Hiyo sera wakishaitoa wanaifanyia nini ikiwa serikali inaongozwa na CCM? Wewe unayeona magari ya serikali ni petty issues ni kwa kutokujua kwako namna yanavyotumiwa vibaya na namna yanavyoigharimu serikali kwenye service.
Kama hizo uliziona ni blah blah basi hakuna maneno utakayoambiwa zaidi ya hayo ukayaona yana maana kwako. Tatizo lako ni kuamua kuishi kwa mazoea kwa kuwa una imani kuwa kuishi kwa kufikiri ni gharama.
Mkuu unakaugonjwa kanakoitwa c
hademaosis changiuim fever, kaugonjwa ka kutaka mabadiliko kwa gharama yoyote bila kujua unakoelekea.
Actually si vibaya kutaka mabadiliko maana ndiyo tabia ya binadamu, akini mabadiliko for its own sake inabidi uwe reckless kutaka hayo mabadiliko yasiyojulikana.
Chama chako hakijaonyesha ukomavu wa kututia moyo kuwa kinaweza kuendesha gari kubwa linaloitwa serikali ya JMT.
Kwamba gari haliendi vizuri, hilo ni muafaka , kila mtu anajua hilo, kubadili dereva? leseni yako bado haijaturidhisha.
Hatutaki kuishia mtaroni, mtaro wa kisiasa na kiuchumi.
Kama ni matumizi ya pesa basi tungeona mfano mzuri wa ile hela ya Sabodo, watu wanawapa hata wake zao tenda kwa milango ya nyuma!
Maskandali tele humu JF, wala haututaki kuzisikia zinaletwa na nyie wenyewe ndani ya chama chenu.
Pamoja na yote sioni kiongozi, nasema sioni kiongozi ndani ya chama chenu mwenye uwezo wa kutengeneza sera itakayoeleweka na wananchi wote Tanzania.
Kutoa lawama kwa sauti kali na kunyoosheana vidole, hilo hata mtu asiyeenda shule anaweza
Ukitaka kujua , leo tunafuata sera zilizo wekwa na Baba wa Taifa, hata kama zimechakachuliwa!