembelewa na kundi lingine la watu wanaodaiwa kuwa wanafunzi kutoka katika Vyuo Vikuu vitatu mkoani Dodoma.
Team Lowassa na suala la Membe kutumia jina la Rais Kikwete na familia yake katika harakati zake za kusaka Urais!
 
Back
Top Bottom