nimefurahi sana malila kutukumbusha sisi tuliosahau kuwa na viwanja na mashamba, mimi pia nahitaji shamba ila lipo eneo gani hasa, ukitoka dar kwenda mkuranga kuna temeke, mbagala............. mkuranga, je kama liko kando ya barabara ni mbali na road reserve maana kuja kuambiwa ondoka tunapanua barabara inakuwa haipendezi tupetaarifa kamili, tuwasaidie na wengine
Mkuu haya mashamba hasa lile la km 78 liko karibu na shamba la AMADORI lililoko karibu na mto au inakuwaje?tupeane mwelekeo zaidi man.
Jamani hapo Kisarawe tu kuna mashamba mazuri kabisa kwa laki moja tu kwa ekari na ni karibu sana kutoka Dar, kama sikosei si zaidi ya km 40.
Kweli kabisa mkuu unachosema,lakini hapo kisarawe unaposema kuna maji ya kufanyia kilimo mkuu? kama ni shamba kiwanja sawa. Kama kuna mashamba mbona watu wanakwenda kununua morogoro na wanapita mapori yote humo njiani ( mdaula,mikese nk),wanakwenda Kilindi kulima kwa nini wasilime hapo Vigwaza.
Mkubwa,sasa hivi shamba zuri ni maji,biashara ya kutegemea mvua inatulostisha mkuu.
Nimekusoma mkuu
Wakuu wakuu wakuu, hebu subirini kwanza. Yani Mnazungumza hela nyingi sana nadhani bora tuzichangie mawazo. Msiwe na wasiwasi Hamna utapeli hapa wakuu. Wenye kuuza wanauza na wenye kununua wananunua. Tutachofaidika nikua tutachangamsha biashara ya mashamba na kufundisha watu haki za mali (Financial Literacy). Lakini kabla ya kufanya kuna maswali itabidi tuyajibu, ili tusiwapatie watu pesa halafu huenda mtu ni mbadhirifu itabidi afundishwe mbinu za ubanizi kidogo (sio ubahili hapana).
Tutaleta customer service bongo. Nimeshawahi kufanya real eastate na kwenye management team yetu tunawatu amba wanaelewa na ni wabongo wenzetu ingawa timu yetu inawatu kutoka nchi tofauti yani tuwaletea expriance from deferent angles.
Ikiwa kuna mtu amevutiwa na kufanya hilo jambo (Ujasirimali wa real estate hata sasa hivi ndio biashara yako tunakuhitaji), naomba unitumie notification with a heading GREEN INVESTMENT, hali , au face book Yasser Mziba. Nitazungumza na ED wa JF, he's cool dude.
We gotta do this guys. Kila mtu atanufaika. tutawapa watu kazi. Mwana JF yoyote anakaribishwa. Itakua ni project kwa hiyo inamaana itakua na mwanzo na mwisho. halafu tunapima matokeo. Wazee wenye mashamba yenu kwanza nawashauri msiuze. nakama mkiuza tafadhali tutumieni mimi na watako jitokeza. Tutaonyesha namna ya kufanya customer services katika finance, alafu mabenki yatakopi model.
Malila,Laki 6 kwa heka mkuranga bado ni nyingi mmno,nimenunua heka 90 elfu,heka 20 kwa 1.8million,hazina mazao ,ni uwala tu, na miembe michache,lilikuwa limepandwa nanasi,miaka 3iliyopita mkuranga,kuna mto,65km from BP roundabout kilwa Road.
nadhani bei hiyo ni ya shamba lenye mazao yakudumu mengi,ila kwa msolwa mashamba mengi yalio na mazao ya kudumu ni KOROSHO ambazo uzalishaji wake mdogo,.
nadhani kwa bei hiyo inabidi utufafanulie shamba lina mazao yapi na uzalishaji ukoje?
Mkuu Malila nimekusoma.
mimi shamba lipo 13km from mkuranga center,eneo linaitwa KISE njia ya kwenda BUPU ,huko bei bado ni poa,ila naweza kufika kwa corola,na kuna vihice sh 2500 from mbagala.sijawahi kuvitumia ila nimeshawahi kumtuma mtu apeleke pesa na kukagua kazi alipanda dalala amesema haikumchukua muda kufika huko kutokea mbagala.
nafikiria kwenda mbele zaidi,maeneo ya nyamisati.
Moja lipo km 78 toka Dsm kwenda Mkuranga,lina mikorosho,linapakana na mto usiokauka,usafiri wa daladala toka mbagala upo. Halifai kwa kilimo cha mazao ya nafaka,linafaa kwa matunda na ufugaji wa aina zote. Bei kwa eka laki sita. La pili ni kama km 60 hivi,linafaa kwa kilimo cha mazao yote na ufugaji,lipo kando ya barabara na usafiri wa daladala upo,ukubwa yapata eka 10 hivi na lina kibanda kibovu na lina mazao ya pwani,bei 5M. Hili lina maji ya msimu wa masika tu. Haya mashamba nimeyaona.
Moja lipo km 78 toka Dsm kwenda Mkuranga,lina mikorosho,linapakana na mto usiokauka,usafiri wa daladala toka mbagala upo. Halifai kwa kilimo cha mazao ya nafaka,linafaa kwa matunda na ufugaji wa aina zote. Bei kwa eka laki sita. La pili ni kama km 60 hivi,linafaa kwa kilimo cha mazao yote na ufugaji,lipo kando ya barabara na usafiri wa daladala upo,ukubwa yapata eka 10 hivi na lina kibanda kibovu na lina mazao ya pwani,bei 5M. Hili lina maji ya msimu wa masika tu. Haya mashamba nimeyaona.