The Burning Spear
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 8,551
- 20,346
MASHARTI 10 KWA SERIKALI BATILI, HARAMU NA KATILI YA SAMIA KABLA YA TAREHE 09/12/2025
1. Serikali ikabidhi miili ya wapendwa wetu ili tuwazike kishujaa. Mwili usipotezwe wala kuchomwa moto Wazo Hills au kuzikwa kwenye makaburi ya siri kama mnavyofanya sasa hivi.
2. Serikali itumie kodi ya Wananchi (Pesa zetu) na iwape familia husika ili kugharamia mazishi ya wapendwa wetu.
3. Walioumizwa na majangili waliotumwa na serikali batili na haramu watibiwe bure na wapewe matibabu mazuri bila kusumbuliwa.
4. Waliohusika na mauaji ndani ya Tanganyika wakamatwe wote haraka na waoneshwe mubashara kwenye Tv na mbele ya waandishi wa habari wa kimataifa wakitajwa majina na walipotokea.
5. Waliohusika kwenye mchakato mzima wa kupanga mauaji ya raia wasio na hatia wajulikane wote kwa majina yao.
6. Mkuu wa Majeshi (CDF), IGP na Mkurugenzi wa usalama taifa wote wajiuzulu nafasi zao kwa kushindwa kuwajibika kwa kulinda nchi na wananchi jambo ambalo ndio waliapa kufanya. Hii pia iwahusishe wote walioshiriki katika njama za kuteka na kuua raia. Majina yao mnayo na sisi tunayo.
7. Watanganyika wote waliotekwa na kupotezwa warudishwe wakiwa hai.
8. Watanganyika wote waliopewa kesi feki za Uhaini na Ugaidi(kesi za kubuni/kutengeneza) kwa nia ovu waachiwe haraka sana bila masharti yoyote na waliohusika kubuni au kutunga kesi hizo au kushiriki kwa namna yoyote wakamatwe mara moja.
9. Uchafuzi feki na batili iliyofanyika ifutwe mara moja na Samia aachie ngazi haraka maana hatambuliki kama rais kwa mujibu wa katiba ya Tanzania. Hakuchaguliwa bal amejiteua, Katiba haina rais wa kujiteua.
10. Bunge feki ya sasa ivunjwe na Serikali ya mpito iundwe chini ya usimamizi wa UN hatimaye mchakato wa Katiba mpya ianze mara 1.
NB: Tunajua huwa mnadharau maoni ya Umma kama kawaida yenu huku mkishirikiana na viongozi wa kidini hao waliokosa uhalali, vyombo vya habari zilizokosa maadili, watu tuliowapa umaharufu pamoja na kikundi cha wachache wanaotafuna nchi yaani wanamtandao. Taifa hili ni letu sote sio mali ya kikundi au familia. Yasipozingatiwa tarehe 09/12/2025 tutaanza maandamano yasiyo na kikomo kudai haki na uhuru wa Tanganyika.
Imetolewa na waratibu wa Maandamano Kitaifa kutoka kila mkoa wa Tanzania.