Mbona shule na vyuo hupata kwa 50400?Toto ni aidha umlipie mtoto 120,000 shuleni au Aunganishwe kwenye kifurushi cha kuanzia laki 504000 cha baba mama na mtoto.
Naona utaratibu umebadilika
Wakati nasoma tulikuwa tunalipa laki chuo kwa ambao wazazi sio waajiriwa. Wenye wazazi waajiriwa walikuwa wanalipa hio 50400.
Nililipa laki halafu sijawahi kuuguaWakati nasoma tulikuwa tunalipa laki chuo kwa ambao wazazi sio waajiriwa. Wenye wazazi waajiriwa walikuwa wanalipa hio 50400.
Source?Mfuko huo sasa una utaratibu mpya ulioanza jana Machi 13, kundi hilo linalazimika kulipiwa malipo yao kupitia uanachama wa wazazi au walezi wao ambao ni wanachama kupitia vifurushi vya mfuko kulingana na ukubwa wa familia.
Vifurushi hivyo ni vilivyopewa majina ya Najali Afya, Timiza Afya na Wekeza Afya.
Januari mwaka huu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, alisema atasimama kidete kuhakikisha kila Mtanzania anafahamu umuhimu wa kuwekeza na kuweka kipaumbele kwenye afya na hakutakuwa na msamaha wowote.
Waziri Ummy alisema ajenda kuu iliyopo mbele ya sekta hiyo ni huduma bora na Bima ya Afya kwa Wote, ambayo kwa sasa kiwango kinachotazamiwa ni kuwa kati ya Sh. 340,000 hadi 360,000 kwa mwaka, ili kuhudumia watu sita kwa huduma za rufani, kanda na kibingwa.
UTARATIBU MPYA
Meneja Uhusiano wa NHIF, Angela Mziray, jana aliiambia Nipashe iliyotaka kufahamu utaratibu mpya kuhusu huduma hizo, kwamba utaratibu huo ulianza rasmi jana na bei za vifurushi kulingana na familia wachangiaji kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35, ni kuanzia Sh. 192,000 kwa huduma za kifurushi cha Najali Afya; Sh. 384,000 (Wekeza Afya) na Sh. 516,000 kwa Timiza Afya.
Aidha, kifurushi kama hicho yaani mtu mmoja, bila wategemezi, kwa wachangiaji kuanzia umri wa miaka 35 hadi 59 gharama ni Sh. 240,000 kwa huduma za kifurushi cha Najali Afya; Sh. 444,000 (Wekeza Afya) na Sh. 612,000 kwa Timiza Afya.
Kadhalika, vifurushi kwa ajili ya wanandoa pamoja na mtoto mmoja kwa wachangiaji kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35, ni Sh. 504,000 kwa kifurushi cha Najali Afya; Sh. 924,000 (Wekeza Afya) na Sh. 1,272,000 kwa kifurushi cha Timiza Afya.
Pia kifurushi kwa ajili ya wachangiaji kuanzia umri wa miaka 36 hadi 59 wakijumuishwa watoto wawili, gharama ni Sh. 696,000 (Najali Afya); Sh. 1,248,000 (Wekeza Afya); Sh. 1,728,000 (Timiza Afya) kwa mwaka.
Zaeni Ndugu ZanguHapo uzazi wa mpango hakwambii mtu mwenyewe utajiongeza,shule za vidumu michango kkbao ukienda private school fees juu ukija kwenye afya hakuna tena utelezi wa 50400,lazima ujiunge safe plan lah unataka watoto wengi utakunywa sana miarovela na miarobaini
Mshukuru Mungu kwa kuto kuugua. Pia tuna kupa Asante maana hela yako ilisaidia watu wengine walio ugua kipindi hicho kupata matibabu, hiyo ndio faida ya BimaNililipa laki halafu sijawahi kuugua
Kumbe research kimefanyika basi itumike katika kufanya maamuzi kulingana na kipato halisi cha mwananchi
Ippmedia.com tarehe 14Source?
Kwa upande wa mtumishi usijaribu kabisa. Siku yakikufika utajuta kazaliwa. Tuambie utatumia mbinu gani kujikinga na majanga ya kiafya?Hivi hakuna namna ya kujitoa NHIF kwa Watumishi wa Umma?
Kama uwezekano upo naombeni utaratibu
Toto sa hv 120k ama nn? Sijaelewa?Toto ni aidha umlipie mtoto 120,000 shuleni au Aunganishwe kwenye kifurushi cha kuanzia laki 504000 cha baba mama na mtoto.
Wanacheza na probability za odds za mkubwa kuugua Ni kubwa mno kuliko kijana ama chini ya 35Daah wameweka vifurushi ili wasikatike kwa Wazee wameweka gharama kubwa kama vile hakuna kitu wamechangia kwenye wenye umri mdogo ambao magonjwa ni kwa kiasi kidogo gharama ni ndogo yaani Serikali inaanzisha kitu kama Kampuni sio kutoa huduma ni faida kwa kila wanachoanzisha...
Najua wanafanya hivyo hao wakubwa sehemu zingine ndio wanachangia kidogo maana wamechangia mifuko mingi ya Serikali mpaka kufika hapo nachomaanisha wazee hawasaidiwi kitu chochote kwenye Nchi yao wakati wenzetu wanatunzwa wazee sisi matibabu tuu mtihani...utasikia tuna gesi,madini sijui wanyama na mbuga zote sasa faida ya kuwa na vitu vyote hivyo kwa Wananchi ni nini?Wanacheza na probability za odds za mkubwa kuugua Ni kubwa mno kuliko kijana ama chini ya 35