Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,758
- 730,005
Masharti ya waganga feki wa kienyeji mengi hayatekelezeki na baadhi yanadhalilisha.
Tiba mbadala ni ya kienyeji ni tiba yenye wateja wengi sana kwakuwa kuna baadhi ya magonjwa na matatizo hayana tiba kizungu.
Kwa njia hii limezuka kundi la matapeli ambao hawana chembe ya ujuzi wa haya mambo lakini kwakuwa wanataka kutengeneza pesa wamekuwa wakijifanya waganga mahiri wa kutibu magonjwa mengi kwa wakati mmoja kitu ambacho kama Ingekuwa ni kweli basi wangekuwa ni zaidi ya maprofesa.
Lakini kitu kingine kibaya sana wamekuwa wadhalilishaji wakubwa, wahanga wakiwa ni akina mama na dada zetu na wamekuwa pia chanzo cha kueneza magonjwa ya zinaa hata ukimwi.
Masharti ya kuambiwa dawa inawekwa sehemu za siri tena na uume wa mganga huu ni utapeli wa Wazi kabisa .
Masharti ya kuambiwa peleka machozi ya simba au jasho la kuku mwenye madoadoa ni vitu visivyowezekana aslani au kuambiwa ukalete maji yaliyooshea maiti ni kutafuta kipigo hata kifo toka kwa wafiwa .
Matangazo yao mengi utayakuta kila kona ya miji na makazi yao mara nyingi ni kwenye gesti za bei poa na matatizo wanayoyapigia debe kuwa wanatibu ni nguvu za kiume, mvuto utajiri na mambo ya mapenzi
Kwahiyo ndugu zangu kama una imani na hizi tiba epuka sana sana kuingizwa chaka unapohitaji hizi huduma usije utaishia kutapeliwa au mikononi mwa vyombo vya dola
Angalizo : @mshana jr sio mganga wa kienyeji

Last edited by a moderator: