Mashaka matupu siasa za bongo

Jul 3, 2012
92
13
Wakati wa Uchaguzi wa mwaka 1995, NCCR Mageuzi kwa upande wa bara, na CUF kwa upande wa Zanzibar vilionekana kuwa ni vyama shindani vyenye nguvu. Mambo hayo yamebadilika hivi sasa, ambapo CHADEMA kinaonekana kua chama shindani chenye nguvu zaidi BARA. Lakini swali ambalo ninajiuliza katika hali ya ushindani wa kisiasa, je Nini haswa tofauti kati ya vyama vyetu yaani CCM, CHADEMA, CUF, TLP, UDP na vinginevyo?
Katika hali ya kawaida kabisa, ingetegemewa kwamba vyama tofauti hua na sera tofauti. Kutokana na utofauti huo wa kisera, lingekua suala gumu sana kwa baadhi ya watu, haswa wanaoshindwa chaguzi za vyama vyao, kubadili vyama kama nguo wakati wa kipindi cha uchaguzi. Je, tuamini kwamba vyama hivi vinafanana kisera, au kwamba kuna viongozi ambao wana tamaa ya madaraka? Vipi kuhusu yale mamia ya wanachama wanaopewa kadi katika mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa? Hua wanaelewa kweli sera za vyama husika, au wanavutiwa tu na hotuba?
Nafikiri umefika wakati kwa vyama vyote kufanya mambo kwa kufuata sera zao haswa, maana kwa hali ya sasa, kila chama kinahangaika na UFISADI, kila chama kinahangaika na UMASIKINI e.t.c., lakini muelekeo wa misingi ya kisera haswa, kama ni ya kiliberali, kisoshalisti na kadhalika haieleweki. Hivyo, japokua leo watu wanasema wanachagua CCM, CHADEMA,NCCR, CUF or TLP, ukweli ni kwamba, ukiwaambia nini maana ya kuchagua vyama hivyo, utapata majibu mbali mbali ya kisiasa, lakini si ya KI-MRENGO wa vyama husika. Hili ni ombwe katika siasa za tanzania, na elimu ya kisiasa kwa watanzania, ambalo tusipolishughulikia, siku zote tutakua tunalumbana kivyama, na kusahau ki sera, na mwisho wa siku, vyama hivi tutavipa kura au kuvinyima kura kutokana tu na makundi ya watu walioko, lakini si kutokana na mpangilio wao wa kisera.
Naomba kuwakilisha
 
Back
Top Bottom