MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Tangu Rais mstaafu Mh JK amuombe Raisi Magufuli awafirikirie kwa jicho lakipekee vijana wa ccm wanaoshinda mitandaoni usiku na mchana kwa sababu walikisaidia sana chama kwenye uchaguzi basi kumekua na paparapapara kwenye mitandao ya kijamii, watu wanatukana, mbaya zaidi kila kitu ni chadema, Chadema!
Ni mshangao mkubwa sana kuona ni chama kimoja tu kinachoshambuliwa, ajenda ya vijana hawa wa ccm ni Chadema tu na viongozi wao lakini Tanzania kuna vyama vya siasa zaidi ya 20! Sawa na mashabiki wa Simba SC ambao ajenda yao kuu kila siku ni Yanga tuu! Yaani watu badala ya kukaa kukijenga chama Chao vizuri kujiimarisha zaidi kuziba nyufa zilizobomoka badala ya bila kujijua wanajenga na kukikuza chama kingine, maana kumshambulia mwenzio ndio kwanza unamfanya awe maarufu, kumshambulia sana unamfanya ajiimarishe zaidi maana hata kiini cha homa flani kikizoea dawa hujenga Resistance ya dawa na kua Sugu.
CCM NA MASHAMBULIZI BUTU KWA CHADEMA.
Hii system ya mashambulizi mitandaoni ilitumiwa sana na wana ccm nyakati zilizopita, lakini pamoja na mashambulizi yale bado Chadema walizidi kujizatiti na kuongeza umaarufu zaidi, Maana ukiangalia hadadi ya wabunge wa Chadema kwa sasa ni wengi kuliko awamu iliyopita.Kuna hata waliodiriki kusema kua Chadema kitakufa hata kabla ya uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 2015 lakini chama kionekana kwanza ndio kinamea, hata baadhi ya watabiri kua Chadema kitakufa lakini wao ndio wakawa wa kwanza kufanya kisiasa. Huu sio ubutu ni nini?
JINSI CCM WANAVYOPOTEZA FURSA KUKIKUZA CHAMA CHAO.
Kwa awamu hii ambapo Rais kutoka chama Chao ameamua kutekeleza ilani yao kwa nguvu zote ni ajabu sana kuona wao wanaenda kinyume na matendo yake, kama Rais alisema kwamba hataki kusikia vijana wanashindia kwenye pooltables badala yake waende kuzalisha, Lakini kushindia mitandaoni kutwa nzima tena kwa wasomi ni sahihi kuliko wale wa pootables? huku mitandaoni kuisema Chadema tu ndio uzalishaji gani kama sio umbea? Je, ni kweli kila kijana ndani ya ccm anategemea kuchaguliwa kua DC? Kwanini wasijizatiti katika kuyaenzi na kuyafanyia kazi yale anayoyasema Mh Rais? Kumshambulia Chadema na failed techniques kuna faida gani kwao? Kama wanafahamu kua watanzania ni waelewa kwanini wasitumie njia nzuri kuwahubiri watanzania maendeleo zaidi ya kukaa kwenye mitandao kuhangaika na Chadema tu?
KWANINI CHADEMA TU?
Kwa wale wasomaji na watumiaji wa mitandao hii ukiangalia kwa umakini utaonga karibu nusu ya mada zote ni mashambulizi dhidi ya Chadema na viongozi wake! Kwa mwenye akili ataona kabisa hii ni faida kubwa sana kwa Chadema tofauti na wapinzani wao hawa wanavyowaza.
USHAURI
Vijana kwa sasa wanatakiwa kujielekeza kwenye uzalishaji kwa nguvu zao mbichi badala ya kushindia mitandaoni kupoteza muda kwenye mitandao! Sijui ni nchi gani duniani vijana tena productive kabisa wenye elimu ya kutosha muda wote wanashinda mitandaoni kutukana tu na kuandika vitu ambavyo havina maana.