Mashaurini huyu Mwanamke

Mashaurini huyu Mwanamke

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,701
Habarini wanajamvi,

mimi ni Msichana umri miaka 25. Nimekuwa katika Mahusiano kwa miaka 7 na Jamaa ambaye ana umri wa miaka 32 kwa sasa. Nampenda sana ila katika kipindi chote cha mahusiano yetu amekuwa akinisaliti mno na wasichana tofauti ambapo nimekuwa nikigundua mara kwa mara na kumsamehe.

Mwaka 2017 alianza kunisaliti na Msichana fulani hivi, ambapo nilifanikiwa kupekua katika simu ya mpenzi wangu na kuchukua mawasiliano ya huyo Msichana. Pia, niliingia katika akaunti ya Facebook ya mpenzi wangu na kumblock kabisa yule msichana kwani walikuwa marafiki fb. Niliwasiliana na huyo Msichana tukakubaliana kuonana tuongee.

Baada ya kuonana na kumueleza kuwa anatembea na jamaa yangu nilifikiri labda atakasirika, kinyume chake alikuwa mpole na kunieleza kuwa atakaa nae mbali kuanzia muda ule nimsamehe kwani hakujua kuwa jamaa anaye Mpenzi kwani alimueleza hakuwa na mtu mwingine zaidi yake. Lakini baada ya miezi michache nikawaona kuwa ni marafiki tena facebook. Sikujihangaisha kumuuliza.

Lakini kinachoniuma zaidi nimegundua kuwa, huyo msichana anayo Mimba ya Boyfriend wangu na kumbe wamekuwa pamoja kwa mwaka wote wa 2018 bila mimi kujua. Baada ya kugundua hayo, nilimtafuta yuke msichana na kumtukana mno lakini hakunijibu chochote na kila nilipompigia hakupokea simu.

Mimi Jamani nampenda mno huyu mwanaume, nimekua nikijitoa kwake kwa kila kitu. Nimetoa mimba zake mara kibao kwa kunilazimisha ila nashangaa huyo mwanamke wake wamekubaliana kutokutoa mimba yake.

Nimekuwa nikilia kila siku, sijui hata nifanye nini nipone haya majeraha. Bado nampenda sana. Naomba ushauri wenu.
FB_IMG_1557635558886.jpeg
 
Hapo hamna ushauri,afungue tuu macho poa.
Ajue tuu kua hapendwi,ajiandae kisaikolojia kua hapo hamna mtu.
Ukijiona mwanamke unatumia nguvu sana kwa mwanamke mwenzio to keep your man,jua tuu uko mwenyewe bob.
 
Umeuwa watoto wangapi wasiokuwa na hatia?ukijua kwa nini ulikuwa unakubali kutoa mimba na kwa nini nwenzio hatoi,basi nadhani utapata jibu kuwa wewe ni kifaa cha starehe na mwenzio ana sifa za kuwa mke
 
We nawe una matukio siku hizi🙆🙆🙆
Kwa siku thread rundo!!!
 
Hapo hamna ushauri,afungue tuu macho poa.
Ajue tuu kua hapendwi,ajiandae kisaikolojia kua hapo hamna mtu.
Ukijiona mwanamke unatumia nguvu sana kwa mwanamke mwenzio to keep your man,jua tuu uko mwenyewe bob.
 
Back
Top Bottom